Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,533
113,668
Wanabodi,

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama kawaida yangu, kila nipatapo nafasi, huwa natoa makala elimishi za kisiasa, kiuchumi na kijamii ziitwazo "Kwa Maslahi ya Taifa" kwa lengo la uzalendo kwa nchi yangu, kuisaidia nchi yetu, serikali yetu, viongozi wetu na jamii yetu.

Utambulisho
Kwa vile huu ni mwaka mpya, sio vibaya pia nikitoa utambulisho mdogo wa mwandishi wa makala hizi, Pascal Mayalla ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea, aliyehudumu kwenye tasnia ya habari ndani na nje ya nchi kwa takribani miaka 30, hivi sasa ni mstaafu hivyo ameamua kuutumia muda wake wa kustaafu kurudisha katika jamii "give back to the society", kile kidogo alichonacho, kwa leongo la kusaidia jamii na taifa kwa ujumla.

Makala za Kwa Maslahi ya Taifa Hutoka Gazeti la Nipashe Jumapili
Makala za Kwa Maslahi ya Taifa ni makala kwa mtindo wa swali, kisha hutoa hoja elimishi, na kumalizia kwa lile lile swali la msingi, ili jibu ulitoe wewe msomaji. Makala ya leo ni swali.

Je, Wajua kuwa kitu ambacho ni haramu, haramu hiyo isipo harimishwa inageuka halali?
Mfano kwa Waislamu kula nyamafu ni haramu!. Muislamu kula nyamafu ni haramu na unapata najis. Lakini ukila nyamafu, bila kujua kuwa ni nyamafu, ukidhani ni halal, ulaji huo unakuwa ni halal na utaendelea kula nyamafu bila kupata najis mpaka pale nyamafu hiyo itakapo harimishwa kwa kutamkwa kuwa nyama hiyo ni nyamafu. Hii maana yake ni haramu isipo harimishwa inakuwa ni halali.

Vivyo hivyo, kitu ambacho ni batili, kisipobatilishwa kinageuka halali!
Mfano ni ndoa inapofungwa inahesabika ni ndoa halali, lakini ili ndoa iwe halali, ni lazima ndoa hiyo iwe consummated ili kuihalalisha, ndoa ikishindikana kuwa consummated inakuwa ni ndoa batili, lakini kwa vile ndoa imeishafungwa , itaendelea kuhesabika ni ndoa halali mpaka pale itakapo batilishwa. Wanandoa wanaoishi kwenye ndoa batili bila kuibatilisha, wanahesabika ni wanandoa halali, ila wanaishi kwenye ubatili. Hii maana yake ni batili isiyo batilishwa itaonekana ni halali machoni kwa watu, lakini kiukweli in reality ni batilihiyo batili.

Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa kufuata, katiba, sheria, taratibu na kanuni
Mfumo wa uendeshaji wa nchi yetu, ni mfumo wa Mihimili mitatu ya Bunge, Serikali, na Mahakama, wakuu wa mihimili hii ni Rais mkuu wa mhimili wa serikali, Spika ni Mkuu wa mhimili wa Bunge na Jaji Mkuu , Mkuu wa mhimili wa Mahakama. Hawa wakuu watatu ndio watu muhimu zaidi kuliko watu wengine wowote, na upatikanaji wao, majukumu yao, madaraka yao na kuondoka kwako kumeelezwa kwenye katiba.

"The Doctrine of Separation of Powers, Check and Balance"
Kila mhimili una majukumu yake, nguvu zake na mipaka yake, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, jukumu lake kuu ni kutunga sheria. Mahakama ni kutafsiri sheria na kutoa haki, serikali ni kutekeleza sheria. Vyombo hivi vitatu, kila kimoja kina mamlaka yake ambayo hayatakiwi kuingiliwa na chombo kingine, lakini kila chombo ndio msimamizi wa mwingine kisije kukiuka mamlala yake, katika kanuni inayoitwa kwa Kiingereza, "The Doctrine of Separation of Powers, Check and Balance". Serikali itakusanya mapato, na kupanga bajeti ya matumizi yake ikiwa ni pamoja na kutoa pedha za uendeshaji wa mihimili ya Bunge na Mahakama na kupendekeza sheria, Bunge litaisimamia serikali kwa kuitungia sheria, kuipitishia bajeti na kufuatilia matumizi na Mahakama itatafriri sheria zilizotungwa na Bunge na kulidhibiti Bunge na serikali.

Moja ya maeneo magumu sana, ni eneo la kutafsiri katiba na sheria
Kwa bahati nzuri, mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari na mtangazaji, mimi pia ni mhitimu wa shahada ya Sheria, LL.B (hons) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), na kupata bahati ya kufundishwa sheria na baadhi ya waalimu mabingwa wabobezi wa sheria akiwemo Prof. Ibrahim Juma, Prof. Palamagamba Kabudi, Dr. Tulia Akson, Prof. Sifuni Mchome, Prof. Issa Shivji na wengi, na kwa upande wangu, moja ya masomo magumu sana ya sheria, ni Katiba, mwalimu wangu alikuwa Prof. Issa Shivji, ikatokea nikawa namwelewa sana, hivyo somo la katiba, ni moja ya somo niliofanya vizuri sana na kupata A hivyo japo jukumu la kutfsiri katiba ni jukumu la mahakama, naomba tafsiri hii yangu ya katiba, ichukuliwe very serious toka kwa mbobezi wa katiba.

