Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,150
- 18,810
Ni kitu ambacho kinasikitisha kila ninapokifikiria, kwamba disaster ya Spice Islander ya Zanzibar iliua watu wanaokadiriwa kuwa 2800, wakati ile ya Titanic iliua watu wapatao 1500. Na ni kweli watoto na wanawake wengi sana walikufa Spice Islander ukilinganisha na Titanic. Machozi yananilengalenga nikifikiria kina mama katika Spice Islander wakiwa hawana la kufanya bali kukumbatia watoto wao waliokuwa wakilia kwa woga na kujiandaa kufa nao, wakijua hakuna ambalo wangeweza kufanya kujiokoa wao na watoto wao wadogo. Nafikiria ningekuwaje ikiwa mwanangu mdogo na mama yake wangekuwa katika hali ile, ndoto gani ningeota kila usiku nikilala; ninajaribu kuwaokoa?
Kwa nini basi dunia ilikaa kimya juu ya Spice Islander ukilinganisha na Titanic? Ina maana dunia inajali zaidi gharama ya meli zilizohusika kuliko roho za binadamu zilizopotea?
Na viongozi wetu wamesahau kama vile lilikuwa tu ni jambo la kawaida. Imekuwaje binadamu tumekuwa wanyama kiasi hiki?