Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

acha leo.hakuna dawa zaidi ya kuacha kuvuta leo.au unataka hadi ikutoe roho.Mimi nilivuta zaidi ya miaka ishirini ila nakasema leo basi na ikawa hivyo sasa ni mwaka wa 11.Ilinitesa sana wakati nachumbia mchumba wangu alikuwa hajui kama navuta na alisema kuwa moja ya sababu za kunipenda ni kuwa sivuti sigara(MTIHANI HUO!!!!!) Nikawa sivuti nikiwa nae.Sasa kama tumekaa tunapata kilaji nadanganya naenda nyumbani nikiondoka njiani napitia baa ya pili hapo nachukua sigara tatu zote nazipiga na kilaji ndo niende home.Mateso ya kujitakia SEMA LEO BASI NA IWE HIVYO
 
Kla tabia ni conditioning tu, pia huwez anza na kuacha ghafla fanya iv, ka unavuta sigara 6 kwa cku bc anza kupunguza idad taratb ad 5, bdae 4, bdae 3, bdae 2 mwsho 1 mwil utazoea hatmae utaacha kabsa kmbka hlo zoez sio la mwez au miez 2, lnahtaj mda zaid ya huo,
 
vuta bangi dry utaona sigara zinazingua,
God made grass man made booze who do you trust?
 
Unasema; "Sigara natamani kuiacha lakini nikiiona SM moyo unanilipuka"

Halafu hapo hapo unasema; "Kiukweli nachukia kuvuta Sigara"


Hapo Mkuu huoni kuwa unajipinga wewe mwenyewe na kwa kauli zako wewe mwenyewe? Kutokana na ilivyoandika sifikiri kwako kama itakuwa ni rahisi kuacha kuvuta!

Tatizo linaonekana Mkeo tu ndio kakushikia Bango uache kuvuta...


Ukiweza kuacha tuletee mrejesho humu..
 
Unasema; "Sigara natamani kuiacha lakini nikiiona SM moyo unanilipuka"

Halafu hapo hapo unasema; "Kiukweli nachukia kuvuta Sigara"


Hapo Mkuu huoni kuwa unajipinga wewe mwenyewe na kwa kauli zako wewe mwenyewe? Kutokana na ilivyoandika sifikiri kwako kama itakuwa ni rahisi kuacha kuvuta!

Tatizo linaonekana Mkeo tu ndio kakushikia Bango uache kuvuta...


Ukiweza kuacha tuletee mrejesho humu..

Mkuu kwa kweli natamani sana kuacha na wife kweli hapendi na hata marafiki zangu nao hawapendi, si unajua harufu ya sigara huwa haijifichi? Sasa huwa nakereka sana nnapoongea na mtu alaf ananishutumu na wewe magigara yako yanakera kweli kweli kweli nipo na wakati mgum kweli kweli natamani siku moja niamke alafu nisipende sigara tena
 
Inaweza ikiwa ni vigumu kwa wewe kukubali kuwa umekuwa na utegemezi wa uvutaji wa sigara (addict) kutokana na sumu ya nicotine iliyomo ndani ya tumbaku ambayo husababisha UTEGEMEZI (ADDICTION) Njia ya kukusaidia kuacha ipo unaweza kuwasilinana Narcotics Anonymous (N.A) ambao ni ushirika wa kujitolea usiojinufaisha au jamii ya wanawake na wanaume ambao sigara na dawa za kulevya zimekuwa tatizo kubwa kwao. Hii ni jamii ya watu wanaopata nafuu ambao hukutana mara kwa mara kusaidiana ili kuendelea kuwa safi, maisha bila uvutaji wa sigara au dawa za kulevya.

Hakuna kiingilio au malipo.

Hitaji ni moja tu la Uwanachama, Ni nia ya kuacha kuvuta sigara au dawa za kulevya.

