Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo

Ndugu 7seven ebu nipe shuhuda zako, maana zinanijenga sana.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Ahaaa, ahaaaa! Sasa inategemea na mada ambayo huwa ninaiwasilisha hapa Jamvini,endelea kusoma masomo yanayofuata na mada mbali mbali nikizikumbuka na kuziweka hapa utazisoma tu mkuu wangu.

Halafu hii ndio inadhihirisha kwamba mtu kusema mimi Mungu amanitendea jambo fulani na siyo kutumia mifano tu ya kwenye Biblia, maana Mungu ni yule yule wa jana na leo na hata milele.

Ninapenda kuwasisitiza watoto wa Mungu, ikiwa wewe unaye Mungu basi uwe na ushirika wa karibu naye, ifikie mahali useme Mungu amenifanyia hiki na kile. Hapa ndipo unamdhihirisha kwamba yuko ndani yako.Umuone katika ndoto,maono ya usiku na mchana,umuone kupitia majibu ya maombi yako,umuone katika ishara na maajabu katika mambo uyafanyayo kupitia Yeye.

Hapa ndipo utakuwa na ujasiri wa kumuelezea na watu wapendao kumjua Mungu wataamini maana unakuta hata wao walishatendewa hivyo,au wanatamani kutendewa hivyo.

Mungu alitupa nguvu ya kuumba kupitia mikono yetu na vinywa vyetu,sasa kabla hujaanza kufanya kitu chochote kiwe ni mradi wa biashara, shamba,nyumba ,mifugo,elimu,ndoa, watoto n.k ,viumbe kwanza katika ulimwengu wa roho ili vije mwilini vikiwa kamili na viweze kukuletea matokeo chanya kama jinsi ulivyoviumba.

Utajiuliza unaviumbaje?

Ni rahisi sana,viumbe kwa njia ya maombi ya muda mrefu, kwa njia ya kujitamkia baraka,tamani viwe katika hali ya ubora ndani ya moyo wako,vitolee sadaka,uwe na shauku ya mambo kuwa sawa au mazuri hakika vitakuwa sawa sawa na jinsi ulivyoviumba.

Watu wengi wanakwama katika mambo yao kwasababu wanapenda kutengeneza mambo au vitu ambavyo tayari vimeshatokea katika ulimwengu wa mwili kutokea rohoni.

Hapa unakuwa unazuia tatizo au unapambana na tatizo badala ya kushughulika na chanzo cha tatizo. Kila tatizo chanzo chake kinaanzia rohoni,ukionacho katika macho ya damu na nyama ni kitu ambacho kilishakuwepo katika ulimwengu wa roho.

Mimi nitakupa mfano.Nikiwa kijana mdogo sana bado niko shule nilikuwa ninatamani mke wangu awe mzuri sana,mrembo sana,awe anavutia sana,awe na tabia njema hadi awe mfano kwa wengine. Yaani awe "wife material" vijana wa mjini ndivyo mnavyosema.

Nilitamani niwe na shamba kubwa, mifugo mizuri maan ninapenda kufuga kwasababu babu zangu wote walikuwa wafugaji, na mimi nilikuwa nikichunga ng'ombe huko malishoni, hii ipo damuni. Nilipenda niwe na kiwanja kikubwa na nyumba kubwa hata kama situmii vyumba vyote, yaani nilipenda kila kitu changu kiwe kikubwa.

Ila nikawa ninajiuliza nitawezaje kuyafikia haya yote kama sina muongozo, sina nguvu ya kiroho,sina kinga ya kiroho,sina mtaji, sina elimu,je nikipigwa juju na mtu mwenye juju zaidi yangu si nimepigwa kipigo kikali na yote niliyojitaabisha miaka yote si itakuwa kazi bure.?

Nilijaribu kufanya kwa akili zangu lakini nilishindwa, ndipo nikaingia kwenye maombi ,siku ya kwanza ninawekewa mikono nilisikia kitu cha tofauti sana,nilikuwa mwepesi sana,nililala usingizi mzuri sana.

Sikuishia hapo nikaanza kusoma maandiko Biblia yote nimeisoma mara 4,kuanzia mwanzo hadi mwisho. Nikapata picha kwamba kumbe mambo yangu yote yatawezekana ikiwa nitampa Mungu mipango yangu yote.

Sasa nifupishe, mke nilimpata kama nilivyomuomba Mungu kwa jinsi nilivyomtengeneza katika maono na ndoto na maombi yangu.Yaani nina mke mzuri kuliko wanawake wote duniani.

Usijiulize ni mke mzuri kiasi gani,angekuwa ni mbaya nisingemuoa, ningekuwa ninawatamani wanawake wengine huko nje.

Kwahiyo sijui wanaume wenzangu mnawaonaje wake zenu,lakini mimi kwangu ni namba moja,hanipasui kichwa, ni mtiifu kwangu,ni mcha Mungu, ana hofu ya Mungu, nikimtazama machoni pangu ananivutia. Umbo lake Maashallah!! Mungu kamjaalia.

Kwahiyo jinsi ninavyomtazama, wanavyomtazama, wanavyomsfia ndugu zangu maana anaishi nao vizuri pasipo ugomvi,vijana wadogo wanasema wanatamani wawe na mke mwenye tabia kama za shemeji yao.Au mama yao mdogo.Mwaka wa kumi huu tupo kwenye ndoa,sijawahi kuletewa kesi kutoka kwa ndugu yeyote isipokuwa wao ndio wanakuja kwetu tuwasuluhishe.

Ieleweke sijaoa malaika, ila hana usumbufu wala tabia mbovu. Huu unabii ulitimia kwa asilimia 100%.Mwanaume kama unamuona mkeo mbaya atakuwa hivyo hivyo maana unamuumbia ubaya,kama ni wa kushindwa, atashindwa hivyo hivyo maana umeshamuumbia kushindwa.

Tukija shambani wanauliza nimeweka nini shambani mbona mazao yangu mazuri sana,katika watu wote nilionao karibu shamba langu ni zuri kuliko ya kwao, kwanini?

Kabla sijaanza kulima nilimuuliza Mungu akaniambia historia ya pale nyumbani, sadaka za kafara zilizotolewa, maagano yao,mazindiko, viapo vyao walivyoapa. Kumbuka mimi ninatokea kwenye familia za uchifu, na kote huko nilirithi.

Yaani babu yangu mzaa mama alimuachia mama na ndugu zake shamba na nyumba yake na mifugo target ikiwa miye ndio niwe mrithi maana wajomba zangu walishapewa vitu vyao.Kwa utaratibu wa Kiafrika mara nyingi watoto huwa haturithi ujombani,ila mimi ilitokea, ila ilitokea kwasababu maalumu.

Babu wa baba alikuwa mtawala pia huyu ndiye kabisa aliviacha kwangu,sasa umegeuka umekwenda kwa Mungu,miungu ikachachamaa kwanini nimegeuka makubaliano ya mababu zangu(baba yake na babu alishamuambia babu yangu kuwa mtoto wa mtoto wake ndiye atakayerithi na wala siyo watoto wake(yaani baba zangu Ila mimi ndiye niliyechaguliwa ),wanawake wengine wakainua vita,yaani mama zangu wadogo (wake wa baba zangu wadogo kwa wakubwa),wanasema kwanini aka katoto ndio kaachiwe mji, nao wakafanya yao.

Kwahiyo niliona siwezi kuwashinda isipokuwa nina nguvu kuwashinda wao, na si nyingine ila ni nguvu za Mungu wa mbinguni. Ndg zangu asikudanganye mtu kama huna nguvu na ujasiri huwezi kuupata ufalme wa mbinguni. Nilipigana hasa,nilipigana na miungu ya baba zangu na mama zangu,lakini nilishinda kupitia huyu Yesu. Miaka zaidi ya kumi hakikuwa kitu cha kawaida, kama si Mungu nilikuwa niwe mavumbini siku nyingi sana.

Siku moja nikiwa ninaomba sana, na kutapika sana,nikawa nimelala chini sina nguvu maana nilikuwa nimefunga mfungo wa kavu,siku hiyo nilitapika chai niliyokuwa nimenyweshwa siku 7 kabla ya hayo maombi ya mfungo wangu.

Ebu fikiria ,chai umekunywa Jumamosi unakuja kuitapika siku ya Ijumaa jioni wiki inayofuata ikiwa vile vile ,na wakati huo ulikuwa kwenye mfungo wa kutokula kitu chochote. Jiulize ilikuwa inafanya nini tumboni kama ni chai ya kawaida?

Hapo ndipo nikamuuliza Mungu nani amenifanyia hivi,akaniambia ni maagano ya mababu zako,ni mama fulani wa ujombani siku ile ulivyoenda kwake ile chai ndio hii uliyoitapika, na hapa kuna maagano ya kukuaa japo yalifanyika zamani sana ukiwa mdogo lengo ni usirithi hapa wala kupamiliki hapa.

Nikamuuliza Mungu hivi,ikiwa Mungu uliyaona haya yote na ukayajua, kwanini ukayaacha yanipate? Pia moyo wako ni mkubwa kiasi gani hadi ukumbuke mambo yote yaliyofanyika juu yangu ,ya mababu zangu na watu wote waliokufa na walio hai?

Akasema niliyaacha makusudi ili uje uyaombee na ujifunze kwa ajili ya kuja kuwasaidia watu wangu,pia tazama jinsi mbingu ilivyo kubwa ,na Mimi moyo wangu ni mkubwa kama hiyo mbingu,kwahiyo ninayahifadhi yote maana moyo wangu unayo nafasi ya kutosha hata usiweze kusahau.

Kwahiyo ndugu,shuhuda zipo nyingi,hivyo ,umba sura nzuri ya mkeo,watoto wako,mifugo yako,ndoa yako,jifunze kujitamkia maneno mazuri,wazazi wengi ndio chanzo cha kuharibu watoto wao kwasababu wanawatamkia maneno mabaya watoto wao kwasababu ya kupatwa na hasira. Na hasira zisizoisha, wakati Biblia inasema hasira iishe saa 12 jioni,na usiende kutoa sadaka ikiwa una hasira juu ya mwenzako.

Hata kama wana tabia mbaya waombee sana na kuwatamkia maneno mazuri,watolee sadaka, maana kama ni kwa habari ya sadaka nimetoa sana,tena sana,nisingeweza kushinda kama sikuwa na sadaka kwa Mungu wangu.

Mimi nimebarikiwa katika mambo mengi niliyoyaomba, siyo kwamba mimi ni tajiri,hapana,ila yale niliyoyaomba kwa kweli ninamshukuru sana Mungu yamekuwa na ahadi zake kwangu ni nyingi sana bado tu kutokea katika ulimwengu wa mwili.

Ukiweza kuishi katika ulimwengu wa roho na kuumiliki, ulimwengu wa mwili si kitu kwako,utashinda vita zote maana kabla hazijaanza kukushambulia tayari ulishajua kitu kinachoendelea.

Kuna wakati huwa tunalazimika kwenda kwenye ziara ya viongozi wa Kitaifa kwenda kukanyaga mahali kiongozi atakapofikia au kuombea huo mji atakapofikia ili kuzuia roho za aibu ambazo ametegeshewa kiongozi ili kuharibu heshima yake.(Hii ni njia mojawapo katika kitengo cha intelijensia kwenye ulimwengu wa roho),iwe gizani au nuruni kote ni hivyo hivyo.Ndio maana kuna wakati huwa ninaongea mipango ya maadui zangu ambayo wanaipanga juu yangu au juu ya watoto wa Mungu; watu wengine wanadhani kuna mtu ananiambia, si kweli,sisi wa nuruni huwa tunaingia na kutoka gizani na habari zao pasipokujulikana na wao.Giza halijawahi kuishinda Nuru hata siku moja.

Nikupe mfano,hivi kwa mfano Waziri anaenda ziarani halafu anaanza kuhutubia anaanza kuongea maneno ya hovyo, anavua nguo na kukimbia hovyo. Watu watamtafsiri vipi, aliyemteua je atamuonaje,jamii yake au familia yake itamuonaje?

Kwahiyo tukishaambiwa hivyo aidha tutaomba juu ya aibu yake iondoke, au itabidi twende au mtu aende, na utaenda kwa nauli yako pasipo huyo kiongozi kujua.

Hata kama yeye ni mdhambi ila Mungu anaheshimu mamlaka za hapa duniani maana zimepata kibali kutoka mbinguni, na sisi tu mawakili wa Mungu hapa duniani. Pia huyu kiongozi ni kiongozi wa watu wa Mungu.

Kwahiyo watu wanahangaika kujua madhaifu ya Biblia ni kwasababu hawana Mungu wala kumjua Mungu wakiwemo baadhi ya watumishi wajiitao watumishi wa Mungu. Ukimjua Mungu ni zaidi ya kutumia maandiko, ni zaidi ya kwenda kanisani,ni zaidi ya ishara na miujiza. Hata ikiwepo miujiza utajua kuwa hii ni fake au siyo fake.

Siku ukisikia mtumishi anasema anamjua Mungu muulize huyo Mungu amekutendea jambo gani,akikujibu utajua tu huyu anaiga au hamjui kabisa kwa jinsi anavyomuongelea, au hajajifunua kwake zaidi,na utajua kwa matendo haya hakika huyu anaye Mungu.

Huwezi kumjua Mungu kama huna ushirika binafsi na huyo Mungu wako,Bible kuwa ni ya kweli au si ya kweli haimfanyi Mungu kutokuwepo, ila Bible imewekwa kutupa njia ya kumjua Mungu, na aliyeiweka ni Yeye mwenyewe.

Watu wengine wanasema nani aliyeandika kitabu hiki na kile, kwamba kama ni Mungu kwanini kiko na hivi na vile,wasichokijua ni kwamba Mungu anamtumia mtu kuandika au kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa kwa jinsi jamii hiyo ilivyo,na kwa uelewa wa hiyo jamii husika.

Kwahiyo anatumia uwezo wa elimu wa huyo mtu,fikra, mazingira yake,hali yake ya kiuchumi, uwezo wake wa kupambanua roho,nguvu zake za kiroho,utamaduni wake, Mila zisizofungamana na nguvu za giza,n.k.

Kwahiyo ninayoyaandika nayaweza kuja kutumika huko baadaye na kizazi hiki au kingine kama reference kwenye mambo ya kiroho,kwasababu hata sasa kuna watu wanayatumia kama.maombi na wanafunguliwa. Ingekuwa ni kwa utashi wangu wasingefunguka, lakini wanafunguliwa kwasababu ni zaidi ya maandishi, yana uhai, yana nguvu za Mungu maana yake yana uvuvio wa Roho Mtakatifu.

Sasa nami niwaulize watu,haya ninayoyaandika, ninayaandika kwa MAMLAKA IPI,KWA UWEZA UPI,KWA WATU GANI?

Kama ni kwa utashi wangu wayapuuze ila kitakachowatokea wasimlaumu mtu, ila kama ni kwa kutoka kwa Mungu na uvuvio wa Roho Mtakatifu basi watu waamini na kutubu.

Hii yote ni kwasababu gani,watu wengi hawaujui ulimwengu wa roho,UJUE ULIMWENGU WA ROHO ILI UPATE KUISHI MAISHA YANAYOMPENDEZA MUNGU SIKU ZOTE.

Mungu awabariki sana ,ninawaombea neema ya Yesu Kristo iwe ndani yenu mvuke salama mwaka huu,mmalize salama,na mwaka ujao 2024 ukawe kheri na wenye kufanyika kuwa na baraka nyingi juu yenu,Mungu awabariki sana watu wa Mungu, AMANI YA KRISTO IWE NDANI YENU KWA WINGI ILI MUISHI MAISHA MASAFI MBELE ZA MUNGU, AMEN.

28.12.2023.
 
Amina
 
JE,UNAOTA NDOTO KISHA UNAZISAHAU,AU HUOTI KABISA?

Ndoto ni njia mojawapo ya kuwasiliana na Mungu, mbali na maombi kama njia ya kuongea na Mungu lakini wanadamu tunapata taarifa za mbinguni na kuzimu kupitia njia ya ndoto.

Mungu anaongea na kila mtu kupitia ndoto,haijalishi mtu huyo ni msafi sana au mchafu,bado Mungu ataongea naye kuhusiana na habari za mambo yake.

Ndoto hutofautiana kati ya mtu na mtu,au kiwango cha uotaji wa ndoto kati ya mtu na mtu hutofautiana kutokana na kiwango cha kiroho cha kila mtu.

Wengine wana viwango vikubwa, na wengine wana viwango vidogo.

Wengine wana macho ya rohoni ambayo ni hafifu, kwahiyo kiwango chake cha kuona ni kidogo,wengine wana macho makali;kiwango chake cha kuona ni kikubwa.

Ndoto ni mojawapo ya macho ya rohoni kwa kila mtu aotaye.

Ni vizuri kila mtu aote ili ajue ni kitu gani kinaendelea katika ulimwengu wa roho kwa habari ya mambo yake.

Mtu asiye ota ndoto ni mfu. Amekufa kwasababu hana alijualo katika ulimwengu wa roho;ambao huu ndio ulimwengu halisi. Kila kitu huanzia huko kisha huja mwilini.

Mtu asiyeota ndoto ni mfu kwasababu amekufa kiroho. Hajafa mwili,ila mambo yake mengi yamekufa, au ni kipofu kwasababu mambo yake mengi anayoonyeshwa na Mungu hayaoni na kuyajua, hivyo hajishughulishi nayo kuyajua.

Mungu anakuonyesha hapa mwanangu kuna shida,hapa umefungwa, huyo si mume sahihi,au si mke sahihi,hiyo nyumba usiingie, hicho chakula usile, hiyo nguo usiivae au usiinunue. Hiyo kazi itakuponyoka, mifugo yako inakufa kwasababu hizi na zile.

Lakini wapi! Mtu wa Mungu yuko busy kutukana watu,yuko busy na sayansi. Yuko busy na,God this,God that. Mtu wa Mungu yuko busy kumjua zeus. Yuko busy kuwatukana waombaji. Mungu naye anaamua kunyamaza juu yake. Shetani anapata sababu ya kumpa mapigo;si umemkataa Mungu bwana.

GO TO HELL na makufuru yako.

Sasa kama ndoto ni njia mojawapo ya kuongea na Mungu, kuna maono,mafunuo, sauti, ishara za waziwazi, mafumbo (Zaburi 92:5).

Lakini hapa tuzungumzie ndoto maana yote hayo juu yanaweza kujifunua katika ndoto.

Ndoto ni kiwango kidogo cha imani na njia rahisi ya mtu kuongea na Mungu;ndio maana hata watoto wetu wadogo wakiamka asubuhi wanakwambia baba au mama nimeota ndoto.

Hii ni ahadi ya Mungu kwetu kwamba nyakati za mwisho Mungu atamwaga roho yake juu ya watu wote na wataota ndoto na kuona maono.

Yoeli.2:28-29.
Hata itakuwa,baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili;na wana wenu,waume kwa wake,watatabiri,wazee wenu wataota ndoto ,na vijana wenu wataona maono;

29.tena juu ya watumishi wenu,wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

Kwahiyo hii ni ahadi ya Mungu kwetu, haijalishi wewe ni mdhambi au msafi,Mungu hataacha kuongea na wewe,shida inakuja unajishughulisha kwa kiwango gani ili ujue ni nini Mungu amekusemesha?!

Kwanini usikumbuke ndoto zako?

Kwanini usiwe unaota ndoto,Yaani huoti kabisa?

Kwanini unaota ndoto usizozielewa?

Kwanini unaota ndoto za kutisha?

Kwanini ukiota ndoto usiku unazikumbuka ila ukishtuka tu usingizini na zenyewe zinapotea?

KUNA AINA NGAPI ZA NDOTO?

Zipo aina tatu za ndoto, ambazo ni Kama ifuatavyo:-

1.NDOTO KUTOKA KWA MUNGU.

2.NDOTO KUTOKA KWA SHETANI.

3.NDOTO ZINAZOTOKANA NA SHUGHULI NYINGI ZA KUTWA.

Hapa makinika na ndoto namba moja na namba mbili kwasababu hizi zinaendana kwa ukaribu sana.

Kwanini ninasema zinaendana kwa ukaribu sana?

Ni kwasababu ndoto za Mungu huwa zinazungumzia habari za pande zote,habari za nuruni na za gizani.Mungu anaweza kukufunulia mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa giza wakati wewe ukiwa upo nuruni.

Nuru na giza havichangamani.Lakini Mungu anaweza kukuonyesha ya gizani ili uyafanyie kazi nuruni. Kuyajua ya gizani siyo dhambi ila ni dhambi kama utaamua kuyafuata na kuyatenda kama mtu aliyeko gizani.

Shetani anaweza kukupa ndoto kwa kujifanya ni malaika wa Nuruni,usipokuwa makini unajikuta unamfuata na kuharibu kiroho chako au mambo yako maana yeye hana nia njema hata kidogo kwa mwanadamu.

Ndipo hapa tunasema tunatakiwa kuwa rohoni muda wote ili tujue ni nini maadui zetu wanapanga juu yetu.Mungu hana upendeleo akikuletea ndoto zika
kuta mazingira mabovu ya kiroho chako,zitapotea na utabaki unalalamika kuhusu Mungu na kusema Biblia kwamba ni kitabu chenye makosa na mapungufu.

Biblia haina makosa wala mapungufu. Mwenye mapungufu ni yeye yule asomaye Biblia na kuitafsiri kwa macho ya upungufu wake.

Kila neno katika Biblia limehakikiwa na linafaa kwa mafundisho ilimradi uwe na ujazo wa Roho Mtakatifu. Hakuna kitabu chenye ubora uliohakikiwa kama Biblia.

Ndio maana kwenye maagano ya utajiri wa kichawi kuna viapo vya watu ambao hawatakiwi kuigusa wala kuisoma Biblia, kuna watu wenye nguvu za giza hawatakiwi kukisoma wala kukifunua hiki kitabu kiitwacho Biblia.

"Huwa wanakiita kitabu cha mjanja wa msalabani "

Hawathubutu hata kusema ni Biblia inayomzungumzia Yesu Kristo.

Huu ni ukweli mchungu. Ni habari njema kwa watu wote,siyo kwa ajili ya Wakristo tu,hapana ni habari njema za ufalme wa Mungu kwa mataifa yote hapa ulimwenguni.

Sasa unaweza kuota ndoto na usijue tafsiri yake,ila kwa kusoma maandiko katika Biblia ndio unaipata tafsiri ya ndoto yako.

Unaweza usijue wala kupata tafsiri kutoka katika maandiko lakini ukaipata kwa watumishi wa Mungu wasomao Biblia maana wao wana maarifa zaidi yetu sisi kutokana na ukomavu wao wa kiroho.

Wako zaidi yetu sisi kutokana na uwezo wao wa kupambanua roho na kuzitafsiri sauti,kuzijua nyakati na majira, uzoefu wa hizo ndoto,uwezo wa kuisikia sauti ya Mungu na kuijua.

Uwezo wa kuongea na Roho Mtakatifu katika kuyafumbua na kuyajua mafumbo ya Mungu wetu.

Wao wana karama hiyo.Hivyo usiote ndoto ukawa huielewi halafu ukakaa nayo mwenyewe usijue ufanye nini.Chukua hatua na umfuate mtumishi wa Mungu aliye hai akupe tafsiri yake.

UTAJUAJE HII NI NDOTO YA MUNGU?

Kwanza,huja mara mbili. Au zaidi ya mara moja, inakuja kwa njia ngumu,Mungu akiona hujaielewa anaileta tena mara ya pili ili upate kuilewa katika njia rahisi zaidi ya mwanzo.

AYUBU 33:14

Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,Naam,hata mara ya pili ,ajapokuwa mtu hajali.

Umeona hapo mtoto wa Mungu, Mungu anaweza kusema na wewe katika ndoto kwamba katika hiyo safari unayoipanga usiende maana kuna hajali imetegwa juu yako.

Ila unakaidi kuisikiliza hiyo ndoto yako,unaenda yanakupata ya kukupata halafu unakimbilia kumlaumu Mungu kwanini hakuizuia hiyo ajali isikupate.

Mstari unaofuata wa 15.
Katika ndoto ,katika maono ya usiku, usingizi mzito uwajiliapo watu,katika usingizi kitandani.

16.Ndipo huyafunua masikio ya watu,Na kuyatia muhuri mafundisho yao.

17.Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,Na kumfichia mtu kiburi;

18.Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.

Hapa utakuta kamtu kanauliza. Chacha chimoni ndio wapi hukwoo ?

Usifikiri ni shimo la udongo au mgodini. Ukiota ndoto za kuzama shimoni ujue hilo ni KABURI,mauti inakutafuta kwa udi na uvumba. Na ukifa utaenda shimoni ambako ni kuzimu maana umekufa katika njia isiyo ya haki, mbinguni huendi.

Mungu akikufunulia jambo,liwe la heri au shari anakuwa anajua unao uwezo wa kulizuia lisitokee katika njia ya maombi au kujiepusha kwa njia ya kutokwenda katika mafungamano ya hao watu, au kitu unachotaka kukifanya.

Kama ni kitu kizuri basi utakiombea na kukingoja ili kiweze kutokea, hata kama kitachelewa wewe kingoje tu kitatokea, usikate tamaa ili shetani asije akakiiba ama akakizuia.

HABAKUKI 2:1:3
Mimi nitasimama katika zamu yangu,nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.

2.BWANA,akanijibu, akasema, Iandike njozi (ndoto) ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili asomaye apate kuisoma kama maji.

3.Maana njozi hii bado ni kwa wakati uliamriwa inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake,wala haitasema uongo ;ijapokawia, ingojee;kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Je, mtoto wa Mungu huwa unaandika ndoto zako kwa ajili ya kumbukumbu au unaziacha zipotee tu halafu jambo likitokea unasema limetokea pasipo sababu?

Au huwa ukiota ndoto nzuri isipotokea unajikatia tamaa na kusema haikuwa ndoto kutoka kwa Mungu?

Tazama hapa mstari wa 4.
Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake;Lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.

Imani katika ulimwengu wa roho ndio msingi mkuu wa kumjua Mungu na kujua kusudio lake kwako . Usife moyo,usikate tamaa, mambo yote anayokuonyesha Mungu yatatokea kama ilivyopangwa na Yeye.

AYUBU 4:12-13
Basi,nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake.

13.Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.

Kwahiyo ndoto ni mawasiliano ya Mungu na mtu kumwambia habari za ndani za maisha yake ,mambo ya sirini kiasi kwamba huwezi kumwambia mtu yeyote ukishayajua.

Au kwa habari ya nchi, kiongozi wa nchi, viongozi wa dini,wa kiasiasa, waume na wake zetu,watoto wetu n.k.

Mungu akiona huelewi anamfunulia mtumishi wake ili aweze kukuletea ujumbe wako.Kazi kwako uukubali au umfukuze tena kwa kipigo na matusi juu. Haijalishi ilimradi umeshapewa ujumbe wako. Umnenee vibaya hilo halimhusu linabaki kuwa tanzi juu yako.

Wengine mnasumbuliwa na laana ya kuwasema vibaya watumishi wa Mungu, nyinyi kila siku ni maneno tu ya kashifa na kejeli. Mnajifungia malango ya baraka kwasababu ya upuuzi wa maneno yenu.

HESABU 12:1-15.

