Jeuri ya Urusi kwa nchi za Ulaya hii hapa

Cheche Mtungi

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
2,619
771
eu_pipes-2.jpg
===>Nchi za ujerumani,ufaransa na italy zinatumia kiasi kukubwa sana cha gesi kutoka Urusi,inawezekana Marekani wakabaki kupiga makelele kwa Crimea kujiunga na Urusi'

Soma zaidi hapa:Map: Why the EU and U.S. are out of step on Russia sanctions - CNN.com
 
na Tanzania tukianza kusambaza gesi yetu,tutakua na jeuri kama Russia.
 
Mumuuzie nani Gas, Rwanda? Kenya? Hapo Arusha tu, kwa nini Mama Yeyoo anunue Gas wakati kuna kuni kibao?

Ulaya wanatumia Gas kwa wingi kwa ajili ya ku-heat nyumba wakati wa Winter na maji ya moto kwa mwaka mzima. Pia wanatumia Gas kwenye magari na viwanda vyao vikubwa. Ndiyo maana utumiaji wao Gas ni mkubwa sana. Pia Urusi ipo karibu na hizo nchi na kwa sasa wamejenga kabisa Mabomba na siyo kubeba kwa meli. Hilo ndiyo linafanya hata Gas ya Norway iwe aghali kuzidi ya Mrusi.

Sasa wewe ulete kwa Meli kutoka Tanzania hadi huko Italy au UK, si ni rahisi kuleta kutoka Norway? Tungelikuwa kama ilipo Libya au Morocco, hapo wangelitukoma kama siyo kutuzushia vita ili wabebe gas kwa bei chee.
Anyway, tutapata Cake yetu kutoka kwa akina Kagame au Uhuru Kenyatta kama siyo Museven na Kabila. Hata SA wanaweza kununua, so longer Msumbiji hawajaanza na wao kuchimba yao ambayo ni nyingi kuzidi yetu.
Soon we will sharing the Gas cake with them.
 
Na gas ni silaha kubwa kwa mrusi bila hii gas mmarekani na mwingereza wangeshasogeza manuari za kumwaga na vifaa vingine ya kijeshi maeneo ya urusi kama walivyo fanya kwa sriya
 
Hivi unajua kua Russia na US walisaini mkataba wa kutopigana kwa muda mrefu sn na sisi hapa kwa kua hatufatilii mambo ya nje tutakuja na simplest and narrow arguement mara Ukraine siyo member wa NATO,mara gas ila atufikirii mbali ata kidogo.

Mwaka 2008 Mrusi aliingia Georgia na kutwanga mtu pale licha ya Bush Jr kupga mkwara za sanctions kama hizi za sasa ila KGB hakutishika ata kidogo. Hivi unaamini kwamba kama kungekua na sanctions Angela Merkel angempigia simu tena KGB PUTIN dakika za mwisho kabla awajaanza kutofautiana huko Brusselles ? Just for advice. Thanx.

Na gas ni silaha kubwa kwa mrusi bila hii gas mmarekani na mwingereza wangeshasogeza manuari za kumwaga na vifaa vingine ya kijeshi maeneo ya urusi kama walivyo fanya kwa sriya
 
putin alisema kwa namna yeyote kuiwekea vikwazo nchi yake kutaathiri pande zote mbili.
 
Urusi hategemei Gas pekee, ana technolojia nzuri sana kijeshi, kwa maana ya kutengeneza maslaha makubwa na makombora ya kivita anauza sana Asia,Afrika, Asia Pacific,Latin America na Middle East,msisahau hata serikali ya Misri Majuzi imenunua silaha za dola bil 2 Russia sasa kifedha hawa jamaa wako vizuri pia..sema kwasababu kwa muda mrefu walikua wana hali mbaya kwa sababu ya Rushwa na Tax evasion Urusi sasa anakuja vizuri kujipanga, Ulaya wote wanajua kwamba ile nchi sio mchezo...

Kuhusu Masuala ya kupeleka silaha kule Ukraine ni wazi ni wazo ambalo Ulaya na mkuu wao US wanaliona kama wazo zuri na kuweka mbinyo, mkiangalia zaidi kuivamia Urusi au kuisaidia Ukraine kupigana na Urusi ni ndoto za mchana kweupe, wote US na hata EU hawawezi kuthubutu kurusha risasi mooja tu kwenda Urusi maana itakua balaa kubwa sana hii ni kwasababu Kijeshi Russia yuko vizuri sana sana....