Kwa msaada wa saa 24, Piga simu namba: +255 673 006 962
 
Wakuu nina zaidi ya miaka navuta sigara, nimejaribu kuacha lakini dah inaniwia ngumu mno, kibaya zaidi hadi ndoa haina raha kwa sababu ya masigara, natamani kuacha lakini nikiiona sm moyo unanilipuka naomba ushauri kwa waliofanikiwa kuacha walitumia mbinu gani? Manake ki ukweli nachukia kuvuta sigara lakini nashindwa.


Mkuu fanya hizi chukua paketi nzima ya sigara fumua sigara zote ndani kisha,kisha chukua lile tumbaku lote ulilofumua weka kwenye grasi ya mji weka chini ya kitanda au kwenye friji.hiyo ni jioni nenda kanywe pombe tani yako.ukiamka asubuhi kabla ya kuvuta sigara kunywa huo mchanganyiko wa tumbaku na maji yaliyolala hadi asubuhi baada ya kunya vuta sigara kisha leta mrejesho.



swissme
 
160308174133_a_man_smokes_a_cigarette_640x360_afp_nocredit.jpg

Utafiti wa karibuni zaidi umeonesha kwamba njia bora zaidi ya kuacha uraibu wa kuvuta sigara ni kuacha mara moja.

Utafiti ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Annals of Internal Medicine unasema washiriki walioacha mara moja walikuwa na uwezekano mara 25% zaidi ya kutovuta sigara nusu mwaka baada ya kuachana na uraibu huo wakilinganishwa na walioacha uvutaji sigara taratibu taratibu.

Idara ya Afya ya Taifa Uingereza inasema njia bora zaidi ni kutenga siku fulani kuwa ya kuacha kuvuta sigara.

Weka ahadi, tenga siku na uhakikishe umefanya hivyo siku hiyo, idara hiyo inashauri.

Utafiti huo wa karibuni uliofadhiliwa na Wakfu wa Moyo wa Uingereza ulihusisha washiriki 700 wa kujitolea.

Waliwekwa kwenye makundi mawili, moja la kuacha kuvuta sigara mara moja na jingine la kuacha asteaste.

Baada ya miezi sita, ni 15.5% ya washiriki walioacha kuvuta sigara taratibu taratibu waliokuwa bado hawavuti sigara wakilinganishwa na 22% kwenye kundi la walioacha kuvuta sigara mara moja.

151214100819_bad_boss_woman_smoking_car_640x360_thinkstock_nocredit.jpg

Kiongozi wa utafiti huo Dkt Nicola Lindson-Hawley, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford alisema: "Tofauti inaonekana ni kama inatokana na kutatizika kwa watu katika kupunguza uvutaji sigara. Hili liliwapa jambo la ziada la kufanya, ambalo huenda liliwafanya kuacha kabisa mpango wao wa kuacha uvutaji sigara.”

Ingawa wengi wa washiriki walisema wangependelea sana kuacha uvutaji sigara, bado wale waliofanikiwa zaidi kuacha kabisa uvutaji sigara walikuwa wale walioacha Dkt Lindson-Hawley hata hivyo alisema ni heri kupunguza uvutaji sigara kuliko kutochukua hatua yoyote.

Washiriki wote walipewa ushauri pamoja na vitu vya kuwasaidia kukabiliana na makali ya kuacha uvutaji sigara.

BBC
 
Mie niliacha Mara moja baada ya kuvuta kwa kipindi kirefu sana
Niliamka asubuhi siku hiyo na kusema kuanzia Leo sivuti sigara na kweli mpaka sasa ni miaka kumi na sita imepita na itaendelea kupita
Sigara ni utumwa mbaya sana
 
chains4.jpg



Wanajukwaa

Kwanza nikubali kwamba ipo post ya member wa hapa jf ambaye alijaribu kutoa somo kuhusu jambo hili ambayo inapatikana hapa

Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Lakini baada ya kuipitia na kuisoma kwa umakini nikagundua kwamba mwandishi hakuandika akaelewekaa hasa katika matumizi ya lugha na taratibu za kufuata zikiwepo dalili (symptoms) za kuachana na tabia hii mbaya hasa kwa watanzania wengi ambao hawajaijua vyema lugha ile.

