Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,002
Kuna nyaraka za aina mbili; ya kwanza ni makubaliano ya BAES na SFO kuhusiana na sakata la Rada la Tanzania. Tutaona kuwa serikali ya Tanzania haikuwa sehemu ya kesi yenyewe wala haikutoa hata hoja za kisheria.
Nyaraka ya pili ni jaribio la taasisi za harakati kuzuia makubaliano hayo (CAAT na Corner House). Kinachoshangaza ni kuwa muda wote tangu makubaliano hayo yaingiwe Serikali ya Tanzania haikujaribu hata mara moja - as far as I know kujaribu kuzuia makubaliano hayo. AG wetu hakutoa hoja yoyote au hata kujiunga na wanaharakati hawa. Naamini serikali ingefanya hivyo ingejionesha kweli inajali kwani makubaliano haya (ukisoma pingamizi la wanaharakati) yameipendelea sana BAES.
Inasikitisha vyombo vingi vya habari havijaripoti sakata zima hasa siku za karibuni kwa usahihi na hii inawezekana ni kutokana na watu kutokuchukua muda kujifunza juu ya sakata zima na badala yake wanakuwa wanatoa ripoti tu hata zisizokuwa sahihi. Natumaini nyaraka hizi zitawasaidia waandishi na wengine kuweza kuzungumzia sakata la rada na fedha za hisani toka BAES kwa usahihi zaidi.