Jeshi la kujenga Taifa (JKT), linakanusha taarifa zilizotolewa kwa umma kupitia mtandao wa Jamii Forum, tarehe 11 machi 2016 kuwa, JKT limeanza mchakato wa kuchagua vijana mikoani na wilayani kujitolea kwa nia ya kujiunga na mafunzo ya JKT.
Aidha tangazo hilo linasomeka kuwa mwombaji awe mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 23 kwa wenye elimu ya kidato cha saba hadi cha sita, miaka 18 hadi 26 kwa wenye stashahada na miaka 18 hadi 35 wenye shahada na kuendelea. Pia asiwe ameoitia chombo chochote cha ulinzi na usalama.
Tangazo hilo kwa umma sio sahihi na halijatolewa na uongozi wa JKT kama linavyosomeka na kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hadi tarehe 15 Machi 2016 JKT halijaanza mchakato wa kuchukua vijana wa kujiunga na mafunzo ya kujitolea. Muda mwafaka utakapowadia , wananchi watajulishwa rasmi kupitia vyombo vya habari vitakavyoainishwa.
Aidha JKT linazidi kuwakumbusha wananchi kuwa utaratibu wa kuwapata vijana wa kujiunga na JKT haujabadilika. Maombi yanaanzia wilayani na mikoani kwa kutoa uteuzi wa vijana,
Kulingana na nafasi zitakazotolewa kwa kila mkoa. JKT linawaomba wananchi wote kuzingatia utaratibu huo muda utakapowadia.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 15 Machi 2016
Umesomeka,uku kwangu Tulya,vijiji vyote vilishaanza nisumbua:kule migilango,doromoni,tulya!walishaanza nisumbua kwa maswali ya lini nafasi za jkt zitatoka!nashukuru kwa ufafanuzi?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.