JF is my homeland

, aisee wizi upo hadi ngazi ya familia ??!! Inatisha jamani lol, inatisha jamani usipokuwepo hesabu unapigwa bao tu tena bila huruma wala aibu!! Hongera mkuu tangulia ngoja nikusanye kamtaji uzuri utaalamu na uzoefu wa nitakachoenda kukifanya ninao, acha niandae kiberiti na petrol ya kuchomea meli.

Hehehe balaa sana kaka watu ni waizi hadi hatari!!
 
pengine hizo biashara huwa na faida sana kiasi hata wakiibiwa kinachobaki kiakuwa si haba. ila kitu kingine nimejifunza ni kuwekeana malengo na mtu uliye muajiri na ajue kabisa kitakachompata asipofikisha malengo. hili liahitaji uwe umekaa kidogo kwenye biashara yako ili ujue jinsi ya kupangiana malengo na uliyemuajiri. kitu kingine ni documentations hiki muhimu sana. kitakupa mwanga jinsi mambo yanavyoenda. hata hivyo mkuu biashara nyingi tu kati ya hizo ulizotaja zinakufa kila leo hasa ya mabasi na nahisi sababu kubwa ni huu usimamizi wa remote control.

Nilipokuwa chuo mwalimu wangu wa Marketing aliuliza swali, je asilimia ngapi ya biashara mpya huwa zinakufa? wengine tukasema 50% wengine walidai 30% , wengine 70% lakini akatuambia kwamba zaidi ya 95% ya biashara mpya huwa zinakufa. Nilistuka sana!!
 
Hongera sana mkuu.Ujasiriamali ni mgumu hasa unapoanza kwanza unakutana na changamoto ya jamii inayokuzunguka kukuona umechanganyikiwa kwanini uache kazi ambayo ilikuwa na uhakika wa kipato kila mwisho wa mwezi.Na hili ndio linalopelekea kushusha hari ya vijana kupata udhubutu wa kufanyamambo makubwa mana kwa tafsiri finyu ya kitanzania ukiwashukuwa na degree wewe hurusiwi kufuga kuku kama shughuli yako rasmi, ni lazima uwe kwenye taasisi ndo utapata heshima.Lakini mi naamini hizi shughuli zauzalishaji zikifanywa kwa nguvu zote na vijana amabo wameenda shule kuna mwanga mkubwa sana huko mbeleni.Hongera sana
 
Mkuu Ngumakasi hata mimi nilikuwa mchunguliaji wa JF toka 2009 nikajiunga mwaka jana tu. Ukishaionja JF huwezi kuiacha! Heshima kubwa iende kwa waasisi na wachangiaji, hasa jukwaa hili ambalo limenibadili mtazamo na mwelekeo wangu! Mkuu Ngumakasi mimi bado nimenasa kwenye utando wa buibui ya ajira ya serikali. Huwezi kufanya ujasilia mali ukiwa kazini. Ni mara nyingi sana kila ninapojipanga na kuanzisha dili kubwa sana linalohitaji usimamizi wa karibu, ninapewa safari kikazi nakuwa nje wiki nzima au zaidi, nabaki naagizia kwa simu, nikirudi nakuta mkorogo tu kila kitu kimetibuka. Wakati mwingine maboss wakigundua unamiradi watakupa safari kila mara mwisho wa siku miradi inakushinda. Kinachotushinda tuliomakazini kufanikisha miradi kwa kasi yenye tija ni kutoweza kusimamia, na kwa hakika kwa jinsi nilivyoshuhudia watu wengi niliowahi kuwaomba wasaidie kusimamia walivyo wezi na waongo ninajiuliza hawa matajiri ambao wamesambaza miradi yao ambako wao hawako wanadhibiti vipi wizi, aisee wizi upo hadi ngazi ya familia ??!! Inatisha jamani lol, inatisha jamani usipokuwepo hesabu unapigwa bao tu tena bila huruma wala aibu!! Hongera mkuu tangulia ngoja nikusanye kamtaji uzuri utaalamu na uzoefu wa nitakachoenda kukifanya ninao, acha niandae kiberiti na petrol ya kuchomea meli.

