Jitolee ili uajiriwe

Ahmet

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
1,537
3,404
Habari za wakati huu wapendwa, natumai mnaendelea vizuri.

Katika miaka ya hivi Karibuni kumekuwa na usemi kuwa jitolee ndipo uajiriwe hasa katika sekta ya elimu. Kwa ujumla suala la kujitolea ni zuri lakini ebu tujaribu kuliangalia kwa jicho la tatu, je kinapotumika kigezo cha kujitolea ili kuajiriwa kunakuwa hakuna athari zozote?

Kwa upande wangu na kwa jicho la mbali nimeona kuna athari kadhaa zinazoweza kujitokeza pindi mamlaka zitapotumia kigezo cha kujitolea ili kuajiri watumishi wa umma.

Miongoni mwa athari hizo ni pamoja na;-

Mosi, kigezo cha kujitolea kinaathiri (kinadiscourage) ari ya vijana kufanya ujasiriamali mwengine na uwekezaji mdogomdogo mbali na fani walizosomea. Ebu fikiria mwanafunzi amemaliza chuo badala ya kufanya uwekezaji analazimika kutafuta taasisi ya umma kujitolea ili tu zitakapotangazwa ajira awe katika nafasi nzuri kuajiriwa. Ule wimbo kuwa vijana mjiajiri unazimwa na maamuzi haya ya serikali yetu ambayo bila shaka ina nia nzuri tu.

Ni ukweli kuwa wengi katika wahitimu wanapenda kupata ajira za serikali, kwaiyo mtu atakubali apate tabu kwa kufanya kazi bila kulipwa hata kwa miaka minne au mitano ili tu apate hiyo ajira inayoitwa ya 'uhakika' ya serikali. Kuna kaka yangu kamaliza chuo 2016, Kwa Sasa ni bodaboda ila aliposikia kuwa wanaopewa kipaumbele katika ajira hizi za walimu ni wanaojitolea alitamani kuacha iyo kazi yake lakini hakua na namna. Just imagine mhitimu wa chuo kikuu anauza karanga zake za shilingi 100 na 200 awe hana kigezo cha kuajiriwa kwakua tu hajitolei. Kuna watu wanafikiria hadi kuacha kufundisha private schools ili wakajitolee.

Pili, kigezo cha kujitolea kinaongeza mianya ya rushwa na upendeleo ili kupata kazi. Kuna uwezekano mkubwa wa wakuu wa shule kuandika majina au kusaini barua za wanaojitolea kwa upendeleo. Sijalishuhudia hilo lakini akili yangu inaniambia ili haliwezi kuepukika. Ebu fikiria mkuu wa shule hawezi kuwa na mtoto, au ndugu wengine au mtoto wa rafiki anaeomba hizi ajira? Je hana uwezo wa kuwaandika hao watu wake wa karibu kwa upendeleo? Ebu tulitafakari hili pia.

Tatu, si kila alieomba kujitolea alipata fursa hiyo. Ni ukweli kuwa Kuna baadhi ya wahitimu walijaribu kuomba kujitolea lakini walikosa nafasi, sasa mtu Kama huyu ukimuekea kigezo cha kujitolea ili apate kazi huwa anaumia kwelikweli.

Nne, ufanisi katika kazi utapungua pia. Kitakapotumika kigezo hiki kuajiri watumishi, wengi watakimbilia huko ili tu nao wawe katika list ya wanaojitolea. Hapa ufanisi unaweza kuwa mdogo kwasababu mtu analenga benefit fulani ingawa sikatai wapo Leo hii wanaojitolea na ufanisi wake ni mkubwa, hawa walijitolea kwa kupenda na si kutafuta ajira.

Tano, Ni kweli serikali itaajiri watu wote wanajitolea? hili ni swali jengine ambalo tunapaswa tujiulize. Wahitimu mtaani ni wengi sana, mnaweza ona katika hizi ajira za walimu na watu wa afya jinsi nafasi zilivyokuwa chache ukilinganisha na waombaji. Kama kujitolea ni kigezo je watu wote hao au wengi wao wakiwa wanajitolea serikali itawahakikishia ajira?

IPI NI NJIA NZURI KUAJIRI BILA MALALAMIKO?
Moja katika njia nzuri kuajiri ni kuanza na wale waliomaliza zamani na Kisha wanaofuata. Ebu tuwaonee huruma hawa waliomaliza muda mrefu na bado wapo mtaani na maisha yao hayaeleweki. Wengi hadi leo hawana kazi za msingi zinazowaingizia kipato cha maana. Wengi tayari wanafamilia ingawa maisha ni magumu, Mtu huyu leo ukimwambia akajitolee utamuumiza moyo sana. Unakuta kijana yuko mtaani miaka zaidi ya tano, Hana kazi ya uhakika. Ingawa mimi nimemaliza karibuni lakini nilitamani kuona Kaka zetu hawa wanapata kazi kabla yetu bila kuangalia Kama wanajitolea ama laa.

Pia kipaumbele kiwe kwenye courses zenye mahitaji makubwa, mfano kwa walimu basi wale wa masomo ya sayansi wapewe kipaumbele zaidi kwani wao ndio wanahitajika zaidi na hii ni 'rule' tangu mtu yupo shule ya msingi awe anafahamu kuwa ukisoma masomo ya sayansi basi unakuwa marketable, ili la kijitolea ni jipya sana.

NI LIPI SULUHISHO LA KUDUMU?
Kama wadau mbalimbali wanavyotoa maoni yao, vijana wapewe ujuzi wa kujiajiri na sio tu kutegemea ajira toka serikalini. Kwakua uhalisia ni kuwa wahitimu ni wengi kushinda mahitaji basi serikali lazima iwe na jitihada za makusudi kuwapa uwezo vijana kujitegemea, kutumia rasilimali kutoka katika mazingira na kuzibadirisha kuwa fursa.

Pia sekta binafsi ziimalishwe, shule binasfi, hospitali, na taasisi nyengine za watu binasfi ziimalishwe ili kuleta usawa Kati ya watu wanaofanya kazi katika taasisi hizo, waliojiajiri na walioajiriwa na serikali, wote wawe na hadhi moja.

Shukrani
 
Hiyo namba tatu inanihusu kabisa, niliwahi kupeleka barua ya kujitolea katika shirika flani la serikali lakini sikupata nafasi, lakini kuna jamaa nimesoma naye alipata nafasi ya kujitolea katika shirika hilo hilo kwa Connection
 
Wapo wengi, si kila mhitimu anaweza pata nafasi ya kujitolea
 
Wamesema mpaka sasa wame apply 89000?

Na ajira ni 6000?!!!
 
Habari za wakati huu wapendwa, natumai mnaendelea vizuri.

Katika miaka ya hivi Karibuni kumekuwa na usemi kuwa jitolee ndipo uajiriwe hasa katika sekta ya elimu. Kwa ujumla suala la kujitolea ni zuri lakini ebu tujaribu kuliangalia kwa jicho la tatu, je kinapotumika kigezo cha kujitolea ili kuajiriwa kunakuwa hakuna athari zozote?
Kwa upande wangu na kwa jicho la mbali nimeona kuna athari kadhaa zinazoweza kujitokeza pindi mamlaka zitapotumia kigezo cha kujitolea ili kuajiri watumishi wa umma.
Miongoni mwa athari hizo ni pamoja na;-

Mosi, kigezo cha kujitolea kinaathiri (kinadiscourage) ari ya vijana kufanya ujasiriamali mwengine na uwekezaji mdogomdogo mbali na fani walizosomea. Ebu fikiria mwanafunzi amemaliza chuo badala ya kufanya uwekezaji analazimika kutafuta taasisi ya umma kujitolea ili tu zitakapotangazwa ajira awe katika nafasi nzuri kuajiriwa. Ule wimbo kuwa vijana mjiajiri unazimwa na maamuzi haya ya serikali yetu ambayo bila shaka ina nia nzuri tu. Ni ukweli kuwa wengi katika wahitimu wanapenda kupata ajira za serikali, kwaiyo mtu atakubali apate tabu kwa kufanya kazi bila kulipwa hata kwa miaka minne au mitano ili tu apate hiyo ajira inayoitwa ya 'uhakika' ya serikali. Kuna kaka yangu kamaliza chuo 2016, Kwa Sasa ni bodaboda ila aliposikia kuwa wanaopewa kipaumbele katika ajira hizi za walimu ni wanaojitolea alitamani kuacha iyo kazi yake lakini hakua na namna. Just imagine mhitimu wa chuo kikuu anauza karanga zake za shilingi 100 na 200 awe hana kigezo cha kuajiriwa kwakua tu hajitolei. Kuna watu wanafikiria hadi kuacha kufundisha private schools ili wakajitolee.

Pili, kigezo cha kujitolea kinaongeza mianya ya rushwa na upendeleo ili kupata kazi. Kuna uwezekano mkubwa wa wakuu wa shule kuandika majina au kusaini barua za wanaojitolea kwa upendeleo. Sijalishuhudia hilo lakini akili yangu inaniambia ili haliwezi kuepukika. Ebu fikiria mkuu wa shule hawezi kuwa na mtoto, au ndugu wengine au mtoto wa rafiki anaeomba hizi ajira? Je hana uwezo wa kuwaandika hao watu wake wa karibu kwa upendeleo? Ebu tulitafakari hili pia.

Tatu, si kila alieomba kujitolea alipata fursa hiyo. Ni ukweli kuwa Kuna baadhi ya wahitimu walijaribu kuomba kujitolea lakini walikosa nafasi, sasa mtu Kama huyu ukimuekea kigezo cha kujitolea ili apate kazi huwa anaumia kwelikweli.