Kingne ni Kiongozi wa nchi hii Vladimir Putin,ni mzalendo na wala sio mpiga mayowe jamaa ni jembe kwa ufupi hata wenyewe Russia wanajiuliza huyu jamaa akiondoka nani ataishika hii nchi iende Sawia, iweze kupambana kidume na haya mauaji ya EU NA US??!!! WANAE kijana mmoja wanamuandaa nadhani ana miaka 36 kwasasa wao wenzetu wana mfumo wa kuandaa na kuchekecha viongozi sio kama hapababa akifa mwana anagombea!!!!!

Putin anaweza Fitna, Putin ni kamanda amekua KGB kwa muda mrefu, Putin ni Kachero na ana uzoefu mkubwa wa fitna za Dunia hii ambayo sisi Afrika ni kama kubwa Jinga hatuna usemi ndio maana hata juzi mliona hata nchi za Afrika Zote zilikua upande wa US /EU...huku ni kuendekeza njaa mana anachofanya Putin ni kuilinda Russia hivi nyie leo hii mnaweza kukubali Zanzibar Ijiunge na Rwanda waseme wao ni Coliation of the Willing ya kivyao, watusumbue sana kabisa hakuna hilo!!! wakiruhusu Ukraine kujiunga kule NATO anasogea anakua pale ana mchungulia Mrusi anaoga sasa nani ataruhusu huu ujinga??? #

Kuna ile warsaw pact ambayo US ameivunja kwa hiyo hapa ni undava undavu, na Putin anaweza Undava, wala si mchezo na juzi kafanya mazoezi ya Kijeshi ambayo yeye mwenyewe alikuapo kila siku, kuwaonyesha ni Jeshi la mtu mmoja na yuko tayari..mengineyo tusubiri tuone
 
lazima atambe tu kwasababu nchi za ulaya hazina sehemu ya kukimbilia pindi Urusi ikizima mitambo yake ya gesi inayoenda ulaya.
 
Inapendeza kuwa na nchi ya kusimama dhidi ya mabwana wakubwa marekani na wenzake wanapolazimisha uonevu. Hivi si Urusi inarudisha tu sehemu zake zilizojitoa huko nyuma? Kuna ubaya gani iwopo wananchi wenyewe wameamua hilo?
 
Na gas ni silaha kubwa kwa mrusi bila hii gas mmarekani na mwingereza wangeshasogeza manuari za kumwaga na vifaa vingine ya kijeshi maeneo ya urusi kama walivyo fanya kwa sriya

Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa Marekani nae ana shida sana ya Gas kama hizo Nchi za Ulaya,hivi unajua Reserve ya Gas na Mafuta ya Marekani amabayo haijaguswa kabisa?
 
Nimecheka sana wakati naangalia breaking news ya BBC NEWS eti vikwazo walizowekewa Russia ni travel bans and assets freezes of 21 officials from Russia and Ukraine dah hii kituko kulingana na jamaa walivoenda huko kwenye mkutano wao nilitegemea vikwazo vikubwa vya kiuchumi dhidi ya Russia kumbe travels bans and assets freezes on several officials.

Kwa hiki nadhani KGB PUTIN anaweza akaingia Ukraine na kuwataoa akina Yatsenyuk na kumrudisha Yunokovich na EU na US wasifanye chochote, trust me inawezekana sana ngoja tusubirie kituko kingne cha vikwazo kutoka US.

Nimeamini EU and the likes kwa KGB PUTIN wote chali hawawezi fanya lolote zaidi ya blah blah .
CC: Somoche.
 
Last edited by a moderator:
Nimecheka sana wakati naangalia breaking news ya BBC NEWS eti vikwazo walizowekewa Russia ni travel bans and assets freezes of 21 officials from Russia and Ukraine dah hii kituko kulingana na jamaa walivoenda huko kwenye mkutano wao nilitegemea vikwazo vikubwa vya kiuchumi dhidi ya Russia kumbe travels bans and assets freezes on several officials.

Kwa hiki nadhani KGB PUTIN anaweza akaingia Ukraine na kuwataoa akina Yatsenyuk na kumrudisha Yunokovich na EU na US wasifanye chochote, trust me inawezekana sana ngoja tusubirie kituko kingne cha vikwazo kutoka US.

Nimeamini EU and the likes kwa KGB PUTIN wote chali hawawezi fanya lolote zaidi ya blah blah .
CC: Somoche.

Muogope sana PUTIN...Jamaa ni jembe na US ANAONA kama vile Russia inatanua makucha kwa hali ya kutisha saana...
 
Back
Top Bottom