Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria lahitaji bilioni 4/-

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, unahitaji jumla ya Shilingi bilioni nne (sawa na dola milioni 3.7 za Marekani) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi na makazi ya kudumu ya balozi.
Ubalozi huo tayari umepatiwa notisi ya kunyang’anywa eneo kwa kushindwa kuliendeleza.
Hayo yalielezwa na Balozi Msuya Mangachi, mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotembelea ubalozi huo uliopo jijini Abuja juzi kukagua eneo la kiwanja cha ofisi na kisha kuonana na watumishi wa ubalozi huo.
Balozi Mangachi alisema serikali ya nchi hiyo imeipatia Serikali ya Tanzania eneo la kujenga ofisi za ubalozi lenye ukubwa wa mita za mraba 5,294 na eneo jingine la kujenga makazi ya balozi lenye ukubwa wa mita za mraba 2,500 na kwamba tangu mwaka 1995 halijaendelezwa kwa sababu ya kukosa fedha za ujenzi.
Hata hivyo, Serikali ya Tanzania imeshatoa dola 80,000 za Marekani kwa ajili ya kujenga uzio ili eneo hilo lisichukuliwe.
Pia alimweleza Waziri Mkuu kwamba maeneo ambayo Tanzania inaweza kunufaika kwa kushirikiana na nchi ya Nigeria ni sekta ya elimu, kilimo, ufugaji samaki wa mapambo, biashara, michezo hasa soka na utengenezaji wa filamu.
Akitoa mfano, alisema Serikali ya Afrika Kusini imepata walimu wengi kutoka Nigeria wa masomo ya sayansi na Kiingereza lakini ni baada ya kuwafuata na kuwasaili nchini kwao (Nigeria) ili kubaini uhalisi wa vyuo walivyotoka na uhalali wa vyeti vyao.
Akizungumzia kuhusu fursa za kibiashara na Wanigeria, Balozi Mangachi alisema kuna fursa kubwa ya biashara kwa sababu wakazi wake hawalimi kwa kiasi kikubwa na kila kitu wanaagiza kutoka nje ya nchi yao hasa baada ya kugundua wana biashara kubwa ya mafuta.
“Pia kipato cha mtu wa kati ni kikubwa ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika,” aliongeza.
Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kupata walimu kutoka Nigeria kama ambavyo Afrika Kusini imenufaika kwa sababu Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa walimu hata katika vyuo vya kufundishia walimu hao.
Kuhusu kilimo, Waziri Mkuu alisema bado Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kuinua hadhi ya zao la muhogo ili uweze kupata soko zuri duniani.



CHANZO: NIPASHE
 
Ni hili imetokea kutangazwa lakini ukweli ni kuwa hiyo ni hali ya kawaida kwa uwakilishi wetu nje. Viwanja vimekuwa vikichukuliwa na wenyeji kila siku. Kama Taifa tumekosa commitment katika jambo hilo!
 
Back
Top Bottom