Umenena vyema Mh mbunge. Angalau wangetenga shule maalum za serikali kwa ajili ya watoto wa viongozi wakuu / waandamizi wa serikali, ili iwe rahisi kwa usalama wao,ikiwemo usafiri,malazi na chakula. Viongozi hao wenye watoto watachangia gharama za uendeshaji(watu wengine wenye uwezo watoto wao waruhusiwe pia). Tunao mfano wa mabalozi na wanadiplomasia wengine kuwa na shule kwa ajili yao.
Watoto wa Nyerere , Mwinyi,Sokoine na viongozi wengine wa enzi zao tulisoma pamoja,tulicheza pamoja,tulifanya usafi na kilimo wote,tulikula wote chakula cha shule, tulilala bweni moja,JKT wote tulikwenda. Tunajua mfumo umebadilika,tunahubiri ujamaa lakini tunaishi kibepari, ndo maana napendekeza shule maalum ya serikali kwa ajili hiyo.
Tuanzia kwake watoto wake wanasoma wapi? Aache unafiki iwe ka wote ( wabunge) na sio kuwasakama mawaziri tu!Yeye watoto wake wamasoma hizo shulee