JK awasili Poland leo

Dah, yaani huyu mr President hadi vikao vya kupeleka wakurugenzi anaenda

www.theguardian.com/environment/2013/nov/13/warsaw-climate-talks-countries-ministers
 
Mkutano wa jumuia ya madola ushaisha? JK kala miguu ya kuku sijui...kiguu na njia...hana hata muda wa kukutana Na wenzie wa jumuia ya Afrika ya mashariki.

Ndo mana walimtenga mkawa mnalialia..kina m7 na paulo ni vichwa
 
Sasa mlitaka aende nani? Tumemchagua akatuwakilishe.nenda jk, nenda rais wetu mpendwa kachape kazi.nani hapa jf akiwa rais hatosafiri? Tuache unafiki,tena wengine wanaweza kuwa zaidi ya jk.
 
Ndo mana walimtenga mkawa mnalialia..kina m7 na paulo ni vichwa
Naanza kuliamini hilo la kumtenga. PK ana ujinga wake vita lakini huyo rais wetu amekuwa ni mzigo sana aisee. May be akina Mutogorwe wako right.
If I were to choose who to lead Tanzania between PK and JK, it's a no brainer!! I'll go with PK
 
Sasa mlitaka aende nani? Tumemchagua akatuwakilishe.nenda jk, nenda rais wetu mpendwa kachape kazi.nani hapa jf akiwa rais hatosafiri? Tuache unafiki,tena wengine wanaweza kuwa zaidi ya jk.

Kweli nenda Jk wetu tena kajenge ikulu pale Hollwood marekani huku wala hatukuhitaji nchi inajiendesha yenyewe. Nenda Jk hutubia taifa ukiwa visiwa vya malta au pale Brunei kwenye bembea na tutakusikiliza. Nenda Jk wetu ukirudi liambie taifa hujui kwanini marais wenzako wa EAC WAMEKUTENGA HUJUI KAMA NI CHUKI KWA TANZANIA AU WANAKUCHUKIA WEWE. Nenda Jk wetu.
 
Rais amepata safari ya juu kwa juu toka Sri Lanka na sasa yuko Poland kuhudhuria mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Alipita kwa muda Dubai jana na leo asubuhi kaingia Warsaw

Kwa tarhmini ya miaka mitano, Kikwete amefanikiwa kuwa Tanzania kwa mwaka na miezi tisa. Miaka mitatu na robo alikuwa nje ya nchi

Kikwete ni rais wa kwenye ndege
 
Hivi hiyo ni safari ya ngapi ? Maana rekodi zilikuwa zinaonyesha safari zake zilikuwa 357 !
 
Kwa tarhmini ya miaka mitano, Kikwete amefanikiwa kuwa Tanzania kwa mwaka na miezi tisa. Miaka mitatu na robo alikuwa nje ya nchi

Kikwete ni rais wa kwenye ndege

Eee bhana eee ! Kumbe ni hivyo ? Duh!
 
Akimaliza muda wake wa urais atachukua kalamu na karatasi aorodheshe nchi alizokwenda na kurudi mda wote wa urais.,
 
,Hongera baba ila toka ulipoondoka HUKU KWETU TUPO GIZANI,hatuna hata pesa ya kununulia mafuta ya taa,wanao tunalala giza,muhongo kasema matenki yanayoifadhia gasyamejaa uchafu, mpaka yaoshwe,hapa JF tungejitolea kuyaosha lakini tunaogopa kuwachongea wale waliopewa hiyo dhamana,tena wanalipwa kwa kipato chetu kilicho kidogo.
We wasalimie tu huko lakini haiyumkiniki huku kwetu hali si shwari baba.Ukija utuletee zawadi.
 
Back
Top Bottom