Joe Nanauka CHADEMA/UKAWA kupita bila kupingwa Mtwara Mjini, Mburushi koko ajaza madudu

Kama hicho kinafanyika lazima kuna sababu,Chama hakiwezi kumpitisha Mgombea kirasi hivyo kuna sababu obvious. pia kushinda ndani ya Chama ni tofauti na kushinda nje ya Chama kwenye wananchi wengi.Naamini Mpendazoe ni maarufu nje ya Chama kuliko aliyepita,pia kumbuka kuna fitna ktk kura za maoni.

Well said,,, nimependa majibu yako mazuri, hata CCM kumbe wakifanyaga hivi ni kutimiza wajibu na taratibu za chama chao na si vinginevyo... thanks
 
MPENDAZOE KISHAPU KAPATA KURA 11 mwenzie kapata kura 290 mmemkata eti mpendazoe agombee,,, mnarudia yaleyale mliokuwa mnalalamikia CCM kweli kumbe ni CCM B
chadema inaona mbali mno kuliko unavyofikiria .
 
Mm naomba mwana ccm yeyote anishawish nmpgie kura magufur(kwann nmpgie kura magufur?)
 
Hili jambo si jema kwa kweli.
11 kwa 290 hakuna kushabihiana kabisa hapo. Wanakishapu wana haki ya kumkataa.
Kama kuna namna ya kurekebisha hili jambo ni vizuri likafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo. Watu wanaimani na chadema wasivunjwe moyo.
Mkuu tayari tumesharudisha na fomu, hiyo ndo imetoka hivyo walikuwa wapi tangu waliposikia kuwa mtu wao amekatwa? Mkuu hiyo janja ya ccm tumeistukia wacha Mpendazoe akamng'oe mwarabu hatuna mswalie mtume hapa! Huyo mtu alikuwa pandikizi la Mwarabu ili siku ya siku asirudishe fomu au ajitoe kwamba amekosa hela ya kupigia kampeni! Intelijensia ya CHADEMA iko juu sana!! Hivi ulisikia fedha ilyokuwa imemwagwa pale Kishapu kwa ajili ya kumpitisha huyo jamaa? Wote wanaojinyeanyea ni watu walioandaliwa na Mwarabu akidhani kwamba labda mtu wake atarudishwa kwenye kinyang'anyiro!!
 
Nidhahiri wimbi la mambumbu ndani ya ccm linadhihirika baada ya Mgombea wa ccm Mtwara Mjini kuwekewa pingamizi na kijana hodara wa CHADEMA/UKAWA Ndigu Joel Nanauka,

Msingi wa Pingamizi hilo upo katika udanganyifu wa mgombea wa CCM katika ujazaji fomu,

Sehemu inayohoji kuwa "Uliwahi kufikishwa mahakamani?" Yeye amejibu kuwa HAPANA,

Ukweli nikuwa Murji ni mdau mhimu wa mahakama nchini ambapo ameshafikishwa mahakamani kwa kesi nyingi tu za jinai, na mpaka hii leo ana rekodi nzuri tu yakuwa mbunge wa Kusini aliyefikishwa mahakamani kwa kesi ya jinai ya kuchochea maandamano ya gesi.

Kosa hilo la kujaza uongo linaangukia katika kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge mtwara mjini na kuacha nafasi hiyo kwa mgombea pekee wa chadema na ukawa

Wewe si ndio bingwa wa kushambulia wanaopata ushindi wa mezani?
 
Mbona mbowe naye ana hatia ya jinai, laza anyofolewe pia.

Hapo ndo huwa tunatoa somo sasa.
Kwa mujibu wa sheria namba 67(1) yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sifa za Mgombea Ubunge ni zifuatazo:-
Awe Raia wa Tanzania
Awe na Umri wa miaka 21 au zaidi
Awe anajua kusoma na kuandika kwa kiswahili na kiingereza
Awe ni Mwanachama na ni Mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa na
Awe hajatiwa hatiani na mahakama yoyote kwa kosa la KUKWEPA Kodi ya Serekali katika kipindi cha miaka 5 kabla ya tarehe ya uchaguzi.

Pia kuna kukosa sifa ya kugombea Ubunge
Mwongozo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya Tano ya mwaka 2015
Kifungu cha 5.3 kinasema hivi:-
Hata kama mtu anazo sifa zote za kugombea hataruhusiwa kugombea Ubunge kama:-
i) Ni raia wa nchi nyingine; au
ii) Kwa mujibu wa Sheria inayotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imethibitishwa kwamba mtu huyo ana
ugonjwa wa akili; au
iii) AMEHUKUMIWA na mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupewa Adhabu ya KIFO au ya KUFUNGWA GEREZANI kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambata na utovu wa UAMINIFU; au
iv) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; au

na kuendelea hadi kipengele cha (ix)

Mwisho kuna Angalizo!
Nalo ni;
Mtu aliyepewa adhabu ya KULIPA FAINI au KIFUNGO na akalipa FAINI hazuiwi kugombea. Iwapo atapewa adhabu ya kulipa faini na akashindwa na akatumikia kifungo na kukimaliza kabla ya Siku ya Uchaguzi anaruhusiwa kugombea. Mtu hataruhusiwa kugombea kama amehukumiwa na anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi 6 gerezani.

Hivyo ndivyo sheria inavyosema.

Sasa Fomu ya Kugombea Uteuzi wa Mbunge kipengele A. Namba 7 kinauliza hivi:-
Je umewahi kushtakia na kuhukumiwa kwa kosa la jinai? *NDIYO/HAPANA
Kama jibu ni ndiyo eleza mambo yafuatayo:
(a) Makosa au kosa uliloshtakiwa nalo
(b) Tarehe na mahali ulipohukumiwa
(c) Adhabu uliyopewa

Kwa sababu hii uwe umeshtakiwa ni lazima ukiri kuwa uliwahi kushtakiwa kwa kosa la Jinai! Hata kama hujahukumiwa bado ni sharti useme kuwa Umehukumiwa. Hapo utarudi kwenye kipengele (b) tarehe uliyohukumiwa! (c) Adhabu uliyopewa unataja na kama ulilipa faini unasema hapo! Ndo tunarudi kwenye MWONGOZO WA TUME SURA YA TANO kipengele cha 5.2 na 5.3 kinatoa tashwishi hii!
Mbarikiwe sana!
 
Mbona mbowe naye ana hatia ya jinai, laza anyofolewe pia.

Ndg! Tumia akiri basi kidogo.
Siokwamba tume haitaki watu tu ambao hawajawahifikishwa mahakamani, tume inachotaka jibu ni ndiyo au hapana. Sasahuyu kajibu hapana wakati ukweli ni ndiyo.
 
Back
Top Bottom