IronBroom
JF-Expert Member
- Jun 12, 2008
- 521
- 36
Tatizo na jamaa wengine wamejenga chuki isiyokuwa na maana kwani marais wengine waliopita walifanya mara ngapi.
Incredible!
Tatizo na jamaa wengine wamejenga chuki isiyokuwa na maana kwani marais wengine waliopita walifanya mara ngapi.
Mkuu jiulize,
Kwa nini JK achukiwe why? kwa nini? Kuna watu wana ajira zinazolingana na uwezo/elimu yao na wengine wanafanya kazi kwa ufanisi sana, sio wezi na si wafuasi wa mtandao wa mafisadi na wanamchukia JK why? kwa nini?
Mkuu Said jiulize na tuambie hapa!!
As long as Mlishamuudhi ES kwa kumfungi mjue kuwa hamtopata breaking news tena
tutabaki ni hizi speculations zisizo na kichwa wala miguu
Imetolewa mara ya mwisho: 22.11.2008 0010 EAT
Hata katika ziara za Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, matukio ya wakuu hao wengi kuonekana wanafanyakazi kwa kukurupuaka yalionekana huku malalamiko ya wananchi katika vyombo vya habari wakati fulani yakiwahusisha wakuu hao katika tuhuma kama vile kukumbatia wawekezaji wanaonyanyasa wananchi, kushindwa kwao kuwasikiliza wananchi na kutatua shida zao na wengi pia kukosa mbinu madhubuti za kiutawala.
Wakuu hawa wa wilaya wanafanya kama anachofanya yeye mwenyewe JK. Wanawakumbatia matajiri....kama yeye alivyo na anavyoendelea kuwakumbatia..........Hayo mabadiliko sijui yataleta nini kipya.
"sasa turudi kwenye ilani ya uchaguzi....ambayo aliisoma na kuielewa kabla ya kugombea"
Hii mbona alishaikana siku nyingi.... alishasema yeye hakuhusika katika kuiandaa wala kuweka ajenda.... kwa kifupi kainawa kitambo!
mmmhh kweli nam-miss sana Mkuu FM ES
Hata Mkapa aliikana ilani yake akisema kuwa haitekelezeki.
..atakuwa kiongozi wa kwanza kuikana ilani iliyomuweka madarakani ....maana chama chochote duniani kabla ya uchaguzin huandaa ilani ambayo hutumia kwenye uteuzi kwa kutafuta miongoni mwa wanachama wake wenye uwezo wa kuitekeleza huisoma na kuamua kugombea au la....
sasa akikataa ilani atataka tumpime kwa kipimio kipi.............
...sasa hivi wanamkakati wa kikwete wanakuja na hoja dhaifu kuwa kikwete hajashindwa ila wasaidizi wake ndio wanamuangusha....kama mnavyojuwa kikwete amekuwa mwepesi sana kupokea sifa hata pale "TAIFA stars inaposhinda 1-0"....hapo hapo kutaka kujiweka kando na ,mambo yote mabaya yanayofanyika.....simply yeye aonekane mzuri ..wabaya waonekane wengine..."
watanzania tunaweza kuamua moja HILI SUALA LA EPA NA MENGINE ..hata kama yangekuwa hayapo...je still jk analo lipi alilolifikia kimaendeleo ndani ya hii miaka 3....zaidi ya kila wakati kuleta mazingaombwe ya kuteka akili za watu???
natoa changamoto kwa wahariri wa magazeti waanze kumuhumu kikwete kwa ahadi zake..zinazobebwa ba kauli mbiu za "KASI MPYA,NGUVU MPYA NA ARI MPYA"..," MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA "..,: " TANZANIA YENYE NEEMA INAWEZEKANA'"....hizi ni kauli mbinu ambazo ghafla zimekuwa mwiba ..na kuzitamka mbele ya kikwete sembuse yeye mwenyewe kuzitamka ..imejeuka kama uhaini..au kumkebehi..mkuu...
sasa turudi kwenye ilani ya uchaguzi.....ambayo aliisoma na kuielewa kabla ya kugombea ..aliiamini kuwa anao uwezo wa kuitekeleza...tulipohoji alipofikisha mwaka mmoja ikulu..watu walimrushia taulo jeupe wakisema tunamuonea tumpe muda....wakasahau nyota njema huonekana asubuhi...........sasa tuanze kuangalia ameshatekeleza ahadi ngapi na kwa asilimia ngapi..akiwa tayari ana miaka mitatu ikulu????.......hasa ukizingatia kama yeye mwenyewe anavyosema ..kuwa he was president in waiting for ten years.....
kwa hili la wakuu wa wilaya jamani wacheni afanye mabadiliko,huko wilayani kusema za ukweli kumeoza,wilaya nyingi zimeshikiliwa na kina mama,wachache wao wanajitahidi angalau angalau lakini wilaya zilizo nyingi zina watendaji dhaifu sana. Singependa kuzitaja lakini wanachi wa wilaya hizo ndio mashaidi wa jinsi wilaya zao zinavyoendeshwa i.e korogwe,lushoto ,hai wapate watu wa shemu hizo utapata muziki wake.
Kwa hapo jk nakupongeza!
Kwa kweli Watanzania tunataka kuzugwa. Kifupi hii habari nzima imejaa usanii wa hali ya juu kutaka kuwazuga Watanzania. Mabadiliko yanayotaka kufanywa ni remote control ya mtu aliye nje ya utawala anayetaka kujaribu kuonyesha kwamba bado ana nguvu katika utawala wa sasa na hilo ni hatari sana kwa wananchi wa Tanzania.