JK aongeza muda wa kuwasilisha majina ya wajumbe Tume ya katiba...

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Awali mwisho wa wadau wote kuwasilisha majina ilikuwa Jana Machi 16 ambapo majina yalitakiwa kuwa yamefika kwa Katibu mkuu Kiongozi.

Hata hivyo JK amesogeza mbele muda huo na kudai kuwa huenda kuna wengine wamechelewa njiani. Sasa mwisho wa kuwasilisha majina ya watu wanaoombwa kuteuliwa katika Tume ya Katiba ni Machi 23 mwaka huu. Rais anatarajia kuitangaza tume hiyo ya katiba mwezi Aprili mwaka huu.

Source: IKULU

WAZO BINAFSI: Hivi JF hatuoni umuhimu wa kuteua wawakilishi wetu japo wawili tumpelekee Rais jmajina kweli??

Hapa suala si kuextend muda wa kuwasilisha hayo majina, hoja kuu ni kwamba Watanzania wanataka watu makini na wenye moyo wa uzalendo na Taifa letu ndio walisimamie hili suala la kukusanya maoni ya Wananchi ya namna wanavyotaka Katiba ya nchi yetu iweje ili kuleta mwanga wa kijani kwa ajili ya mustakabali na ustawi wa nchi yetu.Mimi naamini kabisa katiba bora ya nchi hutoka kwa wananchi wenyewe na wala si watawala au wanasiasa. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hivi kweli Rais kama taasisi ameshindwa kuitumia taasisi hiyo kupata watu muafaka hadi aletewe na wananchi??
 
Kukubali kuingia kwenye hiyo tume kuna presume kuwa mtu anaikubali. Mimi binafsi sikubali kwani imenyang'anya madaraka ya wananchi na kuyapeleka kwa RAis.

Kutaka watu waombe kuwa wajumbe wa Tume wakati rais bado Ndio mwenye mamlaka ya mwisho kwenye uteuzi ni kiini macho.

Madhumuni ya zoezi hili ni kutaka kuonesha watu kuwa wananchi walishiriki wakati ukweli ni kuwa ushiriki wa wananchi ni mdogo sana.

Nakupongeza kwa msimamo huo, watanzania wengi tungekuwa na mtazamamo wa namna hii tungekuwa mbali sana.
 
Sasa wananch wanapropose,halafu nani anamaamuzi ya mwisho?ukipata jibu hapo utaona bado mtanzania hajashirikishwa vya kutosha
 
Sasa wananch wanapropose,halafu nani anamaamuzi ya mwisho?ukipata jibu hapo utaona bado mtanzania hajashirikishwa vya kutosha

Akikataa Jina halazimiki kutoa sababu ya kulikataa jina hilo, na hawezi kuwa challenged kwa kufanya hivyo, ni upuuzi wa Hali ya juu.
 
Kukubali kuingia kwenye hiyo tume kuna presume kuwa mtu anaikubali. Mimi binafsi sikubali kwani imenyang'anya madaraka ya wananchi na kuyapeleka kwa RAis.

MM, unadhani njia gani ingekuwa bora zaidi kukusanya haya maoni mbali na kutumia tume??
 
Kukubali kuingia kwenye hiyo tume kuna presume kuwa mtu anaikubali. Mimi binafsi sikubali kwani imenyang'anya madaraka ya wananchi na kuyapeleka kwa RAis.

haisaidii, ni sawa na kusema unapinga katiba iliyopo ila bado unaitumia; utapinga tume ila itaundwa na katiba itatungwa na utainukuu na kuitumia kama mtanzania,hivyo ndivyo siasa ilivyo - mambo ni kwa maridhiano (compromise)
 
1. Mchambuzi
2. Mwanakijiji
3. Gaijin

HAKIKISHA WATU HAWA HAWAKUSOMA KATIKA VYUO VIFUATAVYO:
1-CCM-Kivukoni
2-CCM-Hombolo
3- CCM-Handeni

Kama tume ya katiba ikimuweka mtu mmoja aliyesoma katika vyuo hivyo, basi ni sawa na kutia mchicha katika glass ya mtindi.
 
Back
Top Bottom