Jeshi la Polisi laweka wazi namba ya kuwasiliana na IGP

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Jeshi la Polisi Tanzania limewajulisha umma kuwa kuna mabadiliko ya namba ya simu ya mkononi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) ambayo wananchi walikuwa wakitumia kumpigia pale wanapohitaji msaada au kufikisha malalamiko kwake.

Kupitia taarifa yake kwa Umma Jeshi limesema kuwa namba ambayo ilikuwa imewekwa katika Vituo vyote vya Polisi ilikuwa ni 0684 111111 na kubainisha kuwa namba hiyo haitatumika tena kuwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania badala yake namba mpya itakayotumika kwa sasa ni 0699 998899 na itakuwa inapatikana wakati wote, usiku na mchana.

Namba hii tayari imeshawekwa kwenye vituo vyote vya Polisi nchini.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi wote kutumia namba hiyo kwa ajili ya mambo muhimu ambayo wataona hakuna msaada mwingine kuanzia ngazi ya Kituo zaidi ya kumpigia yeye.
 
Back
Top Bottom