Jinsi wauguzi wanavyonyanyaswa

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mimi ni muuguzi niliyemaliza shahada ya uuguzi katika chuo kikuu cha sayansi za Afya Muhimbili MUCHS sasa kikiitwa MUHAS. Nina zaidi ya miaka 5 tangu nimalize chuo, lakini sina ndoto za kuajiriwa na serikali kwa jinsi sisi wauguzi wenye shahada tusivyothaminiwa na serikali yetu.


Ni takribani zaid ya miaka 19 tangu serikali ianzishe Kitivo cha Uuguzi katika Chuo kikuu cha Muhimbili. Lakini mpaka hii leo serikali haina dira ya namna ya kuwatumia hawa wauguzi. Nasema hivyo kwa sababu, Wizara ya Afya na ustawi wa jamii na watu wa Utumishi hawana Muundo muundo wa utumishi kwa wauguzi wenye Shahada. Imefikia hatua ya wauguzi wenye shahada kunyanyasika pale wanapopata Ajira za serikali. Wanapopata hizo ajira, wanaajiriwa kama wauguzi waliomaliza stashahada na kupewa mishahara kama ya wauguzi wenye stashahada. Huku ni kudharau taaluma. Maana sidhani kama ikitokea siku Mbunge apewe posho ya Diwani itakuwaje. Patakuwa hapatoshi, iweje sasa hawa wauguzi wafanyiwe hivi?


Hapa serikali inaonyesha kutokuwa na dira kwa wataalamu wake wanaosomeshwa kwa gharama kubwa. Ni kitu ambacho hakiniingii akilini kwamba muuguzi anamaliza shahada, na serikali inampa kazi na mshahara sawa na muuguzi mwenye stashahada. Kwa mtaji huu "Brain drain kwa Tanzania utakuwa wimbo usioisha.


Serikali hasa hasa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii imeonyesha kukosa mwelekeo na umakini pale inapokuwa inawaajiri wauguzi wenye shahada kwa nadaraja na ngazi za mishahara tofauti. Kuna wale wanakadiliwa tu bila kuwa kupewa ngazi yoyote ya Mshahara na kuna wale wanao


NIMEBAHATIKA kuongea na mmoja wa wauguzi wenye shahada ya uuguzi (B.Sc.Nursing) ambao waliajiriwa na Wizara ya Afya na ustawi wa jamii kama Afisa muuguzi daraja la III (NO III) daraja ambalo ambalo anaanza nalo muuguzi aliyehitimu stashahada. Muuguzi huyo alikubali ajira na kulipoti katika kituo chake cha kazi lakini kwa kutoridhika na daraja hilo pamoja ngazi ya mshahara akamwandikia Katibu Mkuu wa Wizara kuhusu kuomba kubadilishiwa daraja na ngazi ya mshahara ili viendane na kiwango chake cha elimu. Maskini ya mungu muuguzi huyo hakusaidiwa chochote.


UAMUZI uliochukuliwa na muuguzi huyo ni kumwandikia Katibu Mkuu barua ya KUSITISHA ajira. IFUATAYO NI SEHEMU YA BARUA ALIYOMWANDIKIA KATIBU MKUU:-

_____________________________________________________________________






"DAR ES SALAAM

KATIBU MKUU

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

S.L.P

DAR ES SALAAM


Ndugu,

YAH: KUSITISHA AJIRA KWA MUDA


Husika na kichwa cha habari hapo juu. Mimi….(Fulani) ninasitisha ajira yangu kwa muda kama Afisa Muuguzi daraja la III, kwa mujibu wa barua ya ajira ya tarehe…..ambapo niliajiriwa kufundisha katika chuo cha……..(jina linahidhiwa) . Nilipokea barua ya ajira na kuripoti katika kituo changu cha kazi na hatimaye kuanza kazi


Mimi nimemaliza shahada ya Uuguzi ( Bachelor of Science in Nursing-B.Sc. N ) katika chuo kikuu cha sayansi za Afya Muhimbili mwaka 2005. Niliomba ajira Wizarani na kuajiriwa kama Afisa Muuguzi daraja la III (NO III) na kuandikiwa kuanza na ngazi ya mshahara ya TGD D (sawa na 260,000); daraja na mshahara ambao anaoanza nao Muuguzi aliyehitimu stashahada