Hapa tutakuwa na uzi mrefu utakaokuwa msaada kwa vijana na hata watu wazima ambao KWA BAHATI MBAYA wamejikuta katika utumwa wa nicotine.

Kwanza ieleweke wazi kwamba KUACHA SIGARA AU ZAO LOLOTE LA NICOTINE ni kama vita dhidi ya mwili (hasa ubongo) wa mtumiaji. Yaani ni vita ndani ya mwili huku sehemu yenye nguvu zaidi katika mwili (mind/emotions/brain) zikisimama kinyume (kwa muda) na matakwa ya conscious thinking (tuiite hivyo kwa sasa)

Wengi wameshindwa kuacha tabia hii kwa kukutana na magumu au majaribu (temptations) zinazopelekea urges (craving) au ile hali ya kujisikia kuvuta tena. Lakini imekuwa kama janga kwamba kwa huku kwetu Afrika ni mara chache sana watu wanaovuta sigara kupewa hamasa ya kuacha KWA KUAMBIWA UKWELI WOTE. Ni kama limekuwa tatizo sugu kwa nguvu ya taifa (vijana).

Hapa tutapena mbinu na dondoo (tips) za kuacha sigara bila kutumia dependancies (sigara za umeme au electronic cigarettes, vidonge vya nicotine au nicotine pills). Kwa lugha ya wenzetu njia hii inaitwa Cold Turkey. Yaani kuacha sigara kwa kujiwekea mkataba na mwili wako kwamba hutavuta kwa ajili ya afya yako, uchumi wako na zaidi MAISHA YAKO.

Mvutaji wa sigara ana chance za kupata aina tofauti za saratani (cancer) 19 hadi 33 kulingana na eneo analoishi pia aina ya uvutaji. Hii ni hatari inayofumbiwa macho kwa kupewa kipaumbele kidogo sana hasa huku kwetu Afica.


COLD TURKEY
Ni njia ya kuacha uvutaji wa sigara kwa kuachana au kuepuka kabisa bidhaa zenye nicotine.
Yaani huhitaji chochote cha kuongeza ili kufanikiwa. Ni kusema sasa basi sivuti tena (NO MORE PUFF!)

Njia hii imekuwa ikitumika duniani kote japo kwa hakika imekuwa ikihesabiwa kama ni njia ngumu ila YENYE MATOKEO MAKUBWA kupita njia yoyote na haihitaji gharama zozote (mara nyingi njia hii hukuongezea kipato kwa kuondoa gharama za sigara)

INAFANYAJE KAZI?
Hapa ndi[po wengi wanapokosea na kujikuta wanarudi tena kuvuta sigara, ipo elimu ambayo wengi huikosa hadi kushindwa kufanikisha malengo ya kuwa na afya njema tena.

HEBU TUANZE SASA KUACHA SIGARA kwa kufuata mtirirkop huu wenye elimu na dondoo muhimu za kukusaidia wewe na unaowajali kurudisha tena afya na zaidi kupata amani na uhuru kutoka katika GEREZA LA NICOTINE.


1. PANGA TAREHE RASMI
Sikushauri uanze muda huu kuacha sigara yako, hapana, ila unatakiwa kukaa chini na kalamu na karatasi (smartphone au simu yoyote yaweza kuwa mbadala), halafu toka moyoni mwako, kuwa mkweli wa nafsi yako kwa kuandika SABABU zinazokufanya uvute sigara, hii inaweza kuwa makundi (youth gangs) rafiki mmoja mmoja, au muda fulani (wengi hupenda kuvuta wakiamka tu) au kama ni occasions (sherehe, makutano, vijiwe). Hii itakusaidia kupanga kwamba hadi lini utakuwa umepata mbadala wa jinsi ya kuanza kuzitambua triggers (kitu kinachokufanya uwashe sigara na kuitia mdomoni.)

