Jinsi ya kumlea mwanao wa kiume

USIMUACHIE MKEO AMLEE MTOTO WA KIUME;

~Jukumu ni lako kumfanya awe ngangari

25 mfundishe mwanao.

1. Mwambie marufuku kutoa machozi ukianguka na kuumia

2. Mwambie wanaume tunaoga maji ya baridi na sio vinginevyo

3. Mwambie wanaume wanaoga usiku tu baada ya kazi

4. Mwambie wanaume wanakula vitu vigumu na sio laini

5. Mwambie ugali unashuka bila mboga

6. Mwambie wanaume tunamenya na kutafuta miwa kamili

7. Mwambie wanaume hatukai jikoni na kina mama kupika

8. Mwambie wanaume hatukai na dada zetu kuota moto

9. Mwambie wanaume hatuvai kanga za tukienda kuoga

10. Mwambie wanaume hatulalii tumbo tukiwa ugenini

11. Mwambie akatae majina ya kike hata akiitwa kwa masihara

12. Mwanao akija nyumbani analia mchape mpaka anyamaze

13. Mwanao asivae mlegezo, asikune nazi wala kuchagua mboga

14. Mpe hela mwanao na usimpangie matumizi

15. Mpasue akianza kuandika text kifupi na "xaxa, jomon, oy, aje"

16. Mwambie akongee kwa koromeo sio pua

17. Mzingue akiandika "my birthday.."

18. Kama haangalii ngumi, mieleka zaidi ya tamthiliya mfanye alie

19. Mwambie mwanaume hasusi wala kudhira

20. Mwambie mwanaume hafatilii maisha ya mwanaume mwingine

21. Mwambie mwanaume hacheki mpaka jino la mwisho

22. Mwambie mwanaume hatoi ulimi nje

23. Mwambie mwanaume hakati viuno feni yeye sio demu

24. Hata kama geti kali, mwambie mwanaume anashinda kazini

25. Mwambie mwanao asitafute kupendwa na kila mtu.

Mkuze mwanao kwa misingi hiyo tuongeze wanaume kwa maana mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Ukipata nafasi ya kumwambia mwanao utamwambia nini?
Hahahahahaa mzee kuishi kwa kuogopa ushoga ni Dalili ya ushoga pia.
 
Nakuunga mkono, kwa kifupi dogo atapata shida sana hadi akianza kujitegemea hili somo lazima limnyooshe adabu.

Haya turudi huku sasa upande wa pili, nyie mnaochia single mother walelee watoto wenu, mnakwenda kuwachukua lini ili tuanze training?
 
Unakuta kidume anajipost statuz zinafika 40 ..afu kesho yake anasema anashuruku waliompost wote hao wamekula block mara moja ...maana ni tabia za kike .najua kuna wale wa usimpangie mtu na maisha yake na simu... ila mwanaume kujipost mara 40 ni uboya uliopindukia
 
Maisha hayo niya raha sana yaani hata lije gumu una njia nzuri

Binafsi nimeyaishi hayo maisha utotoni mpaka now

Athari yake ni suala la mapishi kupika maisha yanabadilika sana unaenda sehemu ya mbali na hujui kupika nimeteseka sana na tuliambiwa hakuna kula kwa watu hakuna kuingia ingia hotelini au mgahawani

HONGERA SANA MZEE SIMONOVIC BEST FATHER IN THE LIFE ❤️
 
Back
Top Bottom