Jinsi ya kutengeneza kinywaji cha lemonade mocktail (mojito) nyumbani

Aaliyyah

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
15,805
37,775
I hope mko vyema

Ni kinywaji kinachopendwa na watu wengi na ni kitamu sana
Naomba kushare nanyi sikumoja moja muwe mnaenjoy hata mkiwa nyumbani

LEMONADE MOCKTAIL mahitaji:
  • Glass 1
  • Msukumio au kifaa Cha kupondea mchanganyiko wako
  • Ndimu/limao 1
  • Majani ya mnanaa(mint)
  • Sukari kijiko kimoja sio lazima unaweza usiweke kama hupendi sukari au ukaweka kidogo
  • Soda nyeupe(sprite)
  • Vipande vya barafu(icecubes)
Namna ya kutengeneza

1. Kata ndimu Yako slice 4 weka Tatu kwenye glass moja acha kwaajili ya kupambia
weka na majani 5 ya mint pamoja na sukari kiasi upendacho

2. Chukua kifaa Cha kupondea ulichooandaa Kama ni msukumio au chochote anza kuponda mchanganyiko wako taratibu Kwa sekunde 30

3. Weka vipande vya barafu (icecubes) kwenye glass yenye mchanganyiko wako. Weka slice ya ndimu ilobaki kama pambo

4. Miminia soda ya sprite kwenye glass Yako koroga tayari Kwa kunywa

Inapunguza hangover
Hufanya ujisikie vizuri
Mint na limao husaidia digestion

NB kama utatumia limao bas weka kiasi kama ni kubwa sio lazima kutumia lote
Nawatakia weekend njema

😍Nawapenda

IMG_20240218_162843-COLLAGE.jpg
Screenshot_2024_0218_164758.jpg
Screenshot_2024_0218_165610.png
 
Back
Top Bottom