Jeshi la polisi wanawasaka watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti wa CHADEMA USA RIVER

Daudi Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
327
203
Jeshi la polisi Mkoani Arusha inawasaka watuhumiwa wawili wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kata ya usa river.

Watuhumiwa hao wawili walitoroka mahakama kuu kanda ya Arusha wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ameeleza kuwa watuhumiwa hao walimsukuma askari, alipoanguka wakamnyang'anya silaha na kukimbia nayo.

Stay tuned! .............................. There is so much more to come!
 
Samahani kuuliza, hivi uyu jamaa alikuwaga anaitwa said mwema bado ndio igp? Kaenda masomoni au likizo?
 
Wakuu kuna habari imenishtua sana eti yule jamaa aliyemchinja mwenyekiti wa Chadema Arumeru Mashariki ndiye yule aliyemny,ang,anya askari bunduki na kukimbia jana???
kama ndio hivyo basi tujipange upya kwani hiyo movie itakuwa ilipangwa kutoka juu,nina mashaka na nepi kwa kuwa ndiye anayefanyaga deal kama hizi ambazo haoni mwisho wake utakuwaje
 
Kwa hbr za kuaminika ni kwamba hakika aliyekimbia jana pale HQ ni yule mwalifu nambari moja aliyemchinja yule marehemu Mbwambo Mwenyekiti wa Chadema pale Usa river!

Hakika ni hofu sana na jeshi letu la polisi! Hasara tupu!
 
Hivi hawa makamanda na wasemaji wa jeshi la polisi wanapimwa akili kabla ya kupewa vyeo.Mbona wote wanashindwa kupangilia uongo.Je huyo askari alikuwa mwenyewe na je anadegedege au ndio anashindia viroba kupooza joto la kwenye zili nyumba zao
 
Hivi Hilo Jeshi la Polisi awaoni hata aibu kutorokwa na Mfungwa aliyekuwa kwenye mikono yao?Hizi Sinema za Tomy n Jery sijui zitaisha lini.
 
Yawezekana ni jambo ambalo lilipangwa na waliowatuma kuua ili kupoteza ushahidi.
 
Danganya toto hii,wamewatorosha alafu wanazuga wanawatafuta.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwa hali hii, kwa wale watu ambao walikuwa kinyume naye wakae ktk hali ya tahadhari kwani anaweza kuwadhuru/kuwaua ili kupoteza ushaidi
 
Hii tz lini vituko vitaisha hapa maana inakuwaje watu wanapotea

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
[h=2]Mahabusu wapora askari polisi bunduki, watoroka
*Ni aina ya SMG akiwa na risasi kibao
[/h]Mahabusu wawili wanaodai kuwa na kesi ya mauaji wametoroka wakiwa chini ya ulinzi wa polisi katika Mahakama Kuu jijini Arusha baada ya kumkaba askari aliyekuwa anawalinda kisha wakampokonya bunduki aina ya SMG na kukimbia nayo.

Habari zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabas, baada ya mahabusu hao kufanikiwa kumpora askari huyo silaha, waliruka uzio na kuingia katika mto ulioko karibu na mahakama hiyo na kutokomea kusikojulikana.

Mashududa hao walisema kuwa baada ya tukio hilo, polisi walianza kuwasaka mahabusu hao na kufanikiwa kuipata silaha ikiwa imetelekezwa juu ya jiwe kwenye mto huo ikiwa na risasi zote.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao mahabusu hao walikuwa wanatoka kwenye chumba cha mahabusu kwenda kupanda karandinga kwa ajili ya kurudishwa mahabusu katika gereza la Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Taarifa za awali zilizopatikana ambazo hata hivyo, hazijathibitishwa zimedai kuwa mahabusu hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ambayo yalifanyika wilayani Arumeru.

Tukio hilo lilizua hofu kubwa mahakamani hapo baada ya kuwalazimu baadhi ya watumishi wa mahakama hiyo kujifungia ndani ya vyumba vya mahakama wakihofia mahabusu huyo kuwafyatulia risasi.

Kamanda Sabas aliahidi kulitolea ufafanuzi tukio hilo leo na kuongeza kuwa polisi inafanya uchunguzi sambamba na msako mkali wa mahabusu hao.

Mashuhuda wengine waliozungumza na NIPASHE walisema kuwa tukio hilo lililotokea saa 7:30 mchana
lilifanyika kwa kasi kubwa baada mahabusu huyo kumvamia askari polisi kisha kumkata mtama na kumnyanganya bunduki hiyo.

"Yule bwana baada tu ya kumnyanganya akawa ameikoki ile bunduki huku askari akiwa chini amelala, wakati huo askari wenzake hawakuwa na silaha hivyo ilikuwa vigumu kumsaidia."

"Hata hivyo mahabusu huyo alipoona upenyo wa kukimbia alichomoka mbio na bunduki hiyo mkononi akielekea mto uliopo jirani kabisa na mahakama hiyo," alisema shuhuda mmoja Abdalah Jumanne aliyeshuhudia tukio hilo.

Habari ambazo zimetanda jijini hapa lakini hazikuweza kuthibitishwa na upande wa polisi zilizodai kuwa mahabusu huyo alikuwa ni moja ya watu waliohusika na mauaji ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Usa River aliyeuawa kikatili muda mfupi baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashari
ki.
 
Back
Top Bottom