Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
Jamani mmenikumbusha kisa cha yule bibi wa Titanic ("a woman's heart is like an ocean, full but full of secrets"). Kama Jenerali angeamua kufungua moyo wake, akatueleza yaliyomkuta nadhani tungepata mafunzo mengi. Labda tumshauri atuandikie walau kurasa kidogo za kitabu ili tusome na pia wajukuu zetu siku moja wapate kuona jinsi binadamu alivyokuwa mnyama hatari. Jaribu kufikiria, mtu alikuwa DC (rais wa wilaya), MP n.k halafu anaambiwa hana chake. Tumshukuru Mungu kwamba hakupata ugonjwa wa moyo (kweli rafiki yako ndiye adui yako ..by Mr. Nice).