John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
Ukisoma mahojiano na JK kwenye The Citizen, :
Bonyeza hapa: http://www.thecitizen.co.tz/newz.php?id=1964
Ngoja nijaribu kuingia katika akili za Mkuu wetu wa Nchi kutokana na kuyatafakari mahojiano hayo:
Mosi; Rais anampango wa kuvunja baraza la mawaziri lakini asingependa iwe ni kwa msukumo toka nje-ndio maana kwa sasa ameuita uvumi
Pili; Rais ana mpango wa kupunguza ukubwa wa baraza la Mawaziri- lakini hataki ionekane ni mwa msukumo kutoka nje, anataka iwe bayana kuwa ni kwa kuwa wameshatimiza malengo
Tatu; Rais aliunda kamati ya Bomani kuridhisha tu upinzani(wale wakina Tomaso wasioamini) lakini ukweli ni kuwa ana imani na ripoti ambayo wakina Masha tayari walishampelekea.
Nne; Rais anafahamu kuhusu mikataba yote ambayo imesainiwa na pengine ina baraka zake kwa ukamilifu wake na pia anaamini hakuna mazingira ya rushwa hata kidogo katika uingiwaji wa mikataba hiyo.
Tano; Rais hataki kabisa kuwatafuta wachawi- hivyo chini ya Rais huyu tusahau kabisa suala la kurekebisha makosa ya zamani
Sita; Rais anaridhishwa kabisa na hali ya Taifa- kisiasa, kiuchumi na kijamii; anaona mambo yote ni safi kabisa! Katika hii miaka miwili, Rais anaona tumekwenda kwa Ari, Nguvu na Kasi Mpya kwenye Tanzania yenye neema kama alivyopanga na kwamba Misingi ya Maisha bora kwa kila Mtanzania imeshajengwa. Kuanzia mwaka ujao na kuendelea ni wakati wa Ndege kupaa ..abiria fungeni mikanda.
JJ