Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Hao jamaa sio ugonjwa tu umewaondoa huko,walikua na misala kibao,jeshi lina namna ya kudili na watu wagonjwa ambao hawako fit kuendelea na jeshi.mfano ba mdogo wangu mimi alikua mwanajeshi na bahati nzuri alikua huko kwenye mission congo,alivyorudi akapata ugonjwa flani uliomlazimu kuacha kazi,jwtz wamemtibu na mpaka leo anaendelea kutibiwa free pale lugalo ingawa sio mwanajeshi tena.
itakuwa ana kadi ya chama tu. Unaona hawa wanakamatwa kitu cha kwanza kuuliza ni uhusiano wao na Mbowe. Sasa kama wameshakuwa Raia wa kawaida uhusiano wao na Mbowe unashida gani?
 
Hii nchi imeoza kabisa,intelijensia inaruhusu vipi komandoo kuongea mambo mazito ya nchi hadharani?
Komandoo Anapata PTSD(post trauma syndrome desease),harafu anadhulumiwa haki zake anafukuzwa kazi kikatili,hapo Kuna watu weishayamezea mate mafao yake.
Wanajeshi kama Hawa ndio huwa wanakuwa recruited na foreign intelijence service,wanauza Siri zote za nchi!!wanazozijua.
Sahihi
 
Yaani mtu anafukuzwa kama mbwa! Komando anaishia kwenda kulima mahindi jembe la mkono!
Ndio maana hii nchi kila mtu ni mjinga tu , sasa kama hao kabisa wanaafanyiwa hivyo hivi raia wa kawaida ndio ataandamana kweli kudai haki mtaani?
Hawa jamaa wanakiburi cha luaifa kabisa jamani hili sio jambo la kawaida japo sisi humu tunaongea tu na kuliacha , hii inaonesha kuna kitu hawa jamaa wanategemea maana siku zote raia ndio huwa wanavunjiwa heshima sio jeahi, leo jeshi linadharirishwa!!!!! Kwa mara ya kwanza tangu uhuru, hii kitu hawajafanya tu, hili tukio ni lugha kabisa , kuna tafasiri yake wameonyesha hapo kwa vitendo, kuwa sasa wapo wao,
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Mzee mcha Mungu kama yule Akida "SEMA NENO MOJA ......NAO WATAJUTA"....then Jesus turned to the crowd saying " I have never find such kind of faith faith all over Israel"
 
bila elimu ya degree moja kwenye haya majeshi yetu ya tanzania ni shida tupu, utaishia kupigia watu saluti wakubwa, utatumiwa vibaya kama hawa kina Goodluck then ukizeeka unatupwa huko kwenu.

Training za ukomandoo ni ngumu mno zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu, kijana anahitimu unamtumia miaka 5 then unamuacha tena kwa fedheha, hii si haki.
Rais anapataje usingizi wakati watu waliojitolea kumlinda yeye na utawala wake wanadhulumiwa haki zao namna hii!

Nafahamu kwa taratibu za kijeshi haiwezekani na ni kosa la kihaini kwa wanajeshi kulalamika, lakini kupitia kesi hii ya ugaidi inayomuhusu Mbowe wananchi tumejua kinachojiri kwa vijana wetu. Ni wajibu wetu kama raia na wazazi wa vijana wetu hawa waliopo majeshini kuanza kuwapigania, tusingoje wawe wengi mitaani kwa sababu tutakaoumia ni sisi!
 