Mkuu Kubota, binafsi hata mimi natoa heshima kubwa sana kwa waasisi wa na wachangiaji wa Jami FORUM. it's a forum of it's own kinn, yani madarasa kibao. na kweli ukiingia huku hutoki...lol big up sana. kweli kabisa ni tabu kweli kufanya yote mawili, ila perhaps ningekuwa nimeajiriwa na serikali yetu hii tukufu ninge manage. nasikia huko work load ni ndogo! sijui ni kweli? na ni kama vile hamjabanwa sana!! sijui pia kama ni kweli, na job security ipo ya kutosha as opposed to the private sector that i ve been working for ever since time memorial.

ninamfano mzuri wa jirani yangu mmoja amabe yeye nilifikiri amefanikiwa kwenye hili...yeye alikuwa vendor wa m-pesa, tigo pesa, dstv, luku,.you name them. wafanyakazi kila siku wanampigaje? ni shoti tu deile. baadae akaja akampata mtoto wa ndugu yake ambaye waliwekeana makubaliano tofauti kidogo. kwamba yule kijana atafanya kazi pale kwa uaminifu kwa miaka mitatu, atakuwa analipwa nusu tu ya mshahara wake wa mwezi. then baada ya miaka mitatu anamaliziwa the other 36 halves plus kumpeleka shule(yule kijana hakufanya vizuri form four finals). hivi tunavyoongea three years have lapsed na duka la jirani yangu lipo pazuri, na mtaji umekua, kijana hajawahi kuiba hata senti, hajawahi kupata the so called shoti not even once..na yupo shuleni amerudia form three. ila jirani yangu amerudi kwenye same challenge he was facing before, ya kupata mfanayakazi mwaminifu. labda hii inaweza kukusaidia mkuu.

Kila la heri.
 
Hongera sana mkuu.Ujasiriamali ni mgumu hasa unapoanza kwanza unakutana na changamoto ya jamii inayokuzunguka kukuona umechanganyikiwa kwanini uache kazi ambayo ilikuwa na uhakika wa kipato kila mwisho wa mwezi.Na hili ndio linalopelekea kushusha hari ya vijana kupata udhubutu wa kufanyamambo makubwa mana kwa tafsiri finyu ya kitanzania ukiwashukuwa na degree wewe hurusiwi kufuga kuku kama shughuli yako rasmi, ni lazima uwe kwenye taasisi ndo utapata heshima.Lakini mi naamini hizi shughuli zauzalishaji zikifanywa kwa nguvu zote na vijana amabo wameenda shule kuna mwanga mkubwa sana huko mbeleni.Hongera sana

Mkuu Dafo uko sahihi, sanasana pale unapopata changamoto ndio kabisa jamii inakulaumu. tatizo lipo kwenye systems zetu kiasi kwamba watu tumekariri mambo fulani tu kwamba ndiovyo maisha yanapaswa kuwa. ila pia siwalaumu-kwa jinsi serikali yetu isivyo jishuhulisha na wajasiriamali wadogowadogo au SMEs kwa ujumla, ni kwamba ukianguka unaeza a ngukia pua. yani ukianza hata buffer ujiwekee mwenyewe. kwahiyo naweza kusema pia labda hofu yao ni ya msingi. but when there is passion utakomaa mpaka kieleweke despite the harsh conditions. mtu passionate atataka aone results.
 
Mkuu Kubota, binafsi hata mimi natoa heshima kubwa sana kwa waasisi wa na wachangiaji wa Jami FORUM. it's a forum of it's own kinn, yani madarasa kibao. na kweli ukiingia huku hutoki...lol big up sana. kweli kabisa ni tabu kweli kufanya yote mawili, ila perhaps ningekuwa nimeajiriwa na serikali yetu hii tukufu ninge manage. nasikia huko work load ni ndogo! sijui ni kweli? na ni kama vile hamjabanwa sana!! sijui pia kama ni kweli, na job security ipo ya kutosha as opposed to the private sector that i ve been working for ever since time memorial.

