Je, wajua utofauti wa England, Great Britain na United Kingdom (UK)?

Safi sana . Na kwa kuongeza ni kwamba zaidi ya asilimia 60 ya marais wote waliotawala marekani wana asili ya taifa la Wales.
kuna mwingine alisema almost wote waliotawala US wana uhusiano wa damu na ufalme wa UK.......

(anyway, US, Canada, Australia, New Z, Israel, ni nchi zinazokaliwa kimabavu na walowezi wa kingereza mpaka leo........).......
 
Inawezekana hili.
 
Wengi huwa wanapata shida kujua utofauti wa haya maneno hususan pale unaponunua bidhaa na kukuta nyingine imeandikwa 'Made in UK, nyingine 'Made in England' nyingine 'Made in Great Britain'.

Sasa utofauti wake ni huu hapa, ungana nami Didas Tumaini nikujuze.

✅ England
England au kwa kiswahili Uingereza ni nchi kama ilivyo Tanzania. Na makao yake makuu ni London kama ilivyo Dodoma kwa Tanzania. Raia wa hii nchi tunawaita English (mwingereza)

✅Great Britain
Great Britain ni muungano wa nchi 3, ambazo kwa pamoja makao yake makuu ni London. Nchi hizo ni

• England (kwa Wayne Rooney)
• Scotland (Kwa mctominay)
• Wales (Kwa Rayn Giggs)

Raia wa Scotland tunamwita Scottish na Wales ni Welsh.

✅ United Kingdom
Ni muungano wa Great Britain pamoja na Ireland ya kaskazini ( Northern Ireland), kwa maana hiyo United Kingdom (UK) ni muungano wa nchi nne. Nchi hizo ni

• England
• Scotland
• Wales
• Northern Ireland (kwa Jonny Evans na George Best)

Makao makuu ya UK ni London. Wakati mwingine United Kingdom inaweza kuitwa 'United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland'. Raia kutoka Ireland wanaitwa Irish.

🔑Kumbuka; UK na Great Britain ni miunganiko ya nchi, na kila nchi hapo ina mji wake mkuu. Kama ifuatavyo:

• Scotland ni Edinburgh.
• Wales ni Cardiff.
• Northern Ireland ni Belfast.
• England ni London.

📝Nimeeleweka Vijana wangu?

Didas Tumaini
Kwenye Great Britain maelezo hayapo sawa.
 
Hongera mtoa mada
Kwanini Nyerere hakuchukua huu muundo wa Muungano akatengeneza muundo ambao mpaka Leo hutuulewi

Raisi wa Jamhuri ya Muungano
Waziri mkuu wa serikali ya Tanganyika
Waziri mkuu serikali ya Zanzibar

Na hata wengine wakitaka
Waziri mkuu wa Burundi
Rwanda nk
Naam,mwendo wa mawaziri wakuu tu,hata kwa Afrika yote kusingekuwa na maswali yasiyo na majibu.
 
Hii kitu ndo leo najua, ubarikiwe!

Pia naomba unijaze ufahamu maana tunaambiwa Australia, New Zealand na nchi za Scandinavia zote ni mali ya Uingereza. Pia Canada na nchi zote za Amerika kusini tunaambiwa ni sehemu ya Marekani kasoro nchi ya Brazil tu!

Ukweli ni upi katika hilo?
 
maana tunaambiwa Australia, New Zealand na nchi za Scandinavia zote ni mali ya Uingereza
Australia na New Zealand ni nchi zilizotawaliwa na Uingereza. Na pia ni members wa Commonwealth

Commonweath(jumuiya ya madola) ni ushirikiano wa mataifa yaliyowahi kuwa makoloni ya Uingereza ambayo yameamua kuwa na ushirikiano na Uingereza katika nyanja mbalimbali mfano michezo. Ndio maana utasikia kuna mashindano ya jumuiya ya madola (Commonwealth games) yanayoratibiwa na Uingereza

Australia, New Zealand, Canada na Jamaica wao wameamua kwenda mbali zaidi kwenye ushirikiano na Uingereza. Wameamua hata kumtambua mfalme au malkia wa Uingereza kuwa head of state katika mataifa yao.

Australia na New Zealand wao wakaamua hata bendera za mataifa yao ziwe na sehemu ya bendera ya UK kama ishara ya ushirikiano wa karibu na UK

images (1).png

Yote hayo ni mataifa huru na wala sio sehemu ya Uingereza ila yana ukaribu na ushirikiano mkubwa na Uingereza. Hata lugha rasmi za nchi zao ni Kiingereza.

Nchi za Scandinavia hazina uhusiano huo na Uingereza
 
View attachment 2973890

Yote hayo ni mataifa huru na wala sio sehemu ya Uingereza ila yana ukaribu na ushirikiano mkubwa na Uingereza. Hata lugha rasmi za nchi zao ni Kiingereza.

Nchi za Scandinavia hazina uhusiano huo na Uingereza
Australi
Sio kama Uingereza ni muungano wa nchi zote hizo?
Uingereza ni England. Uingereza siyo UK
 
Wengi huwa wanapata shida kujua utofauti wa haya maneno hususan pale unaponunua bidhaa na kukuta nyingine imeandikwa 'Made in UK, nyingine 'Made in England' nyingine 'Made in Great Britain'.

Sasa utofauti wake ni huu hapa, ungana nami Didas Tumaini nikujuze.

✅ England
England au kwa kiswahili Uingereza ni nchi kama ilivyo Tanzania. Na makao yake makuu ni London kama ilivyo Dodoma kwa Tanzania. Raia wa hii nchi tunawaita English (mwingereza)

✅Great Britain
Great Britain ni muungano wa nchi 3, ambazo kwa pamoja makao yake makuu ni London. Nchi hizo ni

• England (kwa Wayne Rooney)
• Scotland (Kwa mctominay)
• Wales (Kwa Rayn Giggs)

Raia wa Scotland tunamwita Scottish na Wales ni Welsh.

✅ United Kingdom
Ni muungano wa Great Britain pamoja na Ireland ya kaskazini ( Northern Ireland), kwa maana hiyo United Kingdom (UK) ni muungano wa nchi nne. Nchi hizo ni

• England
• Scotland
• Wales
• Northern Ireland (kwa Jonny Evans na George Best)

Makao makuu ya UK ni London. Wakati mwingine United Kingdom inaweza kuitwa 'United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland'. Raia kutoka Ireland wanaitwa Irish.

🔑Kumbuka; UK na Great Britain ni miunganiko ya nchi, na kila nchi hapo ina mji wake mkuu. Kama ifuatavyo:

• Scotland ni Edinburgh.
• Wales ni Cardiff.
• Northern Ireland ni Belfast.
• England ni London.

📝Nimeeleweka Vijana wangu?

Didas Tumaini
Na Australia kwani haipo kwenye U.K?
 
Ni bora ungesema England sio UK

Hivi UK kwa Kiswahili inaitwaje?
United Kingdom. Unaundwa na muungano wa nchi za England, Scotland, Wales na North Ireland. Hizo nchi zote zina Serikali zake kamili separate na Serikali ya Umoja wa Ufalme wa Uingereza (UK) isipokuwa England. England ni kama Tanganyika. England wao wanategeme Serikali ya Muungano na Waziri Mkuu wa UK ndo Mkuu wao wa nchi pia. Kwa maana nyingine England ndo msanii Mkuu aliyevaa koti la Muungano kama Tanganyika ilivyojibatiza na kujiita Tanzania Ili amtawale mdogo .
 
Back
Top Bottom