JK apuuzwa, mahabusu pia waachiwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ikiwa jana Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 2973,mahabusu pia wameachiwa. Ni taarifa za uhakika. Kati ya mahabusu hao waliofaidika na msamaha huo,wapo wateja wangu wawili. Ifahamike kuwa wafungwa hutofautiana na mahabusu. Mahabusu ni wale wanaoendelea na kesi zao. Wamenipunguzia kazi...
 
Nia yako hasa kwa hao wateja wako ni nini? Kuhakikisha wanakuwa huru, sio?
Lawyers! Sijui kama kuna hata mmoja huko peponi!
 
Kama nimemwelewa vizuri nadhani anakusudia kusema ameingilia mchakato wa kimahakama.

Hata hivyo hili la kuachia mahabusu (kwa msamaha wa rais!) kwangu bado haliingii akilini kwamba linaweza kufanyika. Maabusu wanasamehewa adhabu ipi ikiwa bado mahakama haijhasema kama wana makosa ama la na hata adhabu haijatolewa!?
 
Hili nila kwanza kutokea duniani na la kwanza Tz nazidi kuwa na wasiwasi na Jk pamoja na washauri wake maana sidhani kama unaweza kumsamehe mtu ambae hajulikani kama ana kosa ama la, mahakama hapo imesimama wapi? Maana ni kama imeingiliwa uhuru wake
 
Ikiwa jana Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 2973,mahabusu pia wameachiwa. Ni taarifa za uhakika. Kati ya mahabusu hao waliofaidika na msamaha huo,wapo wateja wangu wawili. Ifahamike kuwa wafungwa hutofautiana na mahabusu. Mahabusu ni wale wanaoendelea na kesi zao. Wamenipunguzia kazi...

Labda ni katika pilikapilika za kutaka kumfungulia na kumwacha huru Lulu anayetuhumiwa kwa mauaji ya Kanumba na wakati kuna tetesi za Ridhiwani Kikwete kumnunulia gari Lulu na kukutwa na messege muda mfupi baada ya kifo cha Kanumba inayosadikiwa kutoka kwa Ridhiwani. Hii Mkulu anatakiwa kutumia kila liwezekanalo kuinusuru familia yake kutoingia kwenye kashfa ya kesi hiyo ingawa haiwahusu moja kwa moja.
 
Ni kweli kuna jamaa mmoja alikuwa mlinzi wa kampuni flani bunafsi, kumbe pia alikuwa anajihusisha na vitendo vya ujambazi..akadakwa mwaka jana..alikuwa mahabusu tu ila leo nimemwona mtaani aliachiwa naye!
 
Ikiwa jana Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 2973,mahabusu pia wameachiwa. Ni taarifa za uhakika. Kati ya mahabusu hao waliofaidika na msamaha huo,wapo wateja wangu wawili. Ifahamike kuwa wafungwa hutofautiana na mahabusu. Mahabusu ni wale wanaoendelea na kesi zao. Wamenipunguzia kazi...

WAteja wako ulikuwa unawauzia nini?
 
Mahakama walishasema hawana hela za kuendesha kesi. Sasa hii ni njia moja wapo ya kupunguza kesi walizonazo kwa sababu hakuna hela>>>>>
 
Labda ni katika pilikapilika za kutaka kumfungulia na kumwacha huru Lulu anayetuhumiwa kwa mauaji ya Kanumba na wakati kuna tetesi za Ridhiwani Kikwete kumnunulia gari Lulu na kukutwa na messege muda mfupi baada ya kifo cha Kanumba inayosadikiwa kutoka kwa Ridhiwani. Hii Mkulu anatakiwa kutumia kila liwezekanalo kuinusuru familia yake kutoingia kwenye kashfa ya kesi hiyo ingawa haiwahusu moja kwa moja.
hili sasa jipya, pamoja na kuwa si la kisiasa lakini hiyo mesage toka kwa mtoto wa Jakaya ilikuwa inasemaje???ina mahusiano ya moja kwa moja na kifo cha kanumba??
 
Wametolewa tu lupango au kesi zao zimefutwa?

Kama nimemwelewa vizuri nadhani anakusudia kusema ameingilia mchakato wa kimahakama.

Hata hivyo hili la kuachia mahabusu (kwa msamaha wa rais!) kwangu bado haliingii akilini kwamba linaweza kufanyika. Maabusu wanasamehewa adhabu ipi ikiwa bado mahakama haijhasema kama wana makosa ama la na hata adhabu haijatolewa!?
 
huwa sioni faida ya hii misamaha, wanaopata misamaha wengi wao tunafahamu njia wanazozitumia kupata hiyo misamaha. Mtu amefungwa kwa kesi ya ubakaji, mauaji, unyang'anyi wa kutumua silaha lakini anapata msamaha. Masikini nchi yangu imeoza kila mahali
 
Mna uhakika na mnayosema??ulizeni mpate cha kusema sio rahisi kama mnavyofokiria ni mchakato mkali sana kuweza kuhonga hadi kupeta kupat huo msamaha kama kweli huusiki nao sio rahisi ulizeni acheni maneno maneno ya mitaani
 
Ikiwa jana Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 2973,mahabusu pia wameachiwa. Ni taarifa za uhakika. Kati ya mahabusu hao waliofaidika na msamaha huo,wapo wateja wangu wawili. Ifahamike kuwa wafungwa hutofautiana na mahabusu. Mahabusu ni wale wanaoendelea na kesi zao. Wamenipunguzia kazi...
Mkuu wameachiwa huku kesi ziko mahakamani? Kwa hiyo kesi zao zikitajwa huko mahakamani Magereza watasemaje, kwamba Rais aliwafutia mashitaka?

Hizi deal huwa zipo na watu huwa wanachomekwa na kuachiwa lakini huwa ni wafungwa wanaotumikia vifungo si mahabusu ambao hawajahukumiwa. Ikiwa mahabusu wameachiwa basi mahakama nazo zitakuwa zinahusika.
 
Mna uhakika na mnayosema??ulizeni mpate cha kusema sio rahisi kama mnavyofokiria ni mchakato mkali sana kuweza kuhonga hadi kupeta kupat huo msamaha kama kweli huusiki nao sio rahisi ulizeni acheni maneno maneno ya mitaani
Mkuu Skills4Ever anachosema Narubongo hapo juu ndicho hutokea. Wafungwa wengine hucheza na kupata vyeti vya madaktari na kuonekana kwamba wana Ukimwi ama ugonjwa wowote ule usiotibika na kuingizwa kwenye msamaha wakati wakitumikia vifungo hata vya mauaji na hutoka huku wakiwa buheri wa afya. Hizi deal zipo kibao ila la mahabusu ndio kwanza naliskia leo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom