JK akemea ufisadi CCM

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
RAIS Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, amesema mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na ufisadi hata kama ni mwanachama wa chama hicho, atashughulikiwa.

Alisema orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa imekuwa ikipokewa na wamekuwa wakichunguzwa, kwa kuzingatia utaratibu uliopo wa kuchunguza na kamwe Serikali haiwezi kukurupuka na kuwakamata na kuwaweka ndani.

Alisema hata mtu anayetajwa katika orodha hiyo ni lazima atendewe haki kwa kuwa zipo sheria na taratibu zinazomlinda.

"Mafisadi ni lazima washughulikiwe ili nchi ipate heshima naomba wale wote wanaowafahamu wasaidie kuwataja," alisema.

source: Nifaamishe
 
mmmmmmmhhhhh....
my comments are reserved!!! may be nikiskia wale walioshitakiwa wameshughulikiwa nitakuwa na la kusema.......
 
msikilizeni mh na story zake!!!


Habari zaidi!
JK: Fisadi ndani ya CCM atakiona
Martha Mtangoo, Dodoma
Daily News; Wednesday,January 07, 2009 @21:15

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na ufisadi hata kama ni mwanachama wa chama hicho, atashughulikiwa.

Akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema kazi ya kuwafuatilia na kuwachunguza wanaotajwa kuhusika katika sakata hilo inaendelea.

Alisema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika lazima lawama ziwapo, kwa sababu ni kazi ngumu na lawama katika uongozi hazikwepeki. Alisema orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa imekuwa ikipokewa na wamekuwa wakichunguzwa, kwa kuzingatia utaratibu uliopo wa kuchunguza na kamwe Serikali haiwezi kukurupuka na kuwakamata na kuwaweka ndani.

Alisema hata mtu anayetajwa katika orodha hiyo ni lazima atendewe haki kwa kuwa zipo sheria na taratibu zinazomlinda. “Jamani tuachieni tufanye kazi na sisi tutafanya hivyo bila kumkomoa mtu yeyote na kazi itafanywa ili wanaotuhumiwa waridhike; orodha za majina tunazopewa hazipuuzwi, zinafanyiwa kazi,” alisema Rais Kikwete.

Alisisitiza kuwa mafisadi ni lazima washughulikiwe ili nchi ipate heshima na kuwataka wanaowafahamu wasaidie kuwataja. Alisema uchunguzi unafanywa kwa muda mrefu na atakayebainika atafikishwa katika vyombo vya dola na iwapo watakaofikishwa katika vyombo hivyo hawataridhika, wako huru kwenda mahali popote kuelezea kutoridhishwa kwao.

“Kazi hii inafanywa na iwapo watu watatuhumiwa na kuona kuwa hawakutendewa haki, waende hata mahakamani … lakini waachiwe watu na vyombo vyao wafanye kazi yao na wasiingiliwe,” alisisitiza. Pia Rais Kikwete aliwataka wajumbe wa mkutano huo, kuchagua viongozi ambao watawafaa kwa kuwa wakifanya kosa, watalijutia kwa muda wa miaka mitano kwani majuto ni mjukuu.

Alisema ni vyema wajumbe hao wasiwachague watu kwa kuwa ni marafiki, ndugu au mashoga zao, kwa sababu tu kwamba watawafaa na kuwafadhili kwani hivyo si vigezo vya uongozi ndani ya jumuiya hiyo. “Usimchague mtu eti tu kwa sababu atakufaa, anayekufaa ni mumeo na ndugu yako, chagueni mtu ambaye atawatoa hapo mlipo na kuwapeleka katika neema,” alionya Mwenyekiti wa CCM.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama vya siasa vya Chadema, CUF, TLP na mabalozi wa nchi mbalimbali. Jana usiku, wajumbe walitarajiwa kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa Baraza Kuu, huku mchuano mkali ukitarajiwa katika nafasi ya mwenyekiti inayowapambanisha vigogo watatu.

Nao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, Sophia Simba, wabunge wa Viti Maalumu, Janeth Kahama na Joyce Masunga. Katika hatua nyingine, vitisho na matusi viliendelea kutawala kwa baadhi ya makatibu wa mikoa na wilaya wa umoja huo, kutishiwa kukataliwa na wenyeviti wao kwa madai kuwa hawakushiriki katika kampeni.

Licha ya makatibu hao kutishiwa kukataliwa na wenyeviti hao, pia baadhi ya wapambe wa wagombea wa nafasi za juu za UWT wamekuwa wakiwatishia makatibu hao, kuwa mgombea wao akishinda makatibu hao ‘wataipata’.

Mwenyekiti wa UWT anayemaliza muda wake Anna Abdallah, alimweleza Rais Kikwete jana kuwa mambo hayo yameanza kujitokeza baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi katika mikoa na wilaya.

“Jambo lingine ambalo limeanza kujitokeza baada ya kukamilika kwa uchaguzi huko mikoani na wilayani ni salamu zilizoanza kufika makao makuu, kuwa baadhi ya wenyeviti wa mikoa na wilaya wamesema hawawataki makatibu wao, kisa eti hawakushiriki katika kampeni zao za uchaguzi.

“Na baadhi ya wapambe wamesikika wakisema mgombea wao akishinda, basi kuna makatibu wataipata,” Abdallah alimweleza Mwenyekiti huyo wa CCM. Mwanasiasa huyo mkongwe alisema mambo hayo yanasababisha makundi ndani ya CCM, kwa kuwa baadhi ya wapambe wa wagombea wa nafasi za juu walikuwa wakizunguka mikoani na kutumia fedha nyingi huku wakipata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa mikoa na wilaya wa UWT.

Alisema matumizi makubwa ya fedha ambayo yamekuwa yakifanywa na wapambe hao, yanawakatisha tamaa wanawake wengine ambao wana nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na hivyo kukifanya chama kugawanyika. “Sasa mimi najiuliza, gharama hizi kweli kwa ajili ya uenyekiti na uongozi wa UWT au kuna la zaidi?,” alihoji na kumwomba Rais Kikwete kuwalinda wanawake walio tayari kugombea nafasi za uongozi na kuiomba CCM ikemee tabia hiyo, kwani inazaa makundi ndani yake.
 
Back
Top Bottom