2. ANZA MWANZO MWEMA
Baada ya tarehe kupatikana (nashauri iwe ndani ya siku 21 (ishirini na moja toka ulipoona bandiko hili). Hatua inayofuata ni kuondoa (ikiwezekana kuharibu na kuvunja) vifaa vyote vya kuvutia sigara ZIKIWEMO SIGARA ZENYEWE. Hapa sio lazima tuvikute jalalani kwako, hapana, waweza kuamua tu kuviweka mbali na wewe (kumbuka unayepambana naye yuko mwilini mwako ila hawezi kuwasha sigara hadi mikono yako imsaidie). Pia wengine hasa wale waliotumia sumu hii (no citation needed) kwa muda mrefu huamua hata kujipatia kijisafari cha ghafla ili kujaribu kukaa mbali na triggers.

3. SIKU YA KWANZA BILA NICOTINE
Hapa ndipo palipo na ugumu na ndipo wengi huamua kurudi nyuma, na wengi tumewahi kuangukia hapa, (mara nyingine kujaribu na kushindwa bila kukata tamaa ni njia mojawapo ya kuandaa mazingira mazuri ya jaribio lifuatalo) Lakini kumbuka ukishakuwa umejiwekea malengo ya kuacha, yatimize pale unapoanza ili kupunguza chronic effects (madhara ya kujaribu mara nyingi bila sababu wakati ungeweza mara ya kwanza tu kama ungepuuza (ignore) kichochezi).

Zipo dalili na magumu (yenye faida) kipindi mtu anaanza kuijali afya yake (mvutaji).
Nitazipanga kulingana na MUDA

DAKIKA 90 ZA KWANZA
Mwili umeanza kuhisi kukosa "kitu cha muhimu" ilichokizoea kwa kila siku. Ubongo unaanza kuziamsha nicotine receptors (vipokezi vya kemikali sumu za sigara kwenye ubongo) na hapa mvutaji huyu wa zamani anajikuta anapata hamu kali zaidi ya kuvuta sigara, ubongo unafuta vitu vyote vya msingi na kuiweka sigara namba moja. Hii inatokana na bond ambayo nicotine huiweka kwenye ubongo hasa upande wa unconsciousness needs ( yaani mahitaji ya ubongo yasiyoratibiwa na maamuzi yako.)

Dalili
Mwili kuwa mchovu bila sababu
Mdomo kuwa mkavu wenye emptiness (kuhisi kuna kitu kimepungua mdomoni)


Masaa 24 ya kwanza (siku moja)
Hapa mwili unakuwa umepunguiza hadi 64% asilimia ya nicotine kwenye damu (asilimia zinategemea mtu na mtu lakini haiwezi shuka chini ya 51%). Katika stage hii kuna vitu vya kuzingatia ili kubaki halali (hakuna anayependa harufu ya moshi wa sigara). Naposema kuwa halali namaanisha KUWA BILA SIGARA. Vitu vya kuzingatia ni

* Epuka vinywaji vyenye caffeine kwa wingi, kama kahawa na soda nyeusi.
Hizi huufanya ubongo kuwa active zaidi na kupelekea mvuta sigara wa zamani (wewe) kupoteza usingizi na hata kuweza kupelekea sleeping disorders (matatizo ya usingizi).


* Kula matunda yenye asidi (acidic fruits) kwa wingi.
Matunda haya ni kama zabibu, machungwa, malimao, apples au hata embe japo ina acid kidogo sana. Haya husaidia kupunguza uhitaji (cravings) wa sigara kwa wakati huo, pia husaidia kumeng'enya (ni kama kuvunja-vunja) nicotine kutoka katika damu yako na kuitoa nje kupitia mkojo. Hii itakusaidia kupunguza pia dalili (symptoms) za kuachana na sigara.


MASAA 72 (SIKU TATU)
Unapokamilisha siku tatu za kwanza bila sigara (nasisitiza BILA MOSHI WA SIGARA) mwili unaanza kufuta mahusiano ya matukio au mahali na uvutaji wa sigara, Kile ulichokuwa ukikifanya kwa siku tatu hizi katika muda wa cravings (uhitaji wa sigara) KINAKUWA KIMESAJILIWA KAMA MBADALA RASMI WA SIGARA.

Pia mwili unakuwa na kiwango cha nicotini kisichozidi 7% katika damu na brain receptors (kumbuka ubongo huanza kuzijenga upya neva zako masaa 3 tu baada ya kupuliza moshi wa mwisho). Vya kuzingatia USIWEKE TENA SUMU MDOMONI, HAMU YA SIGARA ITAKUSUMBUA TU KWA DAKIKA ZISIZOZIDI 3 (TATU). Tafuta cha kufanya, jiweke busy, endelea kunywa maji ya kutosha na matunda yenye asidi. Pia tegemea hasira na ghadhabu za bila sababu (ubongo unakuwa unapambana na wewe bila mafanikio NA NI HAKIKA UKIWEKA NIA UNAUSHINDA.)



SIKU 7
Sasa hamu ya kula (appetite) imerudi japo si kwa 100%, sigara inakuja kichwani mara chache kwa siku (mara 2 mpaka 4) ukilinganisha na siku 3 za kwanza (mara 8 mpaka 100 kwa siku kulingana na ulikuwa mfungwa wa nicotine kwa muda gani na ulinunua kiasi gani)

Lakini siku ya saba sigara inaanza kuingia kwenye list ya vitu vilivyopitwa na wakati katika akili yako. Si kwamba hutaitamani tena, hapana, ila haitakuwa na nguvu kama siku 3 za kwanza. Hii inatokana na ratiba mpya ya maisha uliyoianza.

Siku 30 (mwezi 1)
Hongera sasa huna nicotine kabisa katika mwili wako, na utavuta sigara tu kwa sababu mwenyewe umetaka (si kwa msukumo wa ubongo).

KUMBUKA SIGARA MOJA TU ITAKUFANYA UANZE MZUNGUKO HUU MWANZONI KABISA,
linganisha kati ya sigara moja na muda ulioutumia kuziepuka sigara 90 (mtumiaji wa kawaida huvuta kuanzia sigara 3 mpaka pakiti kwa siku, hivyo mara siku 30 ni wastani wa sigara 90)

JIPONGEZE KWA KUHAMISHIA PESA YA SIGARA KATIKA MAENDELEO YA AFYA YAKO

BAADA YA SIKU 30 MPAKA 45, KAZI HUWA NI RAHISI KAMA KUEPUKA TU KUWASHA SIGARA TENA


MATOKEO YA KUACHA SIGARA (MAZURI NA mabaya KAMA YAPO)

1. Uzito unaongezeka hadi kilo 8 mpaka 15 (kulingana na mtu) hii inatokana na insulin (dereva wa sukari mwilini) kuanza utendaji kazi tena baada ya kupokonywa kazi yake na nicotine.

2. Oksijeni (oxygen) (hewa tunayovuta ili kuwa hai) inakuwa nyepesi zaidi kifuani, huku mapafu na koo vikiacha utalishaji wa tars (au makohozi) yasiyo na lazima

3. Furaha halisi inarudi, (sasa furaha haitegemei kiwango cha nicotine mwilini)

4. Poteza marafiki wavutaji (mimi napenda kuwaita askari wa gereza la nicotine)

Ongeza za za kwako kulingana na sababu za wewe kuacha.



mods uzi huu usiunganishwe na ule na ikiwezekana uwekwe sticky ili uwe msaada kwa wengi wa Watanzania hasa vijana wanaopotea katika gereza dhalimu la nicotine

N.B muongozo huu ni kwa mujibu wa uzoefu wangu, (mimi pia nimetoroka gereza hilo la nicotine nilikotumikia kifungo cha miaka minne 4, kabla ya kutoroka january mwaka huu na sitamani kurudi tena) pamoja na msaada wa internet.



Best Wishes On Your Quitting!!

losangelessmokingcessationprograms.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom