Jinsi Siku ya Wanawake Duniani inavyopotosha wanawake

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,722
15,701
Vuguvugu hili linaloonekana linania njema lakini kinyumenyume linatengeneza tatizo kubwa kwa wanawake na familia.

Linamfanya kila mwanamke ajione kama anaonewa na kunyimwa haki za msingi hata kama anazo.

Matokeo ya mafanikio ya vuguvugu hili ni pamoja na:

1. Kuzalishwa kwa kundi kubwa la wadada na wamama ambao wataona hata kuolewa ni uonevu.

2: Ndoa nyingi kuvunjika.

3: Ongezeko la kasi la wanaume waliovunjika moyo kujituma kutekeleza wajibu wao kama kichwa cha familia maana kuna kichwa kipya kinajitutumua.

4: Kushamiri kwa kasi kwa kundi kubwa la wafuasi viburi wa upinde wa mvua.

My Take.
Tuhamasishe haki za binadamu sio kundi flani mahususi.

Licha ya binadamu kuwa sawa mbele za Mungu mwanamke na mwanaume wameumbwa tofauti kibaiolojia,kihisia na kiakili na hivyo kimajukumu wanatofautiana kwa kutegemeana ( complementary gender roles distinctions).

Nini Maoni yako?
 
Paragrafu ya kwanza umemaliza kila kitu, tusione mambo haya ni mazuri kama tunavyoona kwa nje, ndani ni uharibifu mtupu wa familia.

Baadae matatizo ya kifamilia yakitokea jamii inashindwa kuelewa chanzo cha matatizo hayo.

Sasa hivi kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili ya jamii yakianzia ndani ya familia, malezi ya watoto ni mabovu, ukiangalia kwa darubini kali utaona chanzo ni hizi harakati za wanawake kutaka uhuru wao
 
Naunga mkono hoja, wabaki kuwa submissive kwa wanaume kama walivyoamriwa........kujitia ujuaji ni kujitafutia maangamizi ya kizazi chao wenyewe, wasidanganywe na hao mabeberu wanaosukuma agenda za kishetani za kuvuruga taasisi ya ndoa na familia.​
 
Mnang’ang’ania sana swala la nyinyi kuwa kichwa cha nyumba sijui mkuu wa kaya kwani nani kawapokonya hayo mamlaka? Mnaogopa nini

Kama inafahamika hivyo tangu vizazi na vizazi mbona mnatumia nguvu kubwa ku prove kitu ambacho kipo? Stay on your lane na msikwepe responsibilities zenu kama wanaume. Kuna kipande mnakiruka mnaparamia mada ya kwamba wanawake wana potoshwa.
 
Vuguvugu hili linaloonekana linania njema lakini kinyumenyume linatengeneza tatizo kubwa kwa wanawake na familia.

Linamfanya kila mwanamke ajione kama anaonewa na kunyimwa haki za msingi hata kama anazo...
para ya kwanza tu ujumbe tayari umefika
 
Single mother tulia ...Hauna ubavu wa kupambana na mwanaume kimaumbile endelea kujidanganya na kingereza chako cha ugoko
Mnang’ang’ania sana swala la nyinyi kuwa kichwa cha nyumba sijui mkuu wa kaya kwani nani kawapokonya hayo mamlaka? Mnaogopa nini...
 
Nimejaribu kuangalia mahojiano mbalimbali kuhusu siku hii, asilimia kubwa ni wanawake wasio na ndoa, sasa sijui wanaleaje watoto wao peke yao bila baba?

Kuna sababu gani mama kuishi peke yake bila mume wakati kuna wanaume tele wanahitaji wanawake? Tunachotaka ni kutunza maadili ya ndoa, watoto walelewe katika misingi ya familia bora.

Hata kama mama ana uwezo mkubwa wa kifedha haifai kuishi na watoto wake bila baba. Baba ni muhimu sana katika familia
 
Ukitaka kujifunza jambo kuhusu New World Movement angalia replies hapa jukwaani kuhusu hii issue ndipo utajua hatua kadhaa mbele tunaelekea wapi?.
 
Back
Top Bottom