John Henche ataka Serikali kutoa ripoti ya Vifo vilivyotokana na mgomo

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
MKiti wa vijana CDM kaitaka serikali kutoa ripoti ya idadi ya vifo kutokana na mgomo wa Madaktari, na iwawajibishe wote waliohusika na vifo hivyo. Source: Radio 1 news.

MIE NASHAURI PM AWE WA KWANZA KUNGO'KA Maana kama sio yeye alikosa busara na dira alipowapa vitisho, tatizo lisingekuwa kubwa na kudumu muda hivyo. PM AWAJIBIKE WA KWANZA, wengine wafuate.
 
Heche asitake kufukua makaburi, hizo ni chokochoko zisizo na maana. Au ananataka tuamini kwamba CHADEMA ndio waliratibu mgomo wa madakatari?
 
anataka tu uwajibikaji wa viongozi hawa wasio na hisia au uwajibikaji mbali na visingizio.
 
Heche asitake kufukua makaburi, hizo ni chokochoko zisizo na maana. Au ananataka tuamini kwamba CHADEMA ndio waliratibu mgomo wa madakatari?

Hili lilikuwa ni tatizo ambalo limewakosesha watanzania wenzetu maisha, lingeweza kumkuta mtu yeyote hata wewe. Fikiria kama ungepata ajali wakati huo wa mgomo na matibabu yako yakawa ni lazima yafanyike muhimbili je ungekuwapo hadi leo???? Kila mtanzania mwenye akili timamu lazima awe concerned na hili jambo na hatua zichukuliwe ili kuhakikisha hali kama hii haijurudii tena huko siku za mbeleni. Watu wenye mawazo kama wewe ndo wameteka nyara maendeleo ya nchi hii, kila kitu kwao ni ushindani na ushabiki tuuuuu wa kisiasa, halafu hata siasa zenyewe hamzijui na mna uelewa mfinyu sana. AIBU!!!!
 
Back
Top Bottom