ninamfano mzuri wa jirani yangu mmoja amabe yeye nilifikiri amefanikiwa kwenye hili...yeye alikuwa vendor wa m-pesa, tigo pesa, dstv, luku,.you name them. wafanyakazi kila siku wanampigaje? ni shoti tu deile. baadae akaja akampata mtoto wa ndugu yake ambaye waliwekeana makubaliano tofauti kidogo. kwamba yule kijana atafanya kazi pale kwa uaminifu kwa miaka mitatu, atakuwa analipwa nusu tu ya mshahara wake wa mwezi. then baada ya miaka mitatu anamaliziwa the other 36 halves plus kumpeleka shule(yule kijana hakufanya vizuri form four finals). hivi tunavyoongea three years have lapsed na duka la jirani yangu lipo pazuri, na mtaji umekua, kijana hajawahi kuiba hata senti, hajawahi kupata the so called shoti not even once..na yupo shuleni amerudia form three. ila jirani yangu amerudi kwenye same challenge he was facing before, ya kupata mfanayakazi mwaminifu. labda hii inaweza kukusaidia mkuu.

Kila la heri.
Mkuu Ngamakisi nashukuru sana kwa wazo lako. Hapo kuna elimu kubwa sana nimeiona. Nitaliboresha zaidi maana hakuna jinsi. Kuhusu hayo uliyoyasema serikalini ni kweli hali iko hivyo. Hiyo hali ya security ndiyo adui wa maendeleo. Wataalamu wanasema mtu aliyeko kwenye CONFORT zone huwa hataki misukosuko. Kwa wenye damu ya ujasilia mali, piga ua kuajiriwa ni suala linapaswa kuwa la mpito tu na siyo kuchukulia kuwa nimefika. Nikilima eka 20 za mpunga ambazo ninazitunza kwa miezi 4 tu ambapo wala siyo full time toiling kama ofisini, mwisho wa siku naingiza kipato ambacho ni mara mbili ya mshahara wangu kwa mwaka mzima! (Just in 4 months tu), sasa hii miezi nane inayobaki ......., nikilima vitunguu tena? Sasa haya mavitu ninafanya kwa kujibanabana lakini nafanikisha hakuna shaka kwamba nikiyatokea mzima mzima sitajutia, labda mito yote ikauke na watu wasile chakula tena, Kaka tangulia nitakukuta, acha nimalizie kukamilisha maandalizi maana hata kuchoma meli kwenyewe ni nahitaji niandae kiberiti na petrol.
 
Sana tu Kubota, yataka maandalizi sikatai. Mimi mwenyewe nime battle sana na akili yangu over this wala siwezi kuelezea. Ila kama upo kwenye comfort zone itumie mkuu, ni fursa kwako pia kufanya maandalizi yako vizuri pia kutunisha kale kamfuko ketu pendwa kale( naamini unanipata).

Hili swala la kuwa na wasaidizi waaminifu nalo ni changamoto kweli jamani. Nadhani ndio maana hawa wenzetu waasia n familia nzima inahusika na biashara. yani alomst all their businesses are home businesses ila bado kuna siri hatujaijua. mbona sisi ndugu zetu wanatupiga za uso? tena ngumi sio makofi yani mpaka mtu mzima unatamani kulia. hii inanisumbua sana kwasababu kufikia hatua ya kuweza kuajiri mtu na yeye akabenefit from your entrepreneurship ni sifa nzuri, it is a credit. kwahiyo mkuu siku ukipata the right mode for this tafadhali weka jamvini kwa faida ya wote.

Kila la heri
 
you are there to accomplish his dream not yours. sorry kama naandika sana but this is the spirit i have.[/QUOTE]
Ukweli utabaki kuwa ukweli, ila mkuu inauma hii kauli inauma. Huu ni mwaka wa kumi sasa kumbe nina accomplish someone's dream. Acha tukusanye mitaji kwao katika mazingira hayo hayo ya kufull fill their dreams. 2014 ni mwaka wa KUCHOMA MOTO MELI.
TO DARE IS TO DO!!!!
 
Sana tu Kubota, yataka maandalizi sikatai. Mimi mwenyewe nime battle sana na akili yangu over this wala siwezi kuelezea. Ila kama upo kwenye comfort zone itumie mkuu, ni fursa kwako pia kufanya maandalizi yako vizuri pia kutunisha kale kamfuko ketu pendwa kale( naamini unanipata).

