Jinsi Lowassa alivyojichomeka sherehe za RC Ifakara na kumchefua kardinali Pengo

kwa lowassa kushiriki masuala ya dini hakuanza leo wala jana hiyo ni utashi wake binafsi na mola wake, mimi nadhani kwenye hili hana kosa jamaa ki ukweli ni mchapa kazi sana katika kundi lao wana ccm mimi namuona angalau yeye anafaa kuliko wafuata upepo wengine
 
Sawa mkuu kwa hiyo hiyo kauli ni ya pengo kama pengo na wala si tamko la kanisa katoliki kwa kuwa pengo si msemaji wa kanisa katoliki
Mkuu KIMBYNGA, Cardinal popote anapokuwa anamwakilisha Pope. hata balozi wa vatican anakuwa chini yake. Hivi katika Tec ana-special seat.
 
MWADHAMA Polycarp Kardinali Pengo, amesema kanisa siyo mahali pa "kujisafisha na kujijenga kisiasa."

Amesema kanisa halipaswi kufanyiwa majaribio ya kugeuzwa kuwa uwanja wa watu kujisafisha na kujijenga kisiasa, limeeleza gazeti la kanisa Katoliki, Kiongozi.

Pengo alikuwa akikemea kilichotokea Ifakara, mkoani Morogoro, 19 Machi 2012, ambako Edward Lowassa "alihutubia" sherehe za kuzinduliwa kwa jimbo jipya la Katoliki.

Mbali na kuzinduliwa kwa jimbo, sherehe zilihusu kusimikwa kwa Askofu Salutaris Libena kuwa askofu mwasisi wa jimbo hilo.

Gazeti la Kiongozi, toleo la 30 Machi 2012, lilikuwa likinukuu Radio Tumaini inayomilikiwa na jimbo kuu la Dar es Salaam.

Kardinali Pengo ni askofu mkuu jimbo kuu la Dar es Salaam.

Amesema, "… jambo ambalo ni lazima kulikwepa, ni kwamba kwa namna yoyote, kanisa katoliki halipaswi na lisifanywe uwanja wa siasa; lisigeuzwe kuwa ni uwanja wa mapambano kwa wanasiasa; wanasiasa wana ya kwao, wafanye shughuli zao hukohuko.

"Sio mtu anashindwa kujieleza katika ulingo wa siasa, anakuja kukimbilia ulingo wa Kanisa na hapo anaanza kujinadi na kutoa maoni na vitu vingine kama hivi. Hii si sawa na hiyo ndiyo athari inayoweza kujitokeza iwapo hatutalinda mfumo wa kanisa," amesema.

Katika hali isiyo ya kawaida, kwenye sherere za kanisa Ifakara, mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliyepewa heshima ya kukaribisha Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alikacha maelekezo hayo na kumwita Lowassa kwanza.

Hatua hii ndiyo Kardinali Pengo amelaani kuwa ilikuwa kinyume na ratiba iliyopangwa. "Lowassa hakualikwa kama mgeni rasmi na hakuwa miongoni mwa wageni walioandaliwa kuzungumza lolote wala kupanda jukwaani, bali alichomekwa."

Amesema ni kweli Lowassa "…alialikwa afike, lakini sio kama mgeni rasmi kiasi kwamba asimame azungumze yale aliyoongea. Hiyo haikuwapo; haikuwapo kwa sababu wamekuja wageni wangapi ambao wangesimama na kuongea…."

Habari kutoka MwanaHalisi
 
Sikilizieni Hotuba ya Nyerere ya mwaka 1995 ktk mkutano wa CCM - Dodoma. Huyu Kardinal anasema baada ya mtu kuhutubia yaani sherehe ya kanisa Lowassa aliingia vipi jukwaani kama hakualikwa..Mambo mengine bana sasa kama Lowassa akisiomama ndfio inaharibu jina la kanisa na dini au sii kweli kwamba kanisa lipo kuwapokewa sinners na kuwaongoa..

Hata sielewi kwa nini dini wanaziingiza ktk siasa. Biblia inasema wazi kwamba Ukiristu umekuja kwa ajili ya wakosefu, watu kama kina Lowassa kuwaweka sawa sasa mnapowakana ina maana gani...
 
Sikilizieni Hotuba ya Nyerere ya mwaka 1995 ktk mkutano wa CCM - Dodoma. Huyu Kardinal anasema baada ya mtu kuhutubia yaani sherehe ya kanisa Lowassa aliingia vipi jukwaani kama hakualikwa..Mambo mengine bana sasa kama Lowassa akisiomama ndfio inaharibu jina la kanisa na dini au sii kweli kwamba kanisa lipo kuwapokewa sinners na kuwaongoa.. Hata sielewi kwa nini dini wanaziingiza ktk siasa.