Nne, ufanisi katika kazi utapungua pia. Kitakapotumika kigezo hiki kuajiri watumishi, wengi watakimbilia huko ili tu nao wawe katika list ya wanaojitolea. Hapa ufanisi unaweza kuwa mdogo kwasababu mtu analenga benefit fulani ingawa sikatai wapo Leo hii wanaojitolea na ufanisi wake ni mkubwa, hawa walijitolea kwa kupenda na si kutafuta ajira.

Tano, Ni kweli serikali itaajiri watu wote wanajitolea? hili ni swali jengine ambalo tunapaswa tujiulize. Wahitimu mtaani ni wengi sana, mnaweza ona katika hizi ajira za walimu na watu wa afya jinsi nafasi zilivyokuwa chache ukilinganisha na waombaji. Kama kujitolea ni kigezo je watu wote hao au wengi wao wakiwa wanajitolea serikali itawahakikishia ajira?

IPI NI NJIA NZURI KUAJIRI BILA MALALAMIKO?
Moja katika njia nzuri kuajiri ni kuanza na wale waliomaliza zamani na Kisha wanaofuata. Ebu tuwaonee huruma hawa waliomaliza muda mrefu na bado wapo mtaani na maisha yao hayaeleweki. Wengi hadi leo hawana kazi za msingi zinazowaingizia kipato cha maana. Wengi tayari wanafamilia ingawa maisha ni magumu, Mtu huyu leo ukimwambia akajitolee utamuumiza moyo sana. Unakuta kijana yuko mtaani miaka zaidi ya tano, Hana kazi ya uhakika. Ingawa mimi nimemaliza karibuni lakini nilitamani kuona Kaka zetu hawa wanapata kazi kabla yetu bila kuangalia Kama wanajitolea ama laa.

Pia kipaumbele kiwe kwenye courses zenye mahitaji makubwa, mfano kwa walimu basi wale wa masomo ya sayansi wapewe kipaumbele zaidi kwani wao ndio wanahitajika zaidi na hii ni 'rule' tangu Mtu yupo shule ya msingi kuwa ukisoma masomo ya sayansi basi unakuwa marketable, ili la kijitolea ni jipya sana.

NI LIPI SULUHISHO LA KUDUMU?
Kama wadau mbalimbali wanavyotoa maoni yao, vijana wapewe ujuzi wa kujiajiri na sio tu kutegemea ajira toka serikalini. Kwakua uhalisia ni kuwa wahitimu ni wengi kushinda mahitaji basi serikali lazima iwe na jitihada za makusudi kuwapa uwezo vijana kujitegemea, kutumia rasilimali kutoka katika mazingira na kuzibadirisha kuwa fursa.

Pia sekta binafsi ziimalishwe, shule binasfi, hospitali, na taasisi nyengine za watu binasfi ziimalishwe ili kuleta usawa Kati ya watu wanaofanya kazi katika taasisi hizo, waliojiajiri na walioajiriwa na serikali, wote wawe na hadhi moja.

Shukrani
Wanaoweza kujitolea ni watoto wa wanaojiweza sisi hohehae kufanya kazi bila kulipwa ni sawa na kujiua ndio maana tunajichanganya na mishe yeyote inayoibuka, yanayoendelea sasa hatushangai maana hata maandiko yanasema mwenye nacho atazidi kuongezewa
 
kabisa kabsa sisi wengine hatuwezi tukaacha kufanya shughuli zetu ndogondogo eti tukajitolee
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Mimi kinachonipa mawazo na mshangao ni kwamba kipindi kile cha jk alianzisha program kibao ili kupata walimu nadhani kipindi kile uhaba ulikuepo kwa hali ya juu......mwaka 2014 akaanzisha special diploma, ambayo walipelekwa udom na wakawa wanapewa bumu. punde tu alipoingia bwana mkubwa akawafukuza (nadhani wote mnakumbuka ile scenario), japo walirudi nyumbani lakini walitafutiwa namna ya kurudi vyuoni kwa condition ya kufanya paper za advance kwa masomo mawili tu.
Tatizo likaanzia hapo Magufuli hakuajiri na kila mwaka vyuo vikawa vinatema kuanzia certificate, special diploma, diploma yenyewe pamoja na degree yote hayo yamepelekea maombi kua zaidi ya 89,000 japo wengi pia hawajaomba.
Mimi naona kwa upande wangu zile program zilizoanzishwa ili kuwapata walimu wasitishe ili kupunguza idadi ya walimu wengi walioko mitahani, inabidi wabaki na certificate, diploma na degree basi.,..labda pia idadi ya watu watakaoomba kupitia ualimu itapungua.
watu still ni wengi sana, me nadhani solution ni kuzipa nguvu private sectors pia ili nazo zitoe ajira za uhakika
 
Back
Top Bottom