Hapo utasoma mwenyewe maana ni kisa cha Haruni na Miriamu,wakimsema Musa kwamba ameoa mke asiye Mwebrania bali Mkushi. Na kwamba yeye tu ndiye huongea na BWANA na siyo wao?

Roho ya mawifi hiyo. Maana Miriamu alikuwa dada yake na Musa na Haruni katika nyumba ya Walawi. Ukoo wao wanatokea kwa mtoto wa Yakobo aliyekuwa anaitwa Lawi.

Mungu akawasikia na kuwakasirikia, akasema Yeye anaongea na nabii kwa njia ya ndoto na maono,ila kwa Musa ni tofauti maana Nitasema naye wazi wazi wala si kwa mafumbo ,na umbo la BWANA ataliona.

Miriamu alipewa adhabu ya ukoma kwa siku 7 na Musa alimuombea msamaha baada ya siku 7 ukaisha.

Mungu anaongea na mtu katika ndoto wakati huo mtu labda yuko katika hali ya kusitasita kufanya maamuzi, ana mashaka moyoni mwake.

MATHAYO MT.1:19-25
Naye Yusufu, mumewe,kwa vile alivyokuwa mtu wa haki,asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

20.Basi alipokuwa akifikiri hayo,tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

21.Naye atazaa mwana,nawe utamwita jina lake Yesu,maana,yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

22.Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema.

23.Tazama,bikira atachukua mimba,
Naye atazaa mwana;
Nao watamwita jina lake
Imanueli;
Yaani,Mungu pamoja nasi.

24.Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza;akamchukua mkewe;

25.asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe;akamwita jina lake YESU.

Ngoja niwapunguzie maswali ya kuanzisha nyuzi sababu ya kutokujua tafsiri sahihi.Maana hapa utakuta mtu anasema kama alikuwa mkewe ilikuwaje asimjue tena wakati ameshaambiwa amchukue?

Uzi ukija wanatokea wenzake kucomment, we noma mkuu,umemaliza kila kitu,story za kutunga hizo,wanapongezana eti nao ni magreat thinkers kwenye mambo ya kiroho

Kutokumjua ni kutokufanya naye tendo la ndoa maana Bikira Mariamu alikuwa ametakaswa na kutakasika kwasababu kilicho tumboni ni kitakatifu.

Hata nyinyi wanaume ambao mnaihitaji kuwa na watoto yaombeeni matumbo ya wake zenu,myatakase ili zikitungwa mimba ziwe ni mimba kweli na siyo zenye mafungamano na mapepo. Pia utaambiwa katika ndoto mkeo asile vyakula vya namna gani ili asije akamtia najisi mtoto kwasababu hujui amebeba mimba ya mtoto mwenye kusudio gani kwa Mungu.

LUKA MT.1:11-15
Akatokewa na malaika wa Bwana,amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. 12.Zakaria alipomuona akafadhaika, hofu ikamwingia.

13.Lakini yule malaika akamwambia,Usiogope, Zakaria,maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabethi atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamuita Yohana.

14.Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.

15.Kwasababu atakuwa mkuu mbele za Bwana;hatakunywa divai wala kileo;naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.

Huyu alikuwa ni Eliya aliyerudi tena mara ya pili duniani,baada ya kuzaliwa akaitwa Yohana. Alipoanzisha huduma ya kuhubiri Injili akaitwa Yohana Mbatizaji kwasababu alikuwa anabatiza watu katika toba ya kweli,na ndiye aliyembatiza Yesu.

SOMA.mstari wa 17.
Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya,na nguvu zake ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto ,na kuwatilia waasi akili za wenye haki,na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.

Wanangu na yale maswali yao watauliza sasa kwanini hakuja mzima mzima kama alikuwa mbinguni na badala yake azaliwe tena upya kama mtoto mchanga?(Ila leo mnanichekesha sana aisee ).

Ni hivi, hii miili tuliyonayo duniani siyo tutakayoingia nayo mbinguni. Mbinguni kila kitu ni kitakatifu hivyo hii miili yetu ya duniani inaitwa miili ya uharibifu haiwezi kuingia katika ufalme wa Mungu kwasababu ina ukomo wa kuishi.

Ila hii mingine haina ukomo,haina magonjwa, haichoki.

Kwahiyo hata kama mtu akipaishwa kwenda mbinguni lazima avuliwe mwili huu,halafu avishwe mwili mwingine. Ndio maan Yesu baada ya kufufuka alikataa wanafunzi wake wasimguse maana alikuwa ameshatakasika kwa kuvishwa mwili mpya.

Hata siku hiyo ya hukumu watu watakwenda Jehanamu na miili mipya ambayo ikiungua haiishi wala kuteketea moto,lakini maumivu unayasikia vile vile kama jinsi uunguavyo na moto ukiwa hapa duniani.

Ukitaka kujua hiki kitu ninachokiongea muombe Roho Mtakatifu akuonyeshe Jehanamu kulivyo,yaani kule hata sakafu yake ni moto mkali, vitasa vya milango ni moto mkali,ukiwa mbali nayo unaanza kusikia joto utadhani ni volcano inataka kulipuka. Aisee tuombeane uzima,kule si mahali pa kwenda.

Mimi ninaongea vitu ninavyovijua, nilivyoviona na kuonyeshwa, nilivyoambiwa, na nilivyoagizwa niviseme. Sisemi kwa kumfurahisha mtu au kuifurahisha nafsi yangu,sisemi kwasababu ninajifanya ninajua.

Ninasema ili kuiokoa nafsi iliyopotea na kumuasi Mungu.

Mtu asijiulize mbona yeye siyo mwanachama wa M23 au vikosi vingine. Uasi katika Biblia ni kumtenda Mungu dhambi. Ukitenda dhambi umeasi maana umekwenda kinyume na maagizo ya Mungu wako aliyekuumba kwa sura yake na kwa mfano wake.(Wanangu wa maswali leo nina furaha sana,popote mlipo kunyweni soda kwa ajili yangu ili mnipoze koo kwa kucheka na maswali yenu,).

WAEFESO 5:6
Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana;kwa kuwa kwasababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.

MTU AFANYEJE IKIWA ANAOTA NDOTO LAKINI ANAZISAHAU,AU HAOTI KABISA.

1.Ombea kichwa chako kwa kukiwekea mikono kwamba unakifungua katika malango ya ndoto ili kila ukiota uwe unazikumbuka ndoto zako katika Jina la Yesu Kristo aliye hai.

2.Fungua anga la mahali ulipo au unapoishi maana unakuta kuna wakuu wa anga wa falme za giza wametanda kwa kuzuia maombi yako ili usijibiwe katika maono ya ndoto au sauti za malaika wa Mungu, na Mungu mwenyewe.

Washushe wote hao wafalme wa anga na weka utawala wa Bwana Yesu mahali unapoishi.

3.Ombea ardhi yako mahali unapoishi kuanzia kiwanja cha hiyo sehemu mpaka ulivyojenga nyumba yako(kwa mtu aliyejenga nyumba yake),Kama umepanga achilia damu ya Yesu uiamuru ikufungulie mlango wa ndoto kwa kuondoa vizuizi vyote vilivyowekwa na miungu ya ardhini au madhabahu za miungu ya kipepo iliyopo mahali hapo.

Usjihangaishe kuvunja madhabahu za watu usije ukapata vita na kuanza kupigana vita isiyokuhusu. Wewe sema ninajitenga na hizi madhabahu za mahali hapa na maagano yao hayanihusu, cha msingi ninataka ndoto zangu zije kama ilivyokusudiwa.

Ila kama zikikuchokoza na Mungu akasema zipige,sambaratisha maana tayari una kibali chote cha Mungu,naye atakusaidia. Utashangaa mwenye nyumba anaanza kukunuia. Isikupe shida wewe jua umeshamshinda.

4.Hii ni ya muhimu sana,kitanda chako.Mmeona watu wa Mungu kwamba kitanda ndipo mtu anapolala ili apate ndoto,ombea sana kitanda chako ili kikupe ndoto zilizo sahihi.

Kitanda kwenye ndoto au kiroho kina maana kubwa sana,ukikiota kwa namna mbaya usipuuzie hii ndoto,huwa kinaamanisha unyumba, ndoa, mke, uchumba na usaliti. Usipuuze!!

Ndio maana Biblia inasema ndoa iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi.

Malazi yawe safi,malazi ni kitanda, tafsiri nyingine ni mke bro.

Halafu yale mambo ya lenzi mbinuko hivi mlifundishwaga na nani? Yameruhusiwa kweli? Kama kitanda ni sawa na mke, Je unaweza kukikunja kitanda na kukibinua binua kweli!? Au popo sijui kavuka mto?( Hii iwe kiporo).

NGOJA niwaulize swali wanaume wenzangu.!!!

Hivi ni mara ngapi wake zetu huwa wanatuuliza au wanatuambia wameota ndoto tuna wanawake wengine huko nje, na tunakataa?

Au huwa wanasema wameota ndoto tunataka kwenda kusaliti na mwanamke fulani, au binti fulani mwembamba hivi, mweupe, mweusi ana mwanya hivi. Tunajibaraguza mimi hapa mke wangu, unatoa macho huku ukijipigapiga kifuani, siwezi mimi hayo mambo ya kijinga!!!!

Ila huko rohoni unasema,sasa hii noma ina maana amejua, amejuaje? Huyu kama siyo mwanga ameweka mtego. Kumbe ni ndoto ujue.

Au mara ngapi huwa wanatuambia wameota tuna watoto nje, wa kike na wa kiume? Unasema hii sasa balaa! Unaishia kusema mke wangu unawaza mambo yako huko hadi unayaota usiku, mimi sina, unaikana damu yako!!

Hapa mimi ninaongea na wanaume wenzangu ambao wanazijua fouls zetu (faulo),mimi siyo malaika mjue, kama Mungu alinifundisha haya masomo mjue ninajua maisha tunayoyapitia.

Ndio maana ametupa kibali cha kuoa wake zaidi ya mmoja na hao watoto watambulishwe kwenye familia.

NGOJA niwape mbinu kwenye cheti cha ndoa kuna sehemu imeandikwa wake wengi au mmoja? Wewe kama unahitaji kuoa zaidi ya mke mmoja kinachokufanya uweke tiki kwa mmoja ni nini?

Na kwanini usimwambie mkeo kwamba utaoa mke mwingine ili awe anajua kuliko kumfanyia mshtuko wa moyo? Maana utajifunga kwa machaguzi yako.

Kanisa halitaki kukufungisha ndoa, kuna ndoa za mila, serikali. Kafunge kama unahitaji cheti kuliko kuzaa watoto na kuwatelekeza huko mtaani na kuwa mzigo kwa serikali.

Kama shetani atataka kukufunga kwa hiyo ndoa, mwambie ni maagizo ya mtumishi wa Mungu 7seven aliyopewa na BWANA maana dhambi ni ile unayoificha ila ukiiungama na kuitubia na kuiweka hadharani haiwi dhambi tena maana hatia inaondoka moyoni mwako.

Hata kula chakula pasipo imani ni dhambi maana unakula huku ukiwa na mashaka moyoni mwako sembuse iwe damu yako uliyoitelekeza inaishi kwa dhiki na shida huko mtaani na wewe unakula bata kwa kuogopa kusemwa na mkeo au ndugu zako?

Unamfanyia nani ibada ikiwa unaficha mambo ya kuja kuiangamiza nafsi yako?

Enyi wake watiini waume zenu ,na waume wapendeni wake zenu kama jinsi mnavyoipenda miili yenu maana mu mwili mmoja katika Kristo na watoto wenu ni damu yenu.Ikimlilia Mungu kilio chao anakisikia na unahesabiwa hukumu au hatia.

WAEFESO 5:22
Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

23.Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa;Naye ni Mwokozi wa mwili.

24.Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

25.Enyi waume wapendeni wake zenu,kama Kristo naye alivyolipenda kanisa,akajitoa kwa ajili yake.

28.Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

31.Kwasababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.

33.Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe;wala mke asikose kumstahi mumewe.

WAEFESO 6:1-3
Enyi watoto,watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.2.Waheshimu baba yako na mama yako ;amri hii ndiyo amri ya kwanza kwenye ahadi.

3.Upate heri,ukae siku nyingi katika dunia.

4.Nanyi, akina baba,msiwachokoze watoto wenu;bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

Hicho kifungu cha mwisho, ukiwatelekeza watoto umewachokoza kwasababu hawatapata matunzo na mapenzi ya baba,hawatalelewa katika msingi mzuri,kuna vitu watavikosa na vitakuwa shida huko mbeleni.

Watoto watakuwa na uchungu,hasira, watakosa upendo, huruma kwa wengine kwasababu walishaathirika kisaikolojia. Huku wewe ukisema unasali sana ili ubarikiwe katika mambo yako.

Hicho ni kifungo huwezi kufanikiwa sawa sawa mpaka hiyo dhambi uitubie hadharani, hii si dhambi ya uzinzi au wizi kusema utatubu na mambo yako yataendelea kuwa sawa.

Ukitubu kwa ajili ya dhambi ya uzinzi huku una watoto nje wanateseka na mama yao,ikiwa umesamehewa na hutaki kuwaleta hao watoto,unaonaje ukimuomba Mungu ili awarudishe viunoni mwako na usamehewe dhambi kabisa?

Inawezekana hii!? Hapana. Kwahiyo ni dhambi isiyofichika kama vile mwanamke mwenye mimba ya karibu kujifungua.

Hivi huyu mtoto akishakuwa mkubwa amefanikiwa utajitokeza bila aibu eti unahitaji msaada wake kweli?

Ninaongea na mtu anayepitia katika hali ya namna hii na anahitaji kutengeneza na familia yake. Kama haikuhusu usiseme ninafundisha uongo,subiri siku ikikufika utanikumbuka mahali utakapokuwa.

5.Ombea mito yako ya kulalia, mashuka na godoro. Vyote unavyovilalia viombee ili Mungu avitakase kwa damu ya Yesu ili visitumike kama kikwazo cha kukuzuilia ndoto zako.

6.Kama umeoa muombee mkeo, na mke amuombee mumewe maana unaweza kukuta pepo la kuzuia ndoto lipo kati ya mmojawapo linawaangalia na kuwafuatailia kujua mambo yenu ya kiroho. Likiona ndoto nzuri linazizuia kupitia katika mwili wa mmojawapo.

Mke na mume ni mwili mmoja, hivyo kuna mapigo yanawapata pamoja kwa mmoja wenu kufanya kosa.

7.Ombea nafsi yako,moyo wako na roho yako,kama kuna mambo yamepandwa na shetani yaondoke, ili kuwa na nafasi ya kupanda mambo ya Mungu. Au tunda la Roho wa Mungu.

Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana huko ndiko kutokako chemi chemi za uzima. "The Bible says".Huko ndiko mambo yote ya rohoni huanzia. Na Mungu anaongea nasi kupitia ndoto ambazo ziko katika ulimwengu wa roho.
..........................................................................
Leo nimeongea vitu vingi,nimeongea na kila kundi na kila rika, kwahiyo kila mmoja achague ambacho kitamfaa na Roho Mtakatifu atamsaidia kujua wapi amekwama na amnasue.

Maana hata wanangu, wa Mungu huyu na Mungu yule hata wao huwa wanaota ndoto ila wanaamini zinatoka kwa zeus, apollo, wengine waamini ni mawazo tu.Barida tunaenda sawa maana mnanisoma mnapata kitu hata kama siyo vyote.

Lakini yote kwa yote tunapeana elimu,na siwapingi kwa maswali yenu maana mnauliza kutaka kujua. Huwa ninawapitia pitia kidogo nipatapo muda,nanyi msiache kunisoma maana huwa ninaona mnapata wapi "concept ".

Ninawapenda sana watu wangu ,pamoja sana,mwaka wa 2024 uwe wenye heri nyingi sana kwenu,ninajua ipo siku mtakubali kuwa hakika Mungu yupo, tuombeane uzima.kama vile mimi ninavyowaombea nyinyi ili mbadilike, hasa nyie msiye hoji kwa maksudi tofauti na wale wanaotaka kupotosha. Sir God anawapenda sana maana anawaita watoto wake.
............................................................................

Siku mkiwa mnaombea watu au mtu akalipuka mapepo na kusema nani ameawaagiza haya myafanye na kwa amri ipi,?

Msiogope semeni Yesu wa 7seven yule wa mtandaoni, yakiwauliza kwa mamlaka ipi aliyonayo, yaambieni aliyopewa kutoka mbinguni na Mungu wake ili ayahubiri haya.

Ujue shetani ananijua sana,mapepo yananijua sana.Yakisema mbona yeye ana mke mmoja. Yaambie sisi hayo hatuyajui ila tunachokijua ni maagizo yake kutoka kwa Mungu wake nendeni mkamuulize . Sisi tuna neno moja tu mwacheni mtu huyu awe huru msimfunge katika kosa la kuwa na wake wawili, maana hiyo sheria imebatilishwa kwa kizazi hiki cha kurudi kwa Yesu.

Ukiwa unakemea pepo usipate hofu,ukiingiwa na hofu imani yako inapotea na imani ikipotea nguvu za Mungu zinaondoka juu yako maana Mungu alisema tusiogope mara nyingi sana katika Biblia.

Nitawapa ushuhuda kidogo.

Kuna siku nilikuwa ninamuombea mke mdogo ,yaani huyo baba ana wake wawili. Pepo linakaniambia kwanini unamuombea mwanamke aliye na mume wa wake wawili?

Nikamuuliza huyo mume amefungwa na sheria gani maana yeye haamini katika Mungu wa huyo mke mdogo? Yakasema ni mpagani. Nikayauliza kwani mke mkubwa hajui?

Yakajibu anajua. Nikasema basi maana alimtaarifu, na huyu asiyeamini anaamini kwa mkewe huyu anayeamini. Yakatoka na akawa huru.

Mengine yalitaka kunirarua. Kisa huyo binti alienda kufanya kazi mahali nikaombwa nikamuombee. Aisee hiyo siku siyo kabisa, yalipiga kichagga cha ndani yananiuliza nani kakutuma huyu ni mtoto wetu.Yakasema sisi ni mizimu ya ukoo wake tumepewa sadaka ya damu na mbege.

Nyinyi watu wa mlima mrefu. Ninakuja ,mara hii kitaeleweka, iwe maagano ya kichuri(Mara),kisusio,damu ya mbuzi au ng'ombe, kondoo au kuku, mbege au viapo vya" MASALE". Wenzenu Wahaya wanaita VILAMULA kwa Bukoba, na Muleba wanaita "VIHANE"

Ni aina fulani ya miti huwekwa kwenye mipaka ya shamba au viwanja. Kwa lugha nyingine tuviite VIAMUZI. Hata kwenye Biblia imeandikwa usihamishe mpaka uliowekwa na wazee.

Sasa kwenye hizi jamii wanayatumia kama vilinda mipaka, vihamishe kichwa kichwa uje uone mziki wake,yaani yana maana katika viapo vya ulimwengu wa roho. Na vinatumiwa sana kufunga watu,ndio maana uchagani mtu akija nacho kukuomba msamaha kama mlikuwa na ugomvi lazima umsamehe! Mpo hapo?

Bahati nzuri kulikuwa na watu wakunisaidia maana ilibidi nimuombe Roho Mtakatifu anisaidie maarifa,akaniambia yarushie moto kwa mbali usigusane naye huyo binti.Naye akafunguliwa.

Sasa mtu anajiuliza mbona unasema uko Nyikani lakini unasema ulimuombea fulani na fulani?

UKO SAHIHI,ILA HUWEZI KUFUNDISHWA KUTUMIA SILAHA BILA KUZIFANYIA MAJARIBIO.

MUNGU AWABARIKI SANA.

HAPPY NEW YEAR,2024.

29.12.2024.
 
Message Sent and Delivered Successful , Kazi Kwetu Sasa
 
Sawa sawa kabisa watu wayafanyie kazi haya. Kiukweli hilo somo la leo limenifurahisha sana,katika siku ambazo nimewahi kufundisha sijawahi kufurahi hivyo kama hii siku.

Mungu amenipa kicheko. Kama jinsi mimi nilivyopewa kicheko cha imani na kimwili na nyinyi awape vicheko vya furaha kwa mwaka mzima wa 2024 katika Jina la Yesu Kristo aliye hai. Watu wa kiroho watanielewa.Amen.
 
Sawa sawa kabisa watu wayafanyie kazi haya. Kiukweli hilo somo la leo limenifurahisha sana,katika siku nimeanza kufundisha sijawahi kufurahi hivyo.

Mungu amenipa kicheko. Kama mimi nilivyopewa kicheko cha imani na kimwili na nyinyi awape vicheko vya furaha mwaka mzima wa 2024 katika Jina la Yesu Kristo aliye hai. Watu wa kiroho watanielewa.Amen.

, Amina
 
Asante sana 7seven, ubarikiwe sana, naomba kujua kuhusu hili somo la kufunga
Nimekumbuka somo la mfungo nitakuwa nimeshalifundisha, kuna siku niliongelea mfungo wa matunda kwa siku saba. Sijui kama ulishalipitia. Ila ingekuwa vizuri kama utakuwa una kipengele ambacho unaona kinahitaji kuelezewa vizuri ukakiainisha hapa, maana nalo ni pana sana.Ahsante.
 
Naomba somo hili mtumishi km hutojali somo la mfungo wa matunda nianze nalo mwaka
 
Nilishalifundisha liko kule juu jaribu kusearch, au kama kuna mtu analo karibu alirushe hapa maana nilipokea shuhuda nyingi za watu kufunguliwa kupitia somo hilo.

Actually halikuwa somo per see, bali nilitoa maelekezo kidogo lakini yanayoeleweka.
Hilo limenipita kurudi juu inabidi kutulia sana
 
SANA maana liko mbali,hata mimi nimejaribu kulifuatilia nikaona sitafika mapema. Ila kwa ufupi nilikuwa nimesema hivi;unaweza kufunga kwa kula matunda tu lakini yasiyokuwa na gesi kwa muda wa siku 7 ili kuua nguvu za giza zilizoko mwilini mwako ambazo zilipitia katika vyakula hasa vyenye damu.

Damu ina uhai. Kwahiyo maadui wanatumia sana hivi vyakula kupitisha roho za nguvu za giza kuharibu kiroho chako.

Sasa unapokula chakula cha matunda na uko katika maombi unakuwa unaua nguvu za asili za giza ambazo ziko ndani yako.Unapata nguvu za Mungu maana unakuwa umetoa sumu zote mwilini na kuua uchawi uliolishwa kupitia vyakula.

Unaweza kuwa unakunywa maji yenye uvugu vugu ili yakupe nguvu za kufanya kazi. Kuna watu ambao hawakuzimaliza hizo siku 7 lakini majibu yake waliyapata.

Utajua pale unapokwenda toilet. Kuna mambo yanatoka mpaka unashangaa tumbo lako lilikuwa na nini. Mfungo wa matunda ni mzuri mno kwa kila mtu maana haijalishi uko nuruni au neutral. Ikiwa wewe ni mwanadamu nature haiwezi kukuacha.

Hata kwa mtu mwenye magonjwa mfungo wa matunda una nguvu sana.Siku ukiota ndoto za matunda ujue hayo ni mafanikio. Yakiwa yameoza ujue na mafanikio yako yameoza/yameozeshwa maksudi ili usiyafaidi.

Ndio maana mtu husema ninakula matunda ya kazi yangu. Upo hapo!?

Chukua hatua mkuu,utanipa mrejesho. Unaweza ukafunga wewe ukashangaa majibu yamejibiwa kwa shemeji au watoto.
 
Shslom shalom! Je ni matunda gani yasiokuwa na gesi mtumishi?
 
Shalom! Matunda hutofautiana kati ya mtu na mtu,ila embe, parachichi, ndizi mbivu,mapapai, matikiti maji,korosho na karanga ni nzuri sana kwenye mfungo. Usile nanasi maana huwa linafanya "digestion" kwa haraka sana na linaweza kukusabishia gesi tumboni japo lina sukari ya kukupa nguvu mwilini. (DIGESTION,MMENG'ENYO WA CHAKULA TUMBONI).

Machungwa na machenza hapana,usile yana gesi.

Asali nayo ni nzuri, miwa ni mizuri haina gesi,hapa zingatia vyakula visivyo na jamii ya damu damu,na visivyopikwa. Isipokuwa karanga na korosho unaweza kula havina shida.

Maji ya vugu vugu unaweza kutumia asali badala ya sukari ya kiwandani na majani ya chai ili usipate kichefuchefu,na mwili uwe na nguvu ya kutosha.(Jitahidi iwe siku 7 utaona mwenyewe).Hii itakusaidia kunywa maji mengi zaidi kwa mtu ambaye hajazoea.

Ila kwa mzoefu wa kufunga,hii si kitu kabisa kwake. Mafungo yaendane na kiwango cha mtu cha imani yake,mtu akiweza kufunga siku moja sawa,mbili sawa,tatu na kuendelea ni sawa maana Mungu atamhesabia haki kwa kuwa anazo nguvu kidogo, na hatutakiwi kuwacheka wale wasioweza kufunga bali tuwaombee na kuwatia nguvu ili nao waweze kufunga kama sisi.Amen.
 
7seven shalom mtumishi...
Tarehe 1 ndo hiyo inakuja...twaomba utuongoze kwa neno na maombi ya kufunga na kufungua mwaka mpya 2024
Sawa,naona watu wameguswa na mfungo ,nipeni muda kidogo niandae somo halafu nitalileta hapa kadri Roho Mtakatifu atakavyoniongoza.

Jinsi ya mtu kufunga,afunge siku ngapi, anatakiwa aombeje, kwanini mtu afunge, afungue saa ngapi. Yote haya nitayaelezea kadri nitakavyoongozwa.
 
Shalom! Matunda hutofautiana kati ya mtu na mtu,ila embe, parachichi, ndizi mbivu,mapapai, matikiti maji,korosho na karanga ni nzuri sana kwenye mfungo. Usile nanasi maana huwa linafanya "digestion" kwa haraka sana na linaweza kukusabishia gesi tumboni japo lina sukari ya kukupa nguvu mwilini. (DIGESTION,MMENG'ENYO WA CHAKULA TUMBONI).

Machungwa na machenza hapana,usile yana gesi.

Asali nayo ni nzuri, miwa ni mizuri haina gesi,hapa zingatia vyakula visivyo na jamii ya damu damu,na visivyopikwa. Isipokuwa karanga na korosho unaweza kula havina shida.

Maji ya vugu vugu unaweza kutumia asali badala ya sukari ya kiwandani na majani ya chai ili usipate kichefuchefu,na mwili uwe na nguvu ya kutosha.(Jitahidi iwe siku 7 utaona mwenyewe).Hii itakusaidia kunywa maji mengi zaidi kwa mtu ambaye hajazoea.

Ila kwa mzoefu wa kufunga,hii si kitu kabisa kwake. Mafungo yaendane na kiwango cha mtu cha imani yake,mtu akiweza kufunga siku moja sawa,mbili sawa,tatu na kuendelea ni sawa maana Mungu atamhesabia haki kwa kuwa anazo nguvu kidogo, na hatutakiwi kuwacheka wale wasioweza kufunga bali tuwaombee na kuwatia nguvu ili nao waweze kufunga kama sisi.Amen.
Haya matunda na maji unayala na kunywa baada ya muda gani
Mfano nimeanza kufunga asubuhi nifungulie saa ngapi kwa kula hayo matundq
 
Back
Top Bottom