Hili swala la kuwa na wasaidizi waaminifu nalo ni changamoto kweli jamani. Nadhani ndio maana hawa wenzetu waasia n familia nzima inahusika na biashara. yani alomst all their businesses are home businesses ila bado kuna siri hatujaijua. mbona sisi ndugu zetu wanatupiga za uso? tena ngumi sio makofi yani mpaka mtu mzima unatamani kulia. hii inanisumbua sana kwasababu kufikia hatua ya kuweza kuajiri mtu na yeye akabenefit from your entrepreneurship ni sifa nzuri, it is a credit. kwahiyo mkuu siku ukipata the right mode for this tafadhali weka jamvini kwa faida ya wote.

Kila la heri

Mkuu Kwenye Red hapo, Tatizo kubwa ni kuto kutoa elimu kwa huyo Ndugu yako watu wengi huishia tu kukabidhi majukumu bila kumpa elimu Ni lazima elimu ya kutosha itolewe,
- Ni lazima ndugu zako wapate elimu ya biashara, Umuhimu wa biashara yako kwako, Na faida gani watipata wao mbele a safari, watu huishia kuoneana aibu kisa umemeweka Shemeji yako so hata akfanya nini haulizwi,

Na mwisho ili kweli kufanya the real business basi huna budi ku opt moja, kuendelea na kazi ya kuajriwa au kuchoma meli moto na kuendelea na shughuri zako, Why? Wewe ndo mwanzilishi wa Idea, wewe ndo unapaswa kupigania wazo laoko na si mwingine yoyote yule, si mke wako wala shemeji wala mdogo wako wala kaka wala Dada it is you,

Biashara yako haiwezi kusonga mbele bila wewe na biashar sio kuanzisha na kuweka watu na wewe kubakia kupiga simu kuulizia, Mwazno wa biashara ni lazima upartcipate vilivyo na baadae ikisha kuwa kubwa ndo unawza kaiimisha majukumu, sasa tunacho kifanya ni kinyume, tunakaimisha majukumu mwanzo wa biashara,
 
Ukizingatia idea ni yako yani ni wewe tu ndie unajua nini unataka kufanya kwahiyo wewe ndie utakaefanya kwa ufanisi zaidi. Follow up, close M & E vinahitajika sana. unajua mara nyingi tunasikia watu wana comment'' dah yani jamaa kafa na mali zake zimeondoka''. actually kinachotokea hapa ni kwamba jamaa anakuwa ameondoka na idea yake, ni kama aliowaacha nyuma hawana passion na ile biashara kama alivyokuwa nayo marehemu mhusika. yeye ndie alikuwa anajua mbinu zote, hapa afanye vipi, apunguze vipi costs, nk. na labda anakuwa hajashea na waliomzunguka. succession plan sio ishu ya kuignore wadau.
 
Sema tu vile sie wafanyakazi, academics hatusemi yanayofanyika usiku vyumbani mwetu: nani ambaye hakukesha ili tu apate cheti, degree ili aende kutembeza bahasha aajiriwe? hata huku makazini bado kuna stress hadi kukosa usingizi: deadlines, evaluation, performance appraisals, training, presentations yote haya unavuna vi hela na vi praise ambavyo ni vya muda mfupi na sana vinazidi kukubana uendelee kuwa muajiriwa daima. Yaani mimi nakupongeza sana kwakweli na umekuwa wazi kuonyesha changamoto za ujasiriamali sio kutajirika haraka na bila kuwa committed kama wengi wanavyofikiria: ITS A MATTER OF DEATH AND LIFE, UKIISHACHOMA MOTO MELI THERE IS NO RETREAT NO SURRENDER!
Najaribu kupiga picha, kuamka ucku si kwa kwenda msalani bali kuangalia vifaranga. Ujasiliamali unaweza kukufanya uonekane punguani kupitia macho ya raia wa kawaida.
Hongera kwa mradi mzuri na wenye mafanikio. Nimeandika nikiwa nimesimama kwa heshima yako mkuu. Salaam
 
