mwandiga
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 1,506
- 661
Hii imemtokea rafiki wangu wa karibu sana jana 06/3/2012 saa tisa mchana. Kwenye akaunti yake ya M-pesa alikuwa na tsh 35,000 ambazo kwake ni kiasi kikubwa sana cha fedha na alikuwa anauhitaji nazo ndio maana akazihifadhi. Jana mnamo saa tisa simu anayotumia ikaonyesha ujumbe unaosomeka SIMcard registered failed ikapoteza mawasiliano, aliizima na kuiwasha tena lakini ujumbe ukawa huo huo.
Alidhani simu imeharibika akaipeleka kwa fundi na fundi alipoiangalia tu akamwambia simu sio mbovu laini ndio mbovu hivyo ajaribu kuweka laini nyingine naye alivyofanya hivyo ilifanya kazi vizuri tu. Ilibidi apige simu vodacom customer care leo asubuhi na kuwauliza kuhusu hil0 jambo. walimwambia hiyo namba ipo hewaniba. Baada ya yeye kuwaelezea ilivyokuwa jana walimwuuliza maswali mawili matatu ndipo wakamwambia hiyo namba jana ilitoa fedha zilizokuwemo tsh 35,000 na wakataja jina la wakala aliyetoa hizo fedha, huyu bwana kwenda kumuuuliza huyo wakala akakataa kuwa hajatoa hizo fedha.
Kilichofanyika ni hivi huyu aliyeibiwa fedha kwenye M-pesa juzi tarehe 05/3/2012 alienda kwa huyo wakala akampa simu ili atoe fedha kidogo kwa ajili ya matumizi yake, yeye hajui jinsi ya kutoa fedha Mpesa, wakala akamuuliza namba yake ya siri PIN number naye akamtajia kisha akamkabidhi simu na fedha akaondoka zake.
Yule wakala au mtu mwingine aliyekuwepo eneo hilo alisikia ile namba ya siri na kujua namba ya simu ya huyo mteja kishwa akaswap ile namba, wakati huyu mwizi ameswap ile namba ndipo meseji kwenye simu ya aliyeibiwa ikatokea SIMCARD REGISTRATION FAILED nahuyu mwizi akafanikiwa kuwa mmliliki wa namba hiyo na kutoa kiasi chote cha fedha zilizokuwa kwenye akaunti yake hiyo, na vodacom wamemwambia hawana msaada zaidi wa kumsaidia ila aende polisi, alivyoenda polisi akaambiwa atoe fedha tshs 40000 ili waweze kumsaidia.
*Hivi haya makampuni ya simu hayawezi kuweka utaratibu mzuri wa kuswap line za simu badala ya ule wa kutaja namba tano unazopiga sana???????
*Wananchi wengi hawajui au hawaelewi jinsi ya kotoa fedha kwenye akaunti ya mpesa hivyo wanawapa wakala simu zao na kuwatajia namba za siri ili waweze kutoa fedha na huo ndo mwanya wa tamaa na wizi kwani akiona salio kubwa atakuwa na tamaa na pia mara nyingine wanaokaa kwenye huduma za mpesa ni deiwaka tu mara nyingi watoa fedha hawasaini kwenye ledger kama inayotakiwa. Hapa wizi utaendelea sana Kuweni makini.
Soma huu ujumbe na mweleze mwenzio ili achukue tahadhari.