Jibaba la Miaka 31 Linalovaa Nepi za Watoto..

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
6323842.jpg

Stanley Thornton, Jibaba la Miaka 31 likiwa kwenye meza ya watoto akilishwa chakula
Friday, March 23, 2012 12:43 PM
Duniani kuna mambo, mwanaume mmoja wa nchini Marekani mwenye umri wa miaka 31 kwa miaka 18 iliyopita amekuwa akiishi kama mtoto mchanga akivaa nepi, kunyonya vidole na kucheza michezo yote ya watoto wa miaka miwili.
Akiwa na umri wa miaka 31, Stanley Thornton ana umbile kubwa sana akiwa na uzito wa kilo 133 na urefu wa mita 1.67.

Pamoja na umbile lake kubwa, Stanley amekuwa akiishi kama mtoto wa miaka miwili kwa miaka zaidi ya 18 iliyopita.

Stanley amekuwa akivaa nepi za watoto zilizoshoneshwa maalumu kwaajili yake, amekuwa akinyonya vidole na akivaa nguo za watoto na pia akilala kwenye kitanda kama cha watoto akibembelezwa na nyimbo za watoto huku akiwa amezungukwa na madoli kibao.

Mbali ya hayo, Stanley analishwa kama mtoto ambapo amekuwa akiwaajiri wanawake kuigiza kama mama yake wakimlisha chakula kwa kijiko.

Stanley hafanyi kazi na amekuwa akiishi kwa kutegemea pesa za kujikimu toka serikalini.

Stanley anasema kuwa anajihisi salama zaidi na anafurahia maisha yake hayo ya kufanya kila kitu kama mtoto wa miaka miwili.

Angalia VIDEO za Stanley chini.
Man Obsessed With Being a Baby - YouTube

Man 30 lives as an ' adult baby ' - YouTube
 
Back
Top Bottom