Jifunze kusali japo hata sala ya asubuhi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,572
44,801
Hakuna sala rasmi ya Asubuhi iliyotungwa kwamba watu wafuate mfumo wake lakini ni wajibu wa kila mtu anayeitwa mkristo kusali..Katika kusali au kuomba kuna vitu vikuu vitatu vya kuzingatia katika sala yoyote ile.. Cha kwanza ni Shukrani, cha pili ni kupeleka mahitaji na cha tatu ni kutangaza.

Katika sala ya Asubuni pia ni muhimu kuzingatia hivyo vipengele vitatu. sala hii hapa chini kwa Asubuhi inaweza kukufaa.

Unapoamka kabla ya kufanya kitu chochote kile, hata kabla ya kwenda kupiga mswaki.. Sali sala hii kwa kumaanisha na kwa muda mrefu kwa jinsi uwezavyo ukitaja hata mambo ambao hayajaandikwa katika sala hii.

Sema…

Ee Baba yangu, Mungu muumba wa mbingu na nchi, nakushukuru kwa kuniamsha nikiwa mzima wa afya,(hata kama umeamka na udhaifu fulani mdogo huna buni kumshukuru Mungu pia)

Nasema ahsante sana ni kwa Neema zako tu, wapo ambao hawajaweza kuamka leo lakini mimi nimeamka.

Nakuomba unipe Neema yako katika siku ya leo inayoanza nikatembee katika mapenzi yako, nisikutende dhambi wala nisikuhuzunishe kwa jambo lolote, naomba ukaniepushe na majaribu yote, na mipango yote mibaya ya yule Adui aliyoipanga juu yangu na juu ya watu wangu na vitu vyangu na afya yangu na shughuli zangu katika hii siku ya leo.

Nijalie pia siku hii ya leo angalau niongeze kitu kimoja katika ufalme wako, hata itakapofika tena jioni nikapate kushuhudia matendo yako makuu na kukushukuru. Naomba haya machache katika Jina la Yesu Kristo.

Amen’.

Kumbuka pia tuna wajibu wa kusali muda wote na mahali popote sio tu asubuhi, au jioni…hapana bali hata tukiwa tunatembea, tunafanya kazi..tuna wajibu wa kusali

Bwana akubariki.
 
Sala yoyote ina mambo matatu muhimu sana.
1. Kushukuru, hata kwa kidogo ulichojaaliwa.
2. Kusifu au kuuabudu ukuu wa Mungu
3. Kuomba toba kwa dhambi ulizozitenda.

Mahitaji yako usiyape kipaumbele sana kwani Mungu anayajua
 
Kiwango cha Umasikini wa fikra na Imani.

ni...
...ukosefu wa udadisi wa kiakili, mawazo, na uhusiano wa kiroho

...there is no one right way to pray. Usihadae.
 
Hakuna sala rasmi ya Asubuhi iliyotungwa kwamba watu wafuate mfumo wake lakini ni wajibu wa kila mtu anayeitwa mkristo kusali..Katika kusali au kuomba kuna vitu vikuu vitatu vya kuzingatia katika sala yoyote ile.. Cha kwanza ni Shukrani, cha pili ni kupeleka mahitaji na cha tatu ni kutangaza.

Katika sala ya Asubuni pia ni muhimu kuzingatia hivyo vipengele vitatu. sala hii hapa chini kwa Asubuhi inaweza kukufaa.

Unapoamka kabla ya kufanya kitu chochote kile, hata kabla ya kwenda kupiga mswaki.. Sali sala hii kwa kumaanisha na kwa muda mrefu kwa jinsi uwezavyo ukitaja hata mambo ambao hayajaandikwa katika sala hii.

Sema…

Ee Baba yangu, Mungu muumba wa mbingu na nchi, nakushukuru kwa kuniamsha nikiwa mzima wa afya,(hata kama umeamka na udhaifu fulani mdogo huna buni kumshukuru Mungu pia)

Nasema ahsante sana ni kwa Neema zako tu, wapo ambao hawajaweza kuamka leo lakini mimi nimeamka.

Nakuomba unipe Neema yako katika siku ya leo inayoanza nikatembee katika mapenzi yako, nisikutende dhambi wala nisikuhuzunishe kwa jambo lolote, naomba ukaniepushe na majaribu yote, na mipango yote mibaya ya yule Adui aliyoipanga juu yangu na juu ya watu wangu na vitu vyangu na afya yangu na shughuli zangu katika hii siku ya leo.

Nijalie pia siku hii ya leo angalau niongeze kitu kimoja katika ufalme wako, hata itakapofika tena jioni nikapate kushuhudia matendo yako makuu na kukushukuru. Naomba haya machache katika Jina la Yesu Kristo.

Amen’.

Kumbuka pia tuna wajibu wa kusali muda wote na mahali popote sio tu asubuhi, au jioni…hapana bali hata tukiwa tunatembea, tunafanya kazi..tuna wajibu wa kusali

Bwana akubariki.
Amina mtumishi. Ubarikiwe na Bwana Yesu. AMEN.
 
Back
Top Bottom