Biblia inasema wazi kwamba Ukiristu umekuja kwa ajili ya wakosefu, watu kama kina Lowassa kuwaweka sawa sasa mnapowakana ina maana gani...

Amesema ni kweli Lowassa "…alialikwa afike, lakini sio kama mgeni rasmi kiasi kwamba asimame azungumze yale aliyoongea. Hiyo haikuwapo; haikuwapo kwa sababu wamekuja wageni wangapi ambao wangesimama na kuongea…."
 
kilichotokea ni hiki..lowasa baada ya kufika alipenyeza ujumbe wake kwa mkuu wa mkoa wa morogoro....wakati mkuu wa mkoa anaongea ili nae amkaribishe mgeni rasmi (ali hasani mwinyi) ndipo mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo badala ya kumkaribisha mgeni rasmi yeye akasema ''kabla ya mgeni rasimi kusimama naomba kumkaribisha waziri mkuu msataafu edward lowasa aseme machache...

kitendo hiki kilimchafua sana kadinali na hata baada ya sherehe kuisha lowasa alitaka kupiga picha na kadinali lakini kadinali alikataa kupiga picha akaondoka na kwenda kuvua mavaz maalumu ya ibada....bado lowasa alilazimisha kupiga picha na kadinali...
 
Hapa kuna propaganda fulani zinapigwa. Lowasa ni muumini kama waumini wengine. So sidhani kama pengo anaweza kuwa na chuki na lowasa kiasi hicho. Otherwise kanisa litakuwa linafanya siasa
 
Amesema ni kweli Lowassa "…alialikwa afike, lakini sio kama mgeni rasmi kiasi kwamba asimame azungumze yale aliyoongea. Hiyo haikuwapo; haikuwapo kwa sababu wamekuja wageni wangapi ambao wangesimama na kuongea…."
Hizi ni sherehe za Ufunguzi wa jimbo la kikanisa, Lowassa kama alialikwa kuna ubaya gani kusimama jukwaani ikiwa dini haibagui mtu?. Kardinal ni mkubwa kuliko Lowassa, ni mkubwa zaidi wa kutotafuta publicity za kisiasa bali za kiimani, yeye angemwita Lowassa ktk kile chumba cha kuungama au ofisini mwake akawambia Ungama!... au sitaki kukuona ukishiriki ktk mambo ya kanisa na pia kuwatumia maagizo viongozi wote wa kanisa kama kweli hataki..Mimi nadhani angetumia muda wake mwingi kujaribu kumwokoa huyu mtu badala ya kumtangaza magazetini kama anajipendekeza wakati kila mahala anapokelewa na viongozi wa makanisa.
 
Watu wengine bwana! Pesa zake mnataka alafu hotuba zake hamtaki, na bado mpaka 2015 mtajua El ni nani Tanzania hii
 
Huwa si msupport kabisa lowassa lakini kwa hili . Mapengo anakuwa Kama sio kiongozi wa dini au kashalewa na madaraka?
 
Sikilizieni Hotuba ya Nyerere ya mwaka 1995 ktk mkutano wa CCM - Dodoma. Huyu Kardinal anasema baada ya mtu kuhutubia yaani sherehe ya kanisa Lowassa aliingia vipi jukwaani kama hakualikwa..Mambo mengine bana sasa kama Lowassa akisiomama ndfio inaharibu jina la kanisa na dini au sii kweli kwamba kanisa lipo kuwapokewa sinners na kuwaongoa..

Hata sielewi kwa nini dini wanaziingiza ktk siasa. Biblia inasema wazi kwamba Ukiristu umekuja kwa ajili ya wakosefu, watu kama kina Lowassa kuwaweka sawa sasa mnapowakana ina maana gani...

Mkuu Mkandara,
Nadhani Mpango wa Lowassa wa kutembelea vyombo vya dini haukubaliki kwa baadhi ya Viongozi wa dini akiwemo Pengo

Kilichotokea Ifakara ni kuwa hiyo ilikuwa sherehe ya kidini, lakini na serikali ilialikwa na Raisi mstaafu ALi Hassan Mwinyi ndio alikuwa mwakilishi wa Serikali kwenye sherehe hiyo,
Kiprotokali Viongozi waliokuwa wanasimamia sherehe hiyo walimuinua Mkuu wa Mkoa(Upande wa serikali) Bw Bendera amkaribishe mwakilishi wa Serikali Mzee Mwinyi,
Alichokifanya Bendera kabla ya kumwinua Mwinyi, akamwinua Lowassa kwanza azungumze, na kiutaratibu wa ile Sherehe kulikuwa hakuna ratiba ya Lowassa Kuhutubia, HILO NDILO LINALOMUUMA PENGO, INAKUWAJE LOWASSA AUTUBIE BILA KUWA KWENYE PROGRAM?, NANI ALIMPA HUO UWEZO?
 
Lowassa kanisa/msikiti -Lowasa -siasa/CCM-Lowassa Urais/ubunge!! Mtu huyu hamumwoni ni hatari na qa kuogopwa sana? Mtu huyu ni kabaila wa siku nyingi/Ni fisadi wa siku za karibuni.Ametuhumiwa/Amesingiziwa/Anatajwa tajwa! Kwanini yeye tuu mbona wengine hawatajwi?Arumeru aliingia kwa kishindo/Arusha alivuruga mambo mtu huyo huyo.Bado hamjamweelewa tuu???
 
Mkuu Mkandara,
Nadhani Mpango wa Lowassa wa kutembelea vyombo vya dini haukubaliki kwa baadhi ya Viongozi wa dini akiwemo Pengo

Kilichotokea Ifakara ni kuwa hiyo ilikuwa sherehe ya kidini, lakini na serikali ilialikwa na Raisi mstaafu ALi Hassan Mwinyi ndio alikuwa mwakilishi wa Serikali kwenye sherehe hiyo,
Kiprotokali Viongozi waliokuwa wanasimamia sherehe hiyo walimuinua Mkuu wa Mkoa(Upande wa serikali) Bw Bendera amkaribishe mwakilishi wa Serikali Mzee Mwinyi,
Alichokifanya Bendera kabla ya kumwinua Mwinyi, akamwinua Lowassa kwanza azungumze, na kiutaratibu wa ile Sherehe kulikuwa hakuna ratiba ya Lowassa Kuhutubia, HILO NDILO LINALOMUUMA PENGO, INAKUWAJE LOWASSA AUTUBIE BILA KUWA KWENYE PROGRAM?, NANI ALIMPA HUO UWEZO?
Yote tisa sherehe ni ya dini, EL na Mwinyi na viongozi wa serikali ni WAALIKWA sasa inakuwaje analaumiwa EL wakati yeye ni mwalikwa na program nzima ni ya kanisa?.. Mbona hawasemi kwa nini Mwinyi alisimama wakati yeye ni Muislaam na fisadi vile vile?..Hapakuwa na sababu ya Kardinal Pengo kuendekkeza magazeti na kutafuta publicity, hataki kumwona EL zipo sheria za kikanisa na yeye ndiye rais wa kanisa hilo hapa nchini, hivyo EL hawezi kwenda makanisani na kujikosha wakati makanisa hayamtaki.. kazi ya kanisa ni kumsafisha EL sio kumkweza wala kumkwaza, ufunguzi huu wa jimbo ni sawa na ufunguzi wa kituo cha maradhi. Kama wanamwona sii msafi, mgonjwa wampokee kwa dua na maombi sio kumtenga kwa sababu za kisiasa.

Mimi sio mkristu lakini navyosikia ni kwamba anayoyafanya EL na kanisa yanatakiwa kuwa siri na yalindwe kama mgonjwa na daktari wake, sasa unapomkataa mgonjwa na kutangaza magazetini sii ndio kusema Kardinal anavunja miiko ya kanisa?
 
EL alialikwa wasimchafue rais mtarajiwa na mkuu wa mkoa hawezi kumuomba atoke mbele aongee na umma bila kuzingatia ratiba,
Msitupotoshe hapa
 
Yote tisa sherehe ni ya dini, EL na Mwinyi na viongozi wa serikali ni WAALIKWA sasa inakuwaje analaumiwa EL wakati yeye ni mwalikwa na program nzima ni ya kanisa?.. Mbona hawasemi kwa nini Mwinyi alisimama wakati yeye ni Muislaam na fisadi vile vile?..Hapakuwa na sababu ya Kardinal Pengo kuendekkeza magazeti na kutafuta publicity, hataki kumwona EL zipo sheria za kikanisa na yeye ndiye rais wa kanisa hilo hapa nchini, hivyo EL hawezi kwenda makanisani na kujikosha wakati makanisa hayamtaki.. kazi ya kanisa ni kumsafisha EL sio kumkweza wala kumkwaza, ufunguzi huu wa jimbo ni sawa na ufunguzi wa kituo cha maradhi. Kama wanamwona sii msafi, mgonjwa wampokee kwa dua na maombi sio kumtenga kwa sababu za kisiasa.

Mimi sio mkristu lakini navyosikia ni kwamba anayoyafanya EL na kanisa yanatakiwa kuwa siri na yalindwe kama mgonjwa na daktari wake, sasa unapomkataa mgonjwa na kutangaza magazetini sii ndio kusema Kardinal anavunja miiko ya kanisa?

Ulipomuita mwinyi fisadi ndio ulipoharibu ulichokiandika chooote!
 
Back
Top Bottom