Jinsia ipi ya ni mtoto b

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,712
Imekuwa kawaida mwanamke akijifungua,kama ni wa kiume utasikia wengine wakisema afadhali,wengine jambazi,akiwa wa kike utasikia wengi wakiponda eti katuletea malaya,wengine bora ametuletea mama,je jinsia inahusikaje na ubora wa mtoto?
 
Naanza mimi mwenyewe kwa kusema kuwa,kawaida kuku hawezi kutaga yai viza ila uatamiaji wake mbovu ndo unaweza kusababisha uviza wa yai!
 
Ni upuuzi, nathubutu kusema hivyo.
Kama baba au mama anasema kazaa malaya, basi ye ndo malaya zaid manake ye nd mama/baba yake.
Watu hawajui, wanadhani vitu vingine ni kua wanstahili kumbe ni barakatu,
utajaliwa vipi mtoto halaf unamwita malaya au jambazi.
Tunawalaani watotot wetu wenyewe halaf badae wakija kua malaya/majambazi
tunaaza kulalamika.
 
sio vizuri kunena maneno hayo kwa mtoto uliyekuwa unamsubiri kwa kipindi cha miezi 9
kuna malezi ambayo yanapelekea mtoto wako kuwa jambazi au malaya
 
Bibi yangu aliiniambia
"sisi tunazaa lakini hatujui tunazaa nini"
haya wale wenye akili za kitoto piteni tu
na wanaulewa huo msemo msiudharau..

Mtoto ni zawadi , hatuna uwezo
wa kutabiri watakavyo kuwa..
cha muhimu ni sisi kuwapa malezi
bora na kuwapa miongozo mema
lakini papo hapo tukumbuke wanakua
na akili zao wenyewe kuna wengine wataonyesha
mapema watakavyo kuwa lakini kuna wengine LA..
na si vema kumtabiria mabayaa...
 
Sishangai maana wapo ambao hata majina ya watoto wao hua yanaasharia kwamba wanaona kama mizigo tu!!Kumsema mtoto hivyo sio vizuri wala sio sawa....mtu mwenye perception ya aina hiyo kuhusiana na watoto sidhani hata kama anatakiwa kuwa na watoto!
 
"Ee Mungu kwa huruma zako uwarehemu wanaowabatiza watoto wachanga wasiojua kitu majina ya ajabu ajabu, naomba uwabadilishe vinywa vyao viweze kunenena ukuu wako badala ya kuwaza maneno ya kijinga na kipumbavu, naamini we u mwema na unatenda kazi zako bila kifani, fanya miujiza yako baba ktk hili" amennnn!
 
Mie nawapenda sana watoto wa kike maana wanahuruma kuliko, kila siku mtoto wa kike hukumbuka kwao hata kama kaolewa lkn Mwanaume bwana akioa hapo sasa kila kitu hufanya zaidi au huanza kutengeneza UKWENI kwanza then kama zipo kwao kama zikiisha anaishia hapo hapo...Fanyeni Uchunguzi hapo, ingawa mie ni mwanaume ila nitapenda sana kuzaa wa kike na nikimsikia mtu anasema chochote tu juu ya watoto wangu...nasababisha msiba...
 
Bibi yangu aliiniambia
"sisi tunazaa lakini hatujui tunazaa nini"
haya wale wenye akili za kitoto piteni tu
na wanaulewa huo msemo msiudharau..

Mtoto ni zawadi , hatuna uwezo
wa kutabiri watakavyo kuwa..
cha muhimu ni sisi kuwapa malezi
bora na kuwapa miongozo mema
lakini papo hapo tukumbuke wanakua
na akili zao wenyewe kuna wengine wataonyesha
mapema watakavyo kuwa lakini kuna wengine LA..
na si vema kumtabiria mabayaa...


Na anayetabiria ashindwe kwa jina lake Yesu..na mimi nikimsikia akisemea mbovu wanangu walahi hata nisikie tu kupitia kwa jirani...Maisha yake matatani....
 
Mh haya maneno mi siyakubali,mtoto ni mtoto, ndio maana tuliambiwa waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom