Je, wapinzani hawapotoshi kuhusu vitambulisho vya ujasiliamali?

Muju4

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
5,329
7,176
Wakuu habari zenu,

Katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi huu limejitokeza hili suala la vitambulisho vya ujasiriamali,nami nikasema si vibaya nikilileta hapa jukwaani tuweze kujiuliza yafuatayo:-

- Kama kusingekuwa na hivi vitambulisho je hawa wajasiriamali wangelipa tozo za biashara kiasi gani?

Ilikuwa kawaida kwenye masoko kuwa na ushuru wa biashara usiopungua TZS 500/=, sasa kwa mahesabu ya kawaida huyu mtu kama atafanya biashara kwa mwaka mzima bila kukosa

maana yake (500x30x12=180,000).

Hii maana yake si huyu mjasiriamali angelipa 180,000/= kwa mwaka, lakini kwa sababu ya vitambulisho hivi atalipa 20,000/= tu ?

Sasa najiuliza jambo lipi ni jema kati ya haya mawili kulipa 20,000/= au kulipa 180,000/= kwa mwaka?

Nafikiria tungekuwa wakweli wa nafsi zetu nakuacha kuwadanganya au kuwayumbisha wananchi wenzetu.

Ni hayo tu nakaribisha kuelemishwa na pia povu ni ruksaa.

JPM 2020 - 2025

CCM 5 Tenaa
 
Umesema vyema sana.

Upinzani wanapotosha Maana halisi ya kuanzishwa kwa vitambulisho vya wajasiriamali.

Wanatachotaka ni kuteka kundi hili kubwa la Watanzania kwa nia ya kupata kura zao bila kutumia Sera kamili zenye Mashiko.
Kushinda na JPM hawataweza.

#TumetekelezaKwaKishindo
#TunasongaMbelePamoja
 
Hii maana yake si huyu mjasiliamali angelipa 180,000/= kwa mwaka, lakini kwa sababu ya vitambulisho hivi atalipa 20,000/= tu ?
Ingekuwa hivyo, watu wasingewekewa malengo ya kugawa vitambulisho, na visingetolewa kwa lazima kama ilivyo. Wafanyabiashara wenyewe wangevikimbilia.

Tangu lini uliona mfanyabiashara analazimishwa kupunguza gharama za kuendesha biashara yake mwenyewe?
 
Vp walikuwa wakilipa wanapewa risiti?
Sera ya Chadema vitambulisho hivyo vitagaiwa bure na pia kila mwananchi atapewa na passport book bure akihitaji kwa hiari yake..

Inasikitisha raia bima ya magari kuwa lazma lkn bima ya afya ya mtu sio kipaumbele Cha CCM...
 
Hakuna upotoshaji wowote ile sheet ya ile material inauzwa 10,0000 nadhani printing labda tufanye 2000 kwa kila kitambulisho hivyo ukikiuza bei juu kabisa ni 5000
 
Mkuu hapa issue sio kulipa kiasi gani, hoja ni kuwa hicho ni kitambulisho hivyo kuna ubaya gani kikitolewa bure kwa mjasiriamali mdogo?

Mfano bodaboda kabla hakuwa analipia tozo yoyote, sasa hivi anatakiwa kulipa hiyo elfu 20 je naye umemuondolea mzigo au umemuongezea?

Hawa wajasiriamali wadogo ambao wanatafuta fedha ya kujikimu wanahitaji kusaidiwa na sio kukamuliwa hela kama Meko anavyofanya sasa.

Wanahitaji kuwekewa utaratibu mzuri ambao baadae utawawezesha kuwa walipaji wa kodi na watengeneze ajira kwa wengine sio kuwalipisha elfu 20 kisha kuwaacha wazurure hovyo na kuishia kuwa machinga maisha yao yote.

Mbali na hayo, hii fedha inayo kusanywa haijulikani ni kiasi gani kimepatikana na wala inaenda kufanya kazi gani.

Yote kwa yote, unaye jaribu kumtetea 'kashalegea' na kasema kulipia vitambulisho sio lazima kwa hiyo hata wasipolipa hakuna shida.
tapatalk_1600752423126.jpeg
 
Wakuu habari zenu,

Katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi huu limejitokeza hili suala la vitambulisho vya ujasiriamali,nami nikasema si vibaya nikilileta hapa jukwaani tuweze kujiuliza yafuatayo:-

- Kama kusingekuwa na hivi vitambulisho je hawa wajasiriamali wangelipa tozo za biashara kiasi gani?

Ilikuwa kawaida kwenye masoko kuwa na ushuru wa biashara usiopungua TZS 500/=, sasa kwa mahesabu ya kawaida huyu mtu kama atafanya biashara kwa mwaka mzima bila kukosa

maana yake (500x30x12=180,000).

Hii maana yake si huyu mjasiriamali angelipa 180,000/= kwa mwaka, lakini kwa sababu ya vitambulisho hivi atalipa 20,000/= tu ?

Sasa najiuliza jambo lipi ni jema kati ya haya mawili kulipa 20,000/= au kulipa 180,000/= kwa mwaka?

Nafikiria tungekuwa wakweli wa nafsi zetu nakuacha kuwadanganya au kuwayumbisha wananchi wenzetu.

Ni hayo tu nakaribisha kuelemishwa na pia povu ni ruksaa.

JPM 2020 - 2025

CCM 5 Tenaa
Kitambulisho kinalipiwa na hizo tozo zipo palepale............
 
Hivyo vitambulisho wa wauzaji kama machinga na wamama na vitu vidogo vidogo kujipatia kipato kidogo cha familia havina umuhimu zaidi ya kuwaumiza tu, maana hao siyo wajasiriamali kama munavyowaita sana sana wengi wananunua kwa wajasiriamali ndo wauze wapate chakula, mtu ananunua nusu kilo ya karanga au unga wa maandazi apike auze gengeni unamchaji kitambulisho na bado atatoa pesa ya usafi eneo alilojipachika.
 
[
Mkuu hapa issue sio kulipa kiasi gani, hoja ni kuwa hicho ni kitambulisho hivyo kuna ubaya gani kikitolewa bure kwa mjasiriamali mdogo?

Mfano bodaboda kabla hakuwa analipia tozo yoyote, sasa hivi anatakiwa kulipa hiyo elfu 20 je naye umemuondolea mzigo au umemuongezea?

Hawa wajasiriamali wadogo ambao wanatafuta fedha ya kujikimu wanahitaji kusaidiwa na sio kukamuliwa hela kama Meko anavyofanya sasa.

Wanahitaji kuwekewa utaratibu mzuri ambao baadae utawawezesha kuwa walipaji wa kodi na watengeneze ajira kwa wengine sio kuwalipisha elfu 20 kisha kuwaacha wazurure hovyo na kuishia kuwa machinga maisha yao yote.

Mbali na hayo, hii fedha inayo kusanywa haijulikani ni kiasi gani kimepatikana na wala inaenda kufanya kazi gani.

Yote kwa yote, unaye jaribu kumtetea 'kashalegea' na kasema kulipia vitambulisho sio lazima kwa hiyo hata wasipolipa hakuna shida.View attachment 1578005
Mkuu kwani kweli huoni unafuu wowote kati ya 20,000/= vs 180,000/=? Hakuna taifa linaloendeshwa bila Taxes and levies, mimi naona serikali iliwaza vyema na imeweza kutanua vyanzo vya mapato.

unataka kuniambia bodaboda anakosa (20,000/360=55.55/=) Yaani ashindwe kulipa shillingi 56/= kila siku ambayo kwa mwaka ndio hiyo 20,000/=.

Hapana kwakweli hata Chadema mwaka 2100 itakapo kamata dola lazima itatoza kodi.

Nakubali kuelimishwa Mkuu
 
Jiwe anasema vitambulisho sio lazima ila mimi mwaka juzi alivyoanzisha niliona jamaa wanawalazimisha wafanyabiashara pale Mbagala Zakiem wakilazimishwa kuvilipia huku wamezungukwa na askari wenye SMG.
 
Hivyo vitambulisho wa wauzaji kama machinga na wamama na vitu vidogo vidogo kujipatia kipato kidogo cha familia havina umuhimu zaidi ya kuwaumiza tu, maana hao siyo wajasiriamali kama munavyowaita sana sana wengi wananunua kwa wajasiriamali ndo wauze wapate chakula, mtu ananunua nusu kilo ya karanga au unga wa maandazi apike auze gengeni unamchaji kitambulisho na bado atatoa pesa ya usafi eneo alilojipachika.

Mkuu 20,000/= ni kwa mwaka mzima ambapo kwa siku ni sawa na kulipa TZS 56/=.

Hakuna nchi ambayo itaacha kubuni au kukusanya mapato jamani, nchi ambayo haikusanyi kodi hata Mwalimu Nyerere alisema ni CORRUPT.

Tuache kuwapotosha watu.
 
Nenda kwanza kapitie dhana ya kodi, tozo na ushuru. Si kila mtu/mjasiriamali ana sifa ya kutozwa. Mtu anauza vitumbua apate hela ya kula siku hiyo unamtoza ili iweje?

Kazi ya serikali ni pamoja na kulea hawa watu ili baadae ivune matunda yake kupitia kodi. Ni sawa na kuchinja kifaranga ili upate nyama badala ya kukilea kiwe kuku ambapo kitataga na kutotoa kuku wengine.

Huyo boda boda ana fedha ya kurejesha kwa tajiri au alipokopa, analipa kodi kupitia manunuzi ya mafuta na vipuri, anahudumia familia na wategemezi, anahitaji kulipia matibabu, maji, umeme na manunuzi mengine kama ya nguo ambayo yana indirect tax ndani yake. Bado mtu huyu unamuongezea mzigo wa kitambulisho elfu 20 then unaona ni ndogo?

Tuelewane, hakuna anaye pinga watu kulipa kodi ila huu utitiri wa kodi na tozo za kinyonyaji kwa mtanzania wa chini hazikubaliki. Serikali isipende kuvuna mahali ambapo haikupanda, huo ni ukibaka kwa wananchi wake.

[

Mkuu kwani kweli huoni unafuu wowote kati ya 20,000/= vs 180,000/=? Hakuna taifa linaloendeshwa bila Taxes and levies, mimi naona serikali iliwaza vyema na imeweza kutanua vyanzo vya mapato.

unataka kuniambia bodaboda anakosa (20,000/360=55.55/=) Yaani ashindwe kulipa shillingi 56/= kila siku ambayo kwa mwaka ndio hiyo 20,00/=.

Hapana kwakweli hata Chadema mwaka 2100 itakapo kamata dola lazima itatoza kodi.

Nakubali kuelimishwa Mkuu
 
Back
Top Bottom