JK aikwepa Mei Mosi... Rais Kikwete hatahudhuria Mei mosi

Watanzania, tusimlaumu sana JK kwani taabu hizi zote na mzigo huu kaachiwa na Mkapa, kuwa miwaziri mizi, ujue kama asingeiteua kweli angejiweka pabaya, sasa tunamtaka aende pale Iringa akaseme nini jamani? Kikwete ana nia njema tuu ila hawa maswahiba zake ndiyo wanamuangusha

Isayamwita: naomba utuambie ni mzigo gani alioachiwa Jk na Mkapa ambao ameshindwa kuutua kwa miaka hii 2 na nusu?
Mkapa alimwachia siyo tu urais wa nchi bali hata uenyekiti wa chama mwaka 2006, sasa kazi ilikuwa kwake JK kuufanyia kazi. Pia alikuwa ana uwezo wa kuchagua mawaziri wapya kabisa kwani aliwaleta akina Membe au siyo? Na hao wageni tukajua ni washikaji na wako pale kwa ajili ya ulaji. Hebu cheki RA alivyoutwaa hazina ya chama! Sasa hapo Mkapa amehusika vipi?

Sisi wakristo tunasema kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe, sasa JK naye akubali kimeo hiki ni cha kwake na au bebe, face it like a man! Tumechoka na vijisababu vyake! (channelling Chenge with his vijisenti)
 
Back
Top Bottom