Kwa nini unafikiria kila kitu wanachofanya wazungu ni kizuri kuigwa na sisi?
Hizi mada zinaletwa kishabiki mno bila kujua shina lake,hawa wanajeshi walishafutwa ajira,wangekua kazini kuna utaratibu wa ukamatwaji waje,hawa ni raia wenzetu,kingine mfano umemkamata jambazi unataka akuonyeshe silaha kaficha wapi,utambembeleza akuambie alikoificha au utatumia nguvu ili kupata information unazotaka?,hii system ya kutumia nguvu iko duniani kote ndio maana hata CIA wana black cell huko ndio shuguli ya kuextract information hufanyika,usitegemee kupata information kwa mtu trained kirahisirahisi
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Zamani tulikuwa tunaambiwa kwamba komando mmoja anaweza kupiga watu 1,000 kwa mpigo. Sasa nashangaa kusikia komando analia eti alikamatwa kiholela na kuteswa. Ajabu!
 
Hata mtu akifukuzwa kazi stahiki zake lazima apewe. Kama kuna mafao aliyokatwa katika mshahara akiwa kazini lazima alipwe.
Hao hawakufu
hawakufukuzwa kazi kuna tofauti ya kufukuzwa na kustaafu. Kufukuzwa maana yake wana diclare kuwa hawakustahili kumwajiri mtumishi kama wewe na wanafuta kila kitu na kukurudisha katika hali uliyokuwa nayo kabla ya kuajiriwa na wao wabaki kwenye nafasi ya karibu kana kwamba hawajawahi kumwajiri mtumishi wa hovyo na.mwenye tabia mbovu kama wewe
Kutaafu ni kiwango cha juu kabisa cha heshima kwa mtumishi wa uma na mwajiri anafurahi ukilitumia jina lake baada ya kustaafu.lakini kufukuzwa ni.fedheha na hakuna mwajiri yoyote atakubali ujitambulishe kwa jina la kampuni yake baada ya kui tarnish image ya kampuni yake kwa tabia mbovu iliyosababisha kufukuzwa kwa fedheha
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)

Kwakweli kunyanyasika kwa makomandooo Hawa kwenye kesi ya kisiasa ni DOA kubwa sana kwenye utumishi wa Mkuu wa a majeshi
Ingeeleweka kama kungekua na sababu genuine Lakini kama wameponzwa na kuomba kazi kwa Mh Mbowe basi ni uonevu na Jambo hili limeweka doa sana na malalamiko toka kwa Makomandoo wenzao

1. karibu wote ni wahanga wa kuondolewa jeshini baada ya madhara ya kimapigano sudan au DRC

2. je Haki za komandooo au Askari ni zipi pale anapoondoka kazini kwa madhara yeyote hasa mstari wa mbele

3. Je kuna ubaya gani kufanya kazi ya VIP protection kama ambavyo wastaafu wengine wanafanya kazi za ujuzi wao au walitaka wakawe walinzi wa usiku ?

kiu fupi hii kesi imeli expose sana Jeshi letu na kitendo cha Mkuu wa Majeshi kushindwa hata katika hatua za awali kuwasaidia vijana wake ni doa

pia imeonekana utawala uliopita ni askari wengi tu wa TPDF walikua wanakamatwa kimya kimya …. Hii ni fedheha na kupandikiza mbegu mbaya sana !
 
Hao kwa sasa sio askari wa Jwtz, wapambane na hali zao tu.

Kauli hii inaweza kutolewa tu na mtu ambaye hana heshima kwa Jeshi letu lakini angekua anajua hata asilimia 1% tu ya kazi ya commando usingesema hilo

na unatakiwa kujua commando au askari yeyote hata akiondoka au kuondolewa jeshini kama sio kwa UHAINI anabaki kuwa askari wa akiba ina maana likitokea lolote anaweza kutumika….ndio maana unaona mfano Ethiopia hadi askari waliostaafu wanarudishwa kusaidia …

Mkuu wa zamani wa Utendaji Kivita TPDF Col Alli Mahfoudh aliwahi kuondolewa jeshini lakini ilipotokea tatizo Msumbiji alitudishwa na kwenda kuwa Milllitary Attache kusaidia kama mshauri maalum wa vita ( kupambana na RENAMO)

KImsingi kama mtu hakutoka kwa uhaini a napumzika tu hafukuzwi
 
Back
Top Bottom