Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 119,172
- 222,119
Promota wa Tamasha la Pasaka, Mtangazaji wa vipindi vya kwaya na Mgombea wa nafasi mbalimbali za uongozi huko CCM, Bwana Alex Msama ametajwa kuwemo kwenye 3 bora ya Matapeli Papa wa Viwanja DSM.
====
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kujisalimisha kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam akiwa na baadhi ya watu waliouziwa eneo la viwanja namba 1 kitalu 22 lililopo Kibada Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam ili kurejesha kwa wananchi eneo hilo lijengwa shule ya sekondari.
Silaa ametoa maagizo hayo alipofanya ziara katika eneo hilo Manispaa ya Kigamboni baada ya mgogoro huo kuwa wa muda mrefu kati ya wananchi wa eneo hilo na baadhi ya watu walionunua eneo la shule akiwemo Allex Msama.
Aidha, Waziri Silaa amemtaja Alex Msama kuwa ni tapeli namba 3 wa viwanja jijini Dar es salaam na tayari ameishaagiza baadhi ya maeneo anayoyamiliki kinyemela kunyang’anywa ikiwemo eneo la wazi na eneo la fukwe lililopo Mbweni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
UPDATES
- Mfanyabiashara Alex Msama akamatwa kwa tuhuma za Utapeli wa Viwanja vya Tsh. Milioni 800