Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Sikushauri pia..maana wewe unaonekana sio risk taker
What kind of a risk is that...yaani hate nyumbani watashangaa nimevimba shavu natafuna mirungi eti nipungue..KHAAAAA

Hivyo vitu vinafanywa na Watu wasio jielewa
 
Tissue haiwi repaired na protein tupu. Ingekua hivyo steroids na HGH zingekua na protini tupu.

Narudia tena. Kabohaidreti (Ubwabwa, ugali, viazi n.k) ndiyo nguvu yako. Protini ndiyo inasababisha kuongezeka (kunenepa kwa mwili)

Notisi kwamba nimesema kua kula chakula kingi hakuna madhara kama unafanya mazoezi ya kuendana na chakula unachokula. Hao mabaunsa wenye vitambi hata siyo kwaajili ya kula mostly ni kwaajili ya supplements na yes am saying it hata supplements kama haufanyi mazoezi ipasavyo mwisho ni kutokwa na kitambi.

Niliandika uzi juu ya supplements katika bodybuilding. Nimeutafuta siuoni ila najua juu ya nutrition na bodybuilding so ninachoongea ni personal experience na observation kwa wengine.
Steroid ni kama hormone..zinachochea kitu kinachoitwa Anabolism(build up),Protein ndo inayotumika kwenye build up i.e muscles..

Point zako hazipo sawa mkuu,Carbs ndo kisababishi kikubwa cha unene
 
Nakufatilia mkuu, shule yako imetulia sana na kama jamaa haelewi ana lake jambo. kiufupi wanga unaohitajika na mwili unapatikana ktk makundi mengine ya chakula. Na mwili hauhitaji wanga kwa kula wanga kama tunavyofanya Ila kutoka kwa makundi mengine. Mimi mwenyewe sijala vyakula vya wanga kwa miaka 3 na nipo fresh na afya tele.
True..
 
Tango pori - Nimesoma mahali, mwili hauwezi kutengeneza fats wenyewe na ndio maana tunahitaji kuweka mafuta kwenye chakula.
 
Ngoja nikupe science facts, achana na upuuzi wa sijui vinywaji gani wanavyouza watu kukudanganya vinakata kitambi. Miaka 2 iliyopita nilikua na kilo 115, mwili wangu ulivyo mafuta mengi yalikua kwenye tumbo, watu tunatofautiana wapo ambao mafuta mengi wanatunza kwenye mapaja, wengine mgongoni e.t.c. Leo hii nina kilo 75, misuli tupu, fat imeshuka hadi 12% yaani six packs zinaonekana bila hata kuflex. Nimefikaje hapa?

Inabidi ubadilishe lifestyle lako asilimia 100, sitanii hiki ndicho kitu kigumu sana ambacho hata marafiki zangu mabonge wameshindwa kufanya.
1. Fanya mazoezi mno, mwanzoni uanze na full body workout siku tatu kila wiki, baada ya miezi miwili badilisha uanze kufanya siku tano kwa wiki, specilized kwa kila body part.
2. Kula, hili ni jambo muhimu sana kuliko yote na ndilo gumu ambalo 99% hua wanashindwa, inabidi uanze kuhesabu calories unazokula kila siku, vyakula ninavyorecommend ni vyenye protein sana, wanga kidogo, sukari kata 100%, yaani sitaki kusikia unagusa sukari, chai usiweke sukari, kupika chochote usiweke sukari, maandazi sijui nini vinavyowekewa sukari vyote kata 100%, ni ngumu ila baada ya miezi miwili ulimi unakua usharegister palete mpya ya taste unajikuta umezoea, mimi nakunywa chai bila sukari vizuri tu.

Kisayansi, kupunguza mwili inabidi calories zinazoingia mwilini ziwe ndogo kuliko ya zinazotumika, mwili kufanya kazi zake za kawaida kila siku unatumia calories flani, sasa ukila sana kuzidi calories ambazo mwili unahitaji unajikuta calories nyingine zilizobaki zinabadilika kua mafuta mwili unatafuta sehemu ya kuyatunza yanakaa hapo ukitegemea huko mbeleni labda utakuja kuyatuumia sehemu. Sasa ukiingiza calories ndogo mwilini kuliko mwili unazotumia mwili unakosa pa kupata calories nyingine unaanza kula mafuta uliyonayo na wakati mwingine misuli ili uendelee kufanya kazi.

Navyokwambia kula kidogo na fanya mazoezi kwa wakati moja ni kwa sababu kula kidogo kunafanya upate calories chini so mwili utatumia mafuta uliyonayo ili kufanya kazi zake za kawaida, na fanya mazoezi kwa sababu unavyojenga misuli mwili unakua unahitaji calories nyingi zaidi ili kujenga hiyo misuli, kwa hiyo unajikuta mwili wako unabadilika haraka sana kwa sababu unahitaji calories nyingi zaidi ila unaupatia calories ndogo zaidi ya ulivyozoea.

Mambo mengine yooote utaambiwa sijui tumia dawa gani sijui nini ni uongo mtupu, ni watu wanataka kuuza products zao wapige hela basi, hii ndiyo sayansi imefanya kazi miaka elfu kadhaa hadi leo kila mtu unayemuona ana mwili mzuri hii ndiyo principle anayofata basi hakuna kingine.

Na usiogope kufanya mazoezi kama ya kunyanyua vyuma, kama ni mwanamke ukinyanyua vyuma haimaanishi utakua na mwili wa kiume, huna hormone za kiume za kufanya mwili wako uwe mkubwa hivyo, utaishia kua sexy tu basi, wanawake unaoona wana misuli imejaa wengi wanatumia hormone za kiume kuboost. Mazoezi mwanzoni yanauma mno, mimi siku ya kwanza nimefanya mazoezi ya miguu sikuweza kutembea wiki nzima.

Acha kula ugali, ile ni pure carbohydrate, inabadilika kirahisi sana kua fat, kama huwezi basi kula kidogo sana, zidisha mboga hasa nyama, pendelea kuku kuliko nyama nyingine, hasa chicken breast sababu inaprotein nyingi mno, maharage pia, ukijisikia kunywa chai achana na ya maziwa, tumia ya rangi, weka majani ya chai usiweke sukari au kuongeza kitu chochote kunywa hivyo hivyo, ka vipi kata breakfast kabisa ule lunch na dinner tu, na haimaanishi ule kama unakula msosi wa kijiji kizima, ule kidogo tu, calories kama 1500 zinatosha kabisa kwa siku. Fanya hivyo alafu nunua mizani jipime kila wiki utashangaa kila mwezi unapunguza sio chini ya 4kg. Unaweza uliza kama unataka tips za jinsi ya kufanya mazoezi.

TLDR Eat less, Workout more.

Tafadhali kua mvumilivu mno, huwezi ona results ndani ya wiki mbili, results utaanza kuziona kama umekomaa angalau kuanzia miezi miwili mitatu. Na kua sexy kabisa itachukua miaka miwili au zaidi kulingana na wewe mwenyewe umeanzia wapi. Start now, usipoanza leo hutoanza.
Tatizo la wengi ni kwenye persistence ya mazoezi na diet. Mtu anaanza vizuri kabisa program ya mazoezi na diet ila akiona amefanya mwezi mmoja na hajaona mabadiriko basi anaacha na kurudia zama zake. Ndio maana kila siku aehemu za mazoezi utaona sura mpya tu kila siku na ni vibonge kwelikweli, hii ni ishara kuwa watu wanakata tamaa ndani ya muda mchache sana.
 
Kuna vitu vinaitwa Macro na Micro..Macro vinahitajika kwa kiasi kikubwa na Micro ni kwa kiasi kidogo..Fats hazihitajiki sana mwilini na pia mwili unaweza kujitengenezea wenyewe sometimes as long as unapata carbs na protein..na huwezi kula chakula kisichokuwa na fats hata kidogo..
Nafikiri stored fat ndiyo lipids? Which itatumiwa pale mtu ndiyo hauna fat kabisa
 
Steroid ni kama hormone..zinachochea kitu kinachoitwa Anabolism(build up),Protein ndo inayotumika kwenye build up i.e muscles..

Point zako hazipo sawa mkuu,Carbs ndo kisababishi kikubwa cha unene
Katika bodybuilding kuna anabolic steroids (dianabol n.k) kisha kuna HGH (Human Growth Hormone)

Steroids zinachochea repairment ya seli nyekundu za damu kuongeza circulation ya damu which in turn inamfanya mtu akiwa anafanya mazoezi asiwe fatiqued.

Mimi hamna sehemu nimesema kuna chochote kinasababisha unene so unatakiwa kuwaquote wanaosema ubwabwa na ugali unasababisha unene ili wakuelewe.
 
Mimi Ni Ke..Nina tumbo kuubwa, nimejaribu njia Tofauti Tofauti ila sijapata matokeo.

Nlikua nafanya mazoezi na nikipata matokeo chanya ..ila nikashtuka goti..nikifanya mazoezi linauma goti.

Je nitumie.njia gani.mbadala wa mazoezi ili nifikie lengo.
.nakosa confidence na hili tumbo langu.

N.B Picha Siwezi tuma kwa wale wapenda picha.
Kata wanga (pata portion kidogo sana ya wanga...hahasa wekeza ktk matunda na mbogamboga), kata sukari na mafuta then tembea kila siku at least kwa nusu saa. Kunywa maji mengi ikiwezekana changanya na Apple Cider Vinegar.
 
Nakufatilia mkuu, shule yako imetulia sana na kama jamaa haelewi ana lake jambo. kiufupi wanga unaohitajika na mwili unapatikana ktk makundi mengine ya chakula. Na mwili hauhitaji wanga kwa kula wanga kama tunavyofanya Ila kutoka kwa makundi mengine. Mimi mwenyewe sijala vyakula vya wanga kwa miaka 3 na nipo fresh na afya tele.
Boss umesema mwaka jana ulikua na kilo 115 umezipunguza mpaka 65 means umekua around healthy life haizidi mwaka. Mimi nimekua humo since 2013 training na watu mbalimbali juu ya vyakula, supplements na nikidebunk beliefs mbalimbali. Hata mimi nilikua najua diet ni miongoni mwa msingi mkuu.

Madaktari hua wana kitu wanaita BMI utachekiwa urefu wako na kuambiwa kwa kilo ulizonazo ni sahihi na urefu wako ama hapana. 2015 nilikua na urefu wa 163CM na uzito wa kilo 87 so hiyo BMI inaniweka kwenye kundi la unhealthy, ila hizo kilo zote zilikua ni muscles siyo fat so BMI was wrong ni sawa leo Kai Greene aonekane unhealthy kisa urefu wake na uzito BMI inaukataa.

Hata ule chakula cha wanga kiasi gani what matters ni utafanyaje mazoezi ili kudeal na unachoingiza mwilini.

Mimi siwezi kua na jambo lolote juu ya kusema ninachojua. Kwamba nafanya hivi ili muendelee kubaki wanene?
 
Mimi Ni Ke..Nina tumbo kuubwa, nimejaribu njia Tofauti Tofauti ila sijapata matokeo.

Nlikua nafanya mazoezi na nikipata matokeo chanya ..ila nikashtuka goti..nikifanya mazoezi linauma goti.

Je nitumie.njia gani.mbadala wa mazoezi ili nifikie lengo.
.nakosa confidence na hili tumbo langu.

N.B Picha Siwezi tuma kwa wale wapenda picha.
Mbona Avatar yako inaonyesha wewe ni wa kawaida,tena kipotabo?
 
cardio exercises plus punguza kula more carbs kula zaid protein, fats esp frm mimea, matunda na vegetables usisahau plenty if water, withn a month tu utaona changesn..hamna uchawi wala dawa sijui utameza tumbo liishe..zingatia ushauri huu

Pia aache processed sugar
 
Angalia vizuri, nilikuwa na 85 na kwa sasa nina 65 na urefu ni 169cm

Back
Top Bottom