Sema tu vile sie wafanyakazi, academics hatusemi yanayofanyika usiku vyumbani mwetu: nani ambaye hakukesha ili tu apate cheti, degree ili aende kutembeza bahasha aajiriwe? hata huku makazini bado kuna stress hadi kukosa usingizi: deadlines, evaluation, performance appraisals, training, presentations yote haya unavuna vi hela na vi praise ambavyo ni vya muda mfupi na sana vinazidi kukubana uendelee kuwa muajiriwa daima. Yaani mimi nakupongeza sana kwakweli na umekuwa wazi kuonyesha changamoto za ujasiriamali sio kutajirika haraka na bila kuwa committed kama wengi wanavyofikiria: ITS A MATTER OF DEATH AND LIFE, UKIISHACHOMA MOTO MELI THERE IS NO RETREAT NO SURRENDER!

Mama I could not agree with you more.

Hizi kazi za watu targets, mara andaa presentation, mara Appraisal mara sijui Internal Audit , mara compliance mara mtu wa Risk kapita, mara Extyernal Auditor yaani ni full stress. Nilipoanza kazi fresh from chuo macho yalikuwa yanaona vizuri, mwili ulikuwa mzuri sina hata dalili ya kitambi, mgongo hauumi, tumbo lipo safi. Sasa hivi hapa nilipo tumbo wanasema kuna vidonda, macho yameshaanza kufa kukodolea kompyuta, mgongo sometimes unauma bila sababu ya msingi, Kichwa nayo sometimes inagonga, kitambi nacho napigana nacho kufa kupona nikijisahau kinachomoza. Yaaani haya maisha ya kuajiriwa ni upunda na utumwa sijui kama sukari na BP zitanikosa within these 10 years nikiendelea.
 