Nimejaribu kuafuatilia katika ngazi zote kuanzia kwa Afisa utumishi,Mkurugenzi wa Utumishi, na kwa aliyekuwa anakaimu na kufanya kazi za Katibu Mkuu bila mafanikio yoyote. Sikuridhidhwa na baadhi ya majibu toka kwa baadhi ya watumishi wa Wizara kwamba


Kwa sasa Wizara haina nafasi za ajira kwa Wauguzi wenye shahada
Wauguzi wenye shahada hawana muundo wa utumishi kwa hiyo ajira zao pamoja na ngazi za mishahara zinatolewa sawa na wale wenye stashahada
Kama sintaridhishwa na daraja hilo, basi nisubiri mpaka hapo Muundo wa utumishi kwa wauguzi wenye shahada utakapokuwa tayari

Nimefikia uamuzi huu wa kusitisha ajira yangu baada ya kutoridhishwa na mchakato mzima wa kuajiriwa kwangu pamoja na majibu wa baadhi ya watumishi wa Wizara hususani maafisa utumishi katika mchakato wa kuomba kubadilishiwa daraja na ngazi ya mshahara. Lakini kinachonisikitisha na kunishangaza kidogo ni kwamba:-


Wauguzi wote wenye shahada ambao wengi nimesoma nao darasa moja walioajiriwa kabla yangu, waliajiriwa na Wizara kama Maafisa wauguzi waandamizi daraja la kwanza (SNO I) na kuanza na mshahara kwa ngazi ya TGS F-3. Nilipojaribu kuomba ufafanuzi kwa maafisa utumishi kwamba iweje hao waajiriwe kama maafisa Wauguzi waandamizi daraja la kwanza na mimi niajiriwe kama Afisa Muuguzi daraja la III na wakati tuna kiwango sawa cha elimu, nikajibiwa kwamba; hao walipewa kipaumbele na kuajiriwa kwa lengo maalumu (special offer) na Wizara kwa kuwa waliajiriwa Kipindi ambacho Wizara ilikuwa inawahitaji na haitatokea kwa mtu mwingine wa aina hiyo.
Wauguzi wote waliohitimu shahada na walio katika mafunzo ya Uuguzi (internship), wanalipwa posho ambayo ni 80% ya mshahara wa Muuguzi mwenye shahada aliyeajiriwa. Kabla ya marekebisho ya mishahara mipya hiyo 80% inakaribia 351,000. Ambapo kwa sasa inaweza kuwa inakaribia zaidi ya 351,000 baada ya marekebisho ya mishahara. Nilipojaribu kuuliza ni hadidu gani za rejea (terms of reference) zinazotumika kupata hiyo 80% ya hiyo posho ya Muuguzi aliyeko katika mafunzo ya Vitendo, nilipewa majibu ya kukatisha tama kwamba kama sitaki ajira niache. Nilitumaini kuwa kigezo kinachotumiwa na Wizara kupata hiyo 80% ya posho ya Intern nurse ndicho kigezo ambacho kingeweza kutumiwa kwa wauguzi wenye shahada pindi wanapoajiriwa na Wizara. Hata mie nabaki kujiuliza, iweje nilipokuwa


Nilikuandikia barua tarehe…..ya kuomba uwezekano wa kubadlishiwa daraja na ngazi ya mshahara kulingana na kiwango cha elimu kama ilivyoonyesha kwenye nakala za vyeti nilivyoambatanisha kwenye barua hiyo. Sikuweza kufanikiwa, na niliambiwa nipeleke tena maombi yangu kwa Mkurugenzi wa utumishi ambaye tayari hapo awali alishaniambia kwamba haiwezekani kubadilishiwa.


