lushalila
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 283
- 107
Mwenye idea naomba anifahamishe jinsi ya kupata line za uwakala wa simu za mikononi kama vile Tigo pesa, M-Pesa nk.
Nisaidieni
------------------
Nisaidieni
------------------
KISHERIA: inatakiwa uwe natin namba naleseni yabiashara, ukishakuwa navyo hivyo utapiga copy tin namba yako naleseni yabiashara nakitambulisho kati yahivi kitambulisho chakupigia kura/ kitambulisho chautaifa/ au leseni yaudereva, utachukua nyaraka zako utazipeleka kwamtandao husika nautawaachia mawasiliano yako hapo kazi yako inakuwa imeisha nabaada yamda watakutaarifu kama tayar nautaenda kuchukua till zako.
Kwa kifupi hatua ni hizi:
1. Uwe na TIN ya biashara
2. Uwe na Leseni ya biashara
3. Uwe na kitambulisho kinachotambulika kitaifa mfano passport, driving licence, cha uraia, cha kupiga kura, n.k.
Halafu toa copy nyaraka zote na ku verify then submit kwa dirisha la mtandao linalohusika na miamala ama kwa kampuni ama mtu binafsi anayefanya hiyo kazi kama wakala then ata submit kwa mtandao husika.
Ama unaweza kununua kwa wauzaji maana huwa pia zinauzwa na watu walioshindwa kufanyia biashara ama walioamua kuhama biashara. Bei hutegemeana na mtu hakuna bei rasmi. Currently wanauza kuanzia 250,000 lkn hakuna kiwango rasmi unawezakuta hata akakupa bure hahahahaha
Usisahau na kuwa na hela ya kuanzia biashara yaani mtaji.