Kusema kweli changamoto kubwa ktk biashara zote ni kupata wafanyakazi au partners wenye moyo na biashara yako kama wewe au hata kuliko wewe! Lakini kitu kingine ni jinsi gani wewe utauendeleza hii hali kwa wafanyakazi wako. Kikubwa nilichojifunza kupitia miaka mingi ya kufanya private sector na pia kuajiri watu kuhusu wafanyakazi 1. Jifunze kuajiri mtu sahihi (kusema ukweli kuna watu hata ufanyeje sio sahihi aidha kwa kazi hii au kuwa ktk kampuni hii, anaweza kupata sifa zote akiwa ktk kazi nyingine lakini kwako asiwe mtu sahihi kabisa. 2. Kuwatia moyo na kuwapongeza kwa kazi wakifanya vizuri na kuwaonya wakikosea, hii iwe ni kawaida na ikizidi hata kwa maandishi ili usijepata kesi za kufukuza watu bila sababu na hapa achana na mambo sijui ya ndugu au kabila angalia performance 3. Lipa mshahara kwa wakati na sahihi kwa kazi husika, jitahidi kuongeza mshahara kila inapobidi na utoe sababu, kumbuka kutoa tips au bonus endapo kuna faida nzuri na kutoa onyo hasara ikitokea. Jaribu kukaa na wafanyakazi wako personally na kusikiliza shida zao binafsi na jaribu kuwasaidia hata kwa mkopo hii itaonyesha unawajali na hivyo kujituma kwa bidii zaidi. 4. Epuka kuwa na majungu na maneno ktk mradi wako, ukiajiri ndugu asiwe ananyanyasa wafanyakazi kwa kuwashtakia na kuleta maneno kwako jaribu kuwa neutral na kumsikiliza kila muajiriwa wako utashangaa kusikia wanayofanya hata walio ndugu na hii itasaidia kuwafanya wote kuwa na hofu ya kuhujumu wakijua uko free na kila mfanyakazi anaweza kukuona na kukueleza chochote mradi kuwe na mipaka. 5. Ili kuifanya biashara yako iwe endelevu kuwa muwazi kwa familia yako kwamba hii ndio tegemeo lako na malengo yako ni ufikie wapi iwe watoto au mwenza wajue wazi nini lengo lako, changamoto na wapinzani wako ktk biashara la sivyo utashangaa hawa ndio wanaweza kuua mradi wako wakiamini hapo ndo umefika aua we ni milionea wanafuja kila kinachoingia(hii iko sana kwa waume, wake, watoto na extended family) wakiishakusikia kila siku unabwata hapa jamani sina kitu hela hii yote itaingia kufanyia hivi ili iwe vile hakuna atakayethubutu kuomba au kuchukua bila ruhusa. 6. Kila biashara ina malengo yake: ninafanya hiki muda huu ili nipate kiasi hiki ili nifanye hiki muda ule....inabidi wewe mwenyewe usimame ktk malengo yako, tatizo linakuja sisi wenyewe ni legelege unaweza kuwa mkali kwa familia ndugu na wafanyakazi wasimamie malengo yao lakini wewe mwenyewe ukashindwa kutimiza ya kwako mfano mauzo unafuaj kwa starehe halafu unachelewesha mishahara au kutolipa kabisa, unatakiwa uchangie pato la familia au kulipa mkopo wa mtaji unafuja unajikuta umeshindwa kulipa deni ni rahisi familia kutokuwa nawe tena ktk kusimamia mradi wako, ukishindwa kutimiza malengo yako omba msamaha na uahidi kulipa na uwe na sababu za msingi. 7. Kutoa elimu kwa wafanyakazi wako na hata familia kuhusu uendeshaji wa mradi wako ingawa vitu muhimu kama malipo na akaunti usiviachie kuwa huru (delegation of authority) unatakiwa kuwashirikisha na kuwaelimisha utendaji na uendeshaji wa mradi wako na mara nyingine huku ukiwa karibu unawaachia mamlaka ya kufanya vitu Fulani kasha kuja kuwaelekeza wapi walikosea na wapi wamefanya vizuri. Hapa ndio wenzetu wahindi na wazungu wanapotushinda kuirithisha biashara kwa familia au hata mfanyakazi kisha watoto, na hapa inajumuisha hata kuuza shares kama mradi ni mkubwa hii inamfanya mtu anakuwa bound kwenye biashara maana hata yeye atapata faida akijituma au mtafilisika. 8. Kuwa innovative na mawazo mapya na vilevile ruhusa wafanyakazi wawe innovative mradi isiathiri utendaji na mapato....wengine wataongezea
Mkuu Kwenye Red hapo, Tatizo kubwa ni kuto kutoa elimu kwa huyo Ndugu yako watu wengi huishia tu kukabidhi majukumu bila kumpa elimu Ni lazima elimu ya kutosha itolewe,
- Ni lazima ndugu zako wapate elimu ya biashara, Umuhimu wa biashara yako kwako, Na faida gani watipata wao mbele a safari, watu huishia kuoneana aibu kisa umemeweka Shemeji yako so hata akfanya nini haulizwi,

Na mwisho ili kweli kufanya the real business basi huna budi ku opt moja, kuendelea na kazi ya kuajriwa au kuchoma meli moto na kuendelea na shughuri zako, Why? Wewe ndo mwanzilishi wa Idea, wewe ndo unapaswa kupigania wazo laoko na si mwingine yoyote yule, si mke wako wala shemeji wala mdogo wako wala kaka wala Dada it is you,

Biashara yako haiwezi kusonga mbele bila wewe na biashar sio kuanzisha na kuweka watu na wewe kubakia kupiga simu kuulizia, Mwazno wa biashara ni lazima upartcipate vilivyo na baadae ikisha kuwa kubwa ndo unawza kaiimisha majukumu, sasa tunacho kifanya ni kinyume, tunakaimisha majukumu mwanzo wa biashara,
 
Yaani acha tu hujaongeza kufanya kazi ktk mazingira magumu mtu unaacha familia kwenda mbali na very risk areas nimewaza sana ili tu ulipwe ki allowance hivi hizi trips ningejipinda nikaenda huko shambani hata kwa mwezi mara mbili nikae wiki siningekuwa mbali sana?
Mama I could not agree with you more.