Kwa hiyo; ninaandika barua hii kwa lengo la kusitisha ajira yangu, kama Afisa muuguzi daraja la III mpaka hapo muundo wa utumishi kwa wauguzi wenye shahada utakapokuwa tayari kama nilivyoshauriwa na baadhi ya watumishi wa Wizara katika mchakato mzima wa kuomba kubadilishiwa daraja na ngazi ya mshahara ambapo sikuweza kufanikiwa.


Wako katika Ujenzi wa Taifa"

_____________________________________________________________________


Mpaka hapo nikaamini kuwa huni uhuni tu unaofanywa na Wizara ya Afya. Kama kweli serilakli ingekuwa na dhamira na dira ya kweli na wataalamu wake, isingewachukua zaid zaidi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa program hii ya shahada ya uuguzi na kuiacha bila kujua wataalamu hawa wakimaliza watakuwa akina nani na wataajiriwa na serikali kwa daraja na ngazi ipi ya mshahara


Nakumbuka katika mgomo ulitokea pale hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2005 uliofanywa na madaktari na wauguzi walikuwa wanafanya vitendo kazini kudai nyongeza ya posho kuna siku ilitololewa sentensi moja na kondakta wa daladala ambayo ilituacha hoi. Baada ya kondakta huyo kujua kiasi walichokuwa wanalipwa madaktari alicheka kisha akasema 'Kumbe hawa madaktari wanajishebedua kumbe wanalipwa mshahara ambao haufikii hata posho nayoipata mimi kwa mwezi'

Ni katika mazingira haya ambayo aliyekuwa Mkurugenzi wa uuguzi pale Muhimbili hospitali kipindi cha mgomo wa mwaka 2005 ambapo alikuwa anawalazimisha wauguzi waliokuwa katika mafunzo katika vitendo kufanya kazi usiku bila kutoa motisha yoyote au night allowance ilhali madaktari wao wakiingia usiku au kuwa kwenye list ya ‘call’ wanalipwa. Na izingatiwe kuwa muuguzi ndiye anayekaa na mgonjwa masaa mengi kuliko hata daktari. Na ni muuguzi huyu huyu ambaye anajiweka katika mazingira hatari (risky environment) katika ufanyaji wa kazi. Hakuna hata ile risk allowance inayotolewa kwa hospitali nyingi na hata kama inatolewa basi ni kiasi kidogo sana ambacho hakiendani na mazingira yenyewe anayofanyia kazi muuguzi. Kwa hiyo mazingira magumu wanayofanyia kazi wauguzi, mshahara kiduchu na kutothaminiwa kwa uuguzi kwa ile dhana kwamba uuguzi ni kazi ya wito ni vitu vikubwa vinavyochangia kuzorota kwa huduma za kiuguzi na kazi kutofanyika katika kiwango kinachotakiwa. Kama kweli uuguzi ni wito, basi wauguzi wote kila mwisho wa mwezi wapewe kuponi za kuchukua bure vitu madukani,kulipia nyumba na wao wapande bure magari ya daladala. Ninaipongeza serikali kwa jitihada inazofanya katika kuboresha mishahara ya wafanyakazi hususani wafanyakazi wa afya, lakini kwa hili la kusahaulika kwa wauguzi waliomaliza shahada na kuonekana kunyanyasika pindi wapatapo ajira serikilini ni jambo linalotakiwa kuangaliwa kwa kina nakupatiwa ufumbuzi wa haraka. Mpaka sasa ni wauguzi wengi sana ambao wameshahitimu na kutunukiwa shahada. Cha kushangaza ukienda ma hospitalini huwakuti. Hii inatokana na mazingira na mfumo wa utendaji wa wizara haujaliangalia na kutekeleza swala la hao wauguzi kuhusu muundo wa utumishi ambayo nadhani utasaidia kuonyesha ni daraja gani anaaingia nalo kazini. Nadhani mpaka serikali kuamua shahada ya uuguzi hapa nchini ilikuwa imeshakuwa na muono wa mbele (vision) kuhusu hii kada. Lakini nashangaa ni zaidi ya miaaka 20 bila hata muundo wake wa utumishi kutekelezeka na kubaki kuwaweka kundi moja na waliomaliza stashahada katika ngazi ya ki utendaji


M BARABU
 
Back
Top Bottom