Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Mimi Ni Ke..Nina tumbo kuubwa, nimejaribu njia Tofauti Tofauti ila sijapata matokeo.

Nlikua nafanya mazoezi na nikipata matokeo chanya ..ila nikashtuka goti..nikifanya mazoezi linauma goti.

Je nitumie.njia gani.mbadala wa mazoezi ili nifikie lengo.
.nakosa confidence na hili tumbo langu.

N.B Picha Siwezi tuma kwa wale wapenda picha.
Tafuta dawa ya kuharisha, uharishe week mbili tu. Utakuja kunishuruku 2 november
 
Ngoja nikupe science facts, achana na upuuzi wa sijui vinywaji gani wanavyouza watu kukudanganya vinakata kitambi. Miaka 2 iliyopita nilikua na kilo 115, mwili wangu ulivyo mafuta mengi yalikua kwenye tumbo, watu tunatofautiana wapo ambao mafuta mengi wanatunza kwenye mapaja, wengine mgongoni e.t.c. Leo hii nina kilo 75, misuli tupu, fat imeshuka hadi 12% yaani six packs zinaonekana bila hata kuflex. Nimefikaje hapa?

Inabidi ubadilishe lifestyle lako asilimia 100, sitanii hiki ndicho kitu kigumu sana ambacho hata marafiki zangu mabonge wameshindwa kufanya.
1. Fanya mazoezi mno, mwanzoni uanze na full body workout siku tatu kila wiki, baada ya miezi miwili badilisha uanze kufanya siku tano kwa wiki, specilized kwa kila body part.
2. Kula, hili ni jambo muhimu sana kuliko yote na ndilo gumu ambalo 99% hua wanashindwa, inabidi uanze kuhesabu calories unazokula kila siku, vyakula ninavyorecommend ni vyenye protein sana, wanga kidogo, sukari kata 100%, yaani sitaki kusikia unagusa sukari, chai usiweke sukari, kupika chochote usiweke sukari, maandazi sijui nini vinavyowekewa sukari vyote kata 100%, ni ngumu ila baada ya miezi miwili ulimi unakua usharegister palete mpya ya taste unajikuta umezoea, mimi nakunywa chai bila sukari vizuri tu.

Kisayansi, kupunguza mwili inabidi calories zinazoingia mwilini ziwe ndogo kuliko ya zinazotumika, mwili kufanya kazi zake za kawaida kila siku unatumia calories flani, sasa ukila sana kuzidi calories ambazo mwili unahitaji unajikuta calories nyingine zilizobaki zinabadilika kua mafuta mwili unatafuta sehemu ya kuyatunza yanakaa hapo ukitegemea huko mbeleni labda utakuja kuyatuumia sehemu. Sasa ukiingiza calories ndogo mwilini kuliko mwili unazotumia mwili unakosa pa kupata calories nyingine unaanza kula mafuta uliyonayo na wakati mwingine misuli ili uendelee kufanya kazi.

Navyokwambia kula kidogo na fanya mazoezi kwa wakati moja ni kwa sababu kula kidogo kunafanya upate calories chini so mwili utatumia mafuta uliyonayo ili kufanya kazi zake za kawaida, na fanya mazoezi kwa sababu unavyojenga misuli mwili unakua unahitaji calories nyingi zaidi ili kujenga hiyo misuli, kwa hiyo unajikuta mwili wako unabadilika haraka sana kwa sababu unahitaji calories nyingi zaidi ila unaupatia calories ndogo zaidi ya ulivyozoea.

Mambo mengine yooote utaambiwa sijui tumia dawa gani sijui nini ni uongo mtupu, ni watu wanataka kuuza products zao wapige hela basi, hii ndiyo sayansi imefanya kazi miaka elfu kadhaa hadi leo kila mtu unayemuona ana mwili mzuri hii ndiyo principle anayofata basi hakuna kingine.

Na usiogope kufanya mazoezi kama ya kunyanyua vyuma, kama ni mwanamke ukinyanyua vyuma haimaanishi utakua na mwili wa kiume, huna hormone za kiume za kufanya mwili wako uwe mkubwa hivyo, utaishia kua sexy tu basi, wanawake unaoona wana misuli imejaa wengi wanatumia hormone za kiume kuboost. Mazoezi mwanzoni yanauma mno, mimi siku ya kwanza nimefanya mazoezi ya miguu sikuweza kutembea wiki nzima.

Acha kula ugali, ile ni pure carbohydrate, inabadilika kirahisi sana kua fat, kama huwezi basi kula kidogo sana, zidisha mboga hasa nyama, pendelea kuku kuliko nyama nyingine, hasa chicken breast sababu inaprotein nyingi mno, maharage pia, ukijisikia kunywa chai achana na ya maziwa, tumia ya rangi, weka majani ya chai usiweke sukari au kuongeza kitu chochote kunywa hivyo hivyo, ka vipi kata breakfast kabisa ule lunch na dinner tu, na haimaanishi ule kama unakula msosi wa kijiji kizima, ule kidogo tu, calories kama 1500 zinatosha kabisa kwa siku. Fanya hivyo alafu nunua mizani jipime kila wiki utashangaa kila mwezi unapunguza sio chini ya 4kg. Unaweza uliza kama unataka tips za jinsi ya kufanya mazoezi.

TLDR Eat less, Workout more.

Tafadhali kua mvumilivu mno, huwezi ona results ndani ya wiki mbili, results utaanza kuziona kama umekomaa angalau kuanzia miezi miwili mitatu. Na kua sexy kabisa itachukua miaka miwili au zaidi kulingana na wewe mwenyewe umeanzia wapi. Start now, usipoanza leo hutoanza.
 
84KG ni manageable easily.

Nitakua mkweli. Katika kutaka kupungua zoezi kuu inabidi liwe kukimbia ila kwakua goti linakusumbua ukijog unajitonesha hiyo inamaanisha tuskip hiyo phase na turuke moja kwa moja kwenye mazoezi yasiyohitaji goti litumike.

Kama umenotice sijasema diet ni tatizo hiyo ni kwakua kwa ninavyoamini mimi haijalishi unakula nini but if you work harder hiko chakula unachokula kitakua ni fuel yako ya mazoezi.

So unachotakiwa ni kufanya sit ups, crunches, sit ups, kusukuma rollers, fanya squats na kutembea. Usikimbie tembea.

Niliwahi kuandika huo uzi ila nikaufuta ukicheki watu walioniquote mwanzoni utapata the whole scenario

Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Bila healthy diet piga ua huwezi ona mabadiliko hata ufanye mazoezi kama Arnold Schwarzenegger.
You can't outpace a bad diet hata siku moja, uliza kila body builder atakwambia gym ni kama 20% hiyo 80% ni nutrition. Kama unahisi kula ovyo ni fuel ya workout jiandae kwenda gym miaka kumi alafu kitambi kipo palepale.
 
Bila healthy diet piga ua huwezi ona mabadiliko hata ufanye mazoezi kama Arnold Schwarzenegger.
You can't outpace a bad diet hata siku moja, uliza kila body builder atakwambia gym ni kama 20% hiyo 80% ni nutrition. Kama unahisi kula ovyo ni fuel ya workout jiandae kwenda gym miaka kumi alafu kitambi kipo palepale.
Wewe ni gym goer?
 
No wonder yule mwana anataka umfulie nguo....(tuachane na hilo)

Je .umezaa?...kama ni kibonge

Mazoez hayatakusaidia...na kama unapenda kula kula .inabid ujisacrifice tu uache...

Na kitambi kinapungua kwa diet tu na mazoez kwa mbali...yaan inshort inabid uteseke kwelkwel ili kupata hilo tumbo unalotaka
Mkuuu..unavyo tuponda sisi wenye miili yetu..nliivyoona comment yako nkacheka Sana...nkakumbuka yule demu wako Kibonge ulivyokuwa unamchukia.....vipi ulishamuacha?

Mkuu niliiguwa Sana nikawa bed ridden ndo maana nkanenepa..ila fresh napambana kurudisha mwili
 

Attachments

  • 1494408_IMG_20170318_175240_436.jpg
    1494408_IMG_20170318_175240_436.jpg
    17.6 KB · Views: 2
Bila healthy diet piga ua huwezi ona mabadiliko hata ufanye mazoezi kama Arnold Schwarzenegger.
You can't outpace a bad diet hata siku moja, uliza kila body builder atakwambia gym ni kama 20% hiyo 80% ni nutrition. Kama unahisi kula ovyo ni fuel ya workout jiandae kwenda gym miaka kumi alafu kitambi kipo palepale.
Hii nishawai kuiisikia kabisa..
 
Mimi Ni Ke..Nina tumbo kuubwa, nimejaribu njia Tofauti Tofauti ila sijapata matokeo.

Nlikua nafanya mazoezi na nikipata matokeo chanya ..ila nikashtuka goti..nikifanya mazoezi linauma goti.

Je nitumie.njia gani.mbadala wa mazoezi ili nifikie lengo.
.nakosa confidence na hili tumbo langu.

N.B Picha Siwezi tuma kwa wale wapenda picha.
Kwa kweli uzi bila picha ni sawa na kunywa baltika ukitarajia ikupe stimu za chui lite 😅😅😅!!! Tuma kitambi hicho tuone tunaanzia wapi
 
Piga mazoezi tuuh amna namna ruka kamba,kimbia punguza kula kunywa maji mengi two weeks utaona mabadiliko,,,alafu hii tabia yakushindilia dona usiku Kama mpasua mbao kisha unalala wacha mara moja
Hili ndio kosa wengi hufanyaga
 
Hapa labda ukate kichwa kilo 20.
Mkuu...kinyesi hakiwezi kuwa kingi namna hiyo...hili tumbo lilianza kuwa kuubwa..baada ya kuandikiwa Dawa flani hivi hospital..nikawa NAPATA appetite yakula... Nliyoka kilo 64 Hadi 94.. saiv na 84..nataka nipunguze hizi 20..

Nakosa kukiamini nikiwa na mahusinao
 
Mkuu...kinyesi hakiwezi kuwa kingi namna hiyo...hili tumbo lilianza kuwa kuubwa..baada ya kuandikiwa Dawa flani hivi hospital..nikawa NAPATA appetite yakula... Nliyoka kilo 64 Hadi 94.. saiv na 84..nataka nipunguze hizi 20..

Nakosa kukiamini nikiwa na mahusinao
Hahahah mpaka sasa tofauti yako na tembo ni mkonga tu 😂😂😂
 
Back
Top Bottom