Hizi kazi za watu targets, mara andaa presentation, mara Appraisal mara sijui Internal Audit , mara compliance mara mtu wa Risk kapita, mara Extyernal Auditor yaani ni full stress. Nilipoanza kazi fresh from chuo macho yalikuwa yanaona vizuri, mwili ulikuwa mzuri sina hata dalili ya kitambi, mgongo hauumi, tumbo lipo safi. Sasa hivi hapa nilipo tumbo wanasema kuna vidonda, macho yameshaanza kufa kukodolea kompyuta, mgongo sometimes unauma bila sababu ya msingi, Kichwa nayo sometimes inagonga, kitambi nacho napigana nacho kufa kupona nikijisahau kinachomoza. Yaaani haya maisha ya kuajiriwa ni upunda na utumwa sijui kama sukari na BP zitanikosa within these 10 years nikiendelea.
 
Binafsi namshukuru muanzisha uzi mkuu Ngamakisi, umetoa elimu tosha kwa vijana ambao wengi wetu mawazo yanakuwa yamegota kwenye kuajiriwa shukran mkuu na nakutakia kila kheri, pia michango ya wanajamvi wengine kama Mkuu chasha mzee wa KUCHOMA MELI, mkuu kubota, mama joe na wengine wengi siyo siri michango yenu inasaidia na inaelimisha katika kuondokana na janga zima la kuajiriwa. Shukran sana wakuu binafsi naendelea kuufuatilia mnakasha huu kwa umakin zaidi.
 
Hili nalijua sana wakuu, i've been there, i've lived it. yani kuna wakati nilikuwa najiuliza hivi...idea ya mtu mwingine, targets zake lakini nizifikie mimi? nikaanza kuona pengine ndomana hata kuna baadhi ya vitu i couldn't comply.
and the performance appraisal gig. oh no. kwa uppande wangu hizi harsh conditions ndizo zilinipa msukumo zaidi. siku naamua lengo langu lilikuwa ni kuzalisha kiasi ambacho nalipwa ofisini, lakini kwakweli namshukuru Mungu, mpaka sasa nime burst my own targets na ku set my own lil record.
 
Binafsi namshukuru muanzisha uzi mkuu Ngamakisi, umetoa elimu tosha kwa vijana ambao wengi wetu mawazo yanakuwa yamegota kwenye kuajiriwa shukran mkuu na nakutakia kila kheri, pia michango ya wanajamvi wengine kama Mkuu chasha mzee wa KUCHOMA MELI, mkuu kubota, mama joe na wengine wengi siyo siri michango yenu inasaidia na inaelimisha katika kuondokana na janga zima la kuajiriwa. Shukran sana wakuu binafsi naendelea kuufuatilia mnakasha huu kwa umakin zaidi.

thanks mkuu Piere. Fm..ni furaha yangu kama nimekugusa mahala...hao wakuu uliowataja mimi binafsi nawachukulia ndio kama mentors wangu, ofcourse na wengine wengi wa hapa Ujasiriamali. Of course naamini katika individual thinking ila pia nasikiliza sana mawazo ya wengine. ni ngumu lakini yawezekana. zichange vema mkuu.
 
you are there to accomplish his dream not yours. sorry kama naandika sana but this is the spirit i have.
Ukweli utabaki kuwa ukweli, ila mkuu inauma hii kauli inauma. Huu ni mwaka wa kumi sasa kumbe nina accomplish someone's dream. Acha tukusanye mitaji kwao katika mazingira hayo hayo ya kufull fill their dreams. 2014 ni mwaka wa KUCHOMA MOTO MELI.
TO DARE IS TO DO!!!![/QUOTE]

Mkuu ngumbuke nakuunga mkono, mara nyingi ukweli kwa maana ya fact huwa mgumu kweli.Kwakweli kama kuna uwezekano wa kukusanya mtaji hapo ulipo please do it. mimi pia nawashukuru hawahawa waajiri. ugumu nilioupata umekuwa somo tosha kwangu, ila pia kiukweli sehem ya mtaji imetoka hapohapo. whether nilisave mshahara ama nilitumia mkataba wa ajira kama dhamana ya mkopo, fine tu. ila hili la kuchoma meli moto liko independent kidogo. zamani nilikuwa nikiona wafanyabiashara waliofanikiwa nadhani ni miujiza ila sasa najua ukweli, ni commitment inatakiwa because kiukweli ukilegea unaanguka mbona?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom