Jogoo wa kienyeji halisi akiwapanda chotara aina ya kuroiler ,je, mambo haya yanaweza kutokea?

TANZANIAN NINJA

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
441
496
Heshima kwenu mabibi na mabwana,kuroiler ni aina ya kuku chotara ambao wanasifa za kienyeji kwa kiasi fulani na sifa za kuku wa kisasa kiasi fulani hasa kwenye rangi ya mayai hata wakati mwingine kiini cha yai huwa sio chanjano kama wale wa kienyeji,mimi nataka kuwatumia kuroiler wapandwe na jogoo la kienyeji je, kuku watakao zaliwa wanaweza kuwa na sifa zifuatazo?

1. Kutaga mayai madogo kwa umbo kama ya kienyeji

2. Kutaga mayai yenye ganda jeupe kama ya kienyeji

3. Kutaga mayai yenye kiini cha njano

4. Kuhatamia na kutotoa kama kuku wa kienyeji

Asante kwa kusoma na karibu kwa mchango wa elimu.
 
Hutaga mayai ya kawaida kama aliyokua anataga hapo awali ila yanakua na sifa moja tu kua yani mbegu hivyo unaweza kutotolesha. Kuhusu kulalia kuroiler asili yake hua haatamii mayai na iyo haibadiki sababu jogoo
 
asante mkuu ila naona kama ujanielewa kidogo,nazungumzia kuku watakaozaliwa baada ya kupandisha jogoo la kienyeji kwa mtetea wa kuroiler.
 
asante mkuu ila naona kama ujanielewa kidogo,nazungumzia kuku watakaozaliwa baada ya kupandisha jogoo la kienyeji kwa mtetea wa kuroiler.
Utapata kuku wa aina mbili. Kuna wengine watakua na sifa ya kulalia yan watarithi kwa baba na wengine watarithi kwa mama yao ila utapata mbegu nzuri sana.. hii mm mwenyewe naitumia
 
Hutaga mayai ya kawaida kama aliyokua anataga hapo awali ila yanakua na sifa moja tu kua yani mbegu hivyo unaweza kutotolesha. Kuhusu kulalia kuroiler asili yake hua haatamii mayai na iyo haibadiki sababu jogoo
Mkuu vipi Sasso wanaweza kuatamia?
 
Utapata kuku wa aina mbili. Kuna wengine watakua na sifa ya kulalia yan watarithi kwa baba na wengine watarithi kwa mama yao ila utapata mbegu nzuri sana.. hii mm mwenyewe naitumia

nafikiri hata sifa za mayai zitategemea kuku huyo karithi sifa za baba au mama sindivyo mkuu,asante sana
 
Saso hawatamii
Na hivi tetea wa Sasso wakifikisha umri wa kutaga wale jogoo wake watakuwa wameshapevuka kiasi kwamba wanaweza kupanda?
Au ndio inabidi kutafuta jogoo wengine wakubwa?

Nimefuga ila nna wasi wasi kweli kama tetea wakifika umri wa kutaga jogoo watakuwa Bado!

Hilo liko vipi kwa uzoefu wako?
 
Back
Top Bottom