JF tunasemaje kuhusiana na msimamo huu wa serikali?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Serikali: Hatufuti adhabu ya kifo

na Datus Boniface


SERIKALI imesema haitafuta adhabu ya kifo kama nchi nyingine za Afrika zilivyofanya, hadi itakapopokea taarifa za wananchi kupinga adhabu hiyo.

Msimamo huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano unaohusu adhabu ya kifo.

Alibainisha kuwa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa pamoja na Rais Jakaya Kikwete hawajatoa adhabu ya kifo, hivyo bado kuna watu wenye kutaka ifutwe huku wengine wakitaka isifutwe.
 
Anaye ua mtu moja kwa makusudi ni sawa na ameua watu wote (Qurani Tukufu).

Hukumu yake: Anauliwa na yeye

Anayetetea muuaji ni muuaji na asubuiri siku wakimuua mwanaye au yeye mwenyewe bila sababu....

kama mnachukua hela za NGO msitupigie kelele za zenu hapa kuna mambo ya msingi kuyashughulikia kuliko kutetea "wauaji" wtf!
 
Huu ni msimamo mzuri kwa saa hivi, lakini nadhani hapo baadaye itabidi serikali ibadilishe huu mkondo. Hauwezi kuondoa death sentence bila ya kuwa na sheria madhubuti za kuwaadhibu watu wanaoua kwa makusudi; ili kuweza kufanya hivyo, Justice System nzima ya nchi lazima ibadilike kuhusu suala hili. Kwa mfano, itabidi watunge adhabu nyingine inayolingana na kosa hilo badala ya adhabu ya kifo. Pia, adhabu yenyewe inatakiwa iambatane na labda training ya aina yoyote ili kwamba mtu akitoka huko jela, aweze kuwa raia mwema na wakawaida.

Parole Officers na Social Workers inabidi waongezewe elimu, ili kukabiliana hali kama hii. Naamini kwamba Tanzania, especially the Justice System (Mahakama, Polisi & Prison) havijafikia kiwango hicho cha maendeleo katika kudeal na wahalifu wakubwa ambao ndio wengi wenye kuhukumiwa adhabu hii.
 
Back
Top Bottom