Usaidizi Wangu Kulisaidia Taifa Langu Lifuate Katiba.
Sio mara moja wala mbili, nimekuwa nilikilisaidia taifa langu katika kuitafsiri katiba, hata lile swali langu kwa JPM, pale ikulu siku ile, lilikuwa ni swali la kikatiba:



Japo jibu nililo jibiwa pale, ni "Mayalla kwa Kisukuma ni njaa", amini usiamini swali lile lilisaidia sana kimya kimya kubadilisha baadhi ya mambo na kupunguza makali fulani, mpaka mpaka Mungu alipoamua kuimaliza kazi lakini amini usiamini, bila swali lile, saa hizi sisi wengine sijui kama tungekuwepo!.

Nimewahi kulisaidia sana Bunge letu tukufu, kupunguza kujipendekeza kwa serikali! Japo niliitwa Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Bunge, lakini kiukweli nilisaidia sana!



Hata Bunge letu tukufu licha ya kusheheni wanasheria ma nguli wabobezi, lakini sio wabobezi wa katiba, mwaka juzi ni mimi ndiye nililiokoa Bunge lisivunjwe baada ya Bunge kutoa Azimio fulani batili, kwa kugoma kufanya kazi na CAG!. Ni mimi niliwaeleza azimio hilo ni batili, na kuwaonyesha ubatili wake kikatiba na kisheria, kisha nikawaeleza nini kitatokea azimio hilo batili lingetekelezwa!. Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba Nashukuru somo hili lilieleweka Bunge likaliweka pembeni azimio lake batili kimya kimya na kutimiza wajibu wake.

Wiki hii imeanza kwa ubatili mwendelezo wa ule ubatili wa wiki iliyopita kumefanyika tena ubatili mwingine wa katiba katika Mhimili wetu huu huu wa Bunge letu. Baada ya Spika wa Bunge amejiuzulu, ila barua yake ya kujiuzulu imekiuka katiba! hivyo amejiuzulu kweli lakini kwa kutumia barua batili!. Barua ya kujiuzulu Spika, imepelekwa CCM badala ya Bunge. CCM likaliarifu Bunge limepokea barua, na Bunge lilakiri kupokea taarifa ya CCM, na mchakato wa kumpata Spika mpya ukaanza leo asubuhi kwa watu kuchukua fomu ya kuomba Uspika.

Mmoja wa waombaji hawa ni Naibu Spika, Dr. Tulia Akson, amekwenda kuomba na kujaza fomu ya kugombea Uspika huku akiwa ni Naibu Spika!. Huu ni ubatili!. Dr. Tulia, alipaswa kwanza kujiuzulu nafasi yake ya Naibu Spika, ndipo kisha akachukue fomu kuomba kugombea uspika.

Dr. Tulia alipoulizwa, amejitetea



Huyu ni mwalimu wangu wa sheria pale UDSM, ila kama nilivyoeleza kule juu, moja ya maeneo magumu sana kwenye sheria, ni eneo la kutafsiri sheria, hivyo kweli hili, kuna uwezekano mwanafunzi akaweza kutafsiri katiba vizuri kuliko mwalimu wake!.
Katiba imesema wazi kabisa, katika ibara ya 84 (2).

Kifungu cha katiba sifa ya kugombea Uspika.png

Katika kutafsiri katiba, tunaangalia mtunga katiba alidhamiria nini alipozuia Waziri na Naibu Waziri au "mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge". Mwalimu wangu Dr. Tulia, yeye kadhani maadam ametajwa Waziri na Naibu Waziri, ndio hao tuu, Naibu Spika hajatajwa!. Mbunge sio mtumishi wa umma ni mtumishi wa watu, lakini Spika, Naibu Spika, mawaziri na manaibu mawaziri ni watumishi wa serikali, hivyo wanabanwa na kifungu hicho, kinachomtaka mtumishi wa umma, anapowania nafasi yoyote ya kisisasa kwenye chama chake, kama ni ngazi ya chini, anachukua likizo bila malipo, lakini wa ngaz ya juu anajiuzulu kwanza nafasi yake ndipo agombee nafasi nyingine!. Hivyo ugombea wa Dr. Tulia kuomba Uspika ni bitili, tusiruhusu ubatili huu.

Sasa turudi kwenye ule ubatili wa kujiuzulu kwa Spika kwa kuanza na kifungu cha katiba cha kujiuzulu kwa Spika.

Kifungu cha katiba, kujiuzulu.png

Ibara hii ya 149 1 (c) ya Katiba imeelekeza Spika akijiuzulu, ataandika barua kuliarifu Bunge. Kitu kikiishwa elekezwa na katiba namna ya kufanyika, kikifanyika kwa namna nyingine yoyote kinyume cha katiba, kitu hicho ni batili. Kujiuzulu halali ni kuandika barua kwa mamlaka yako ya uteuzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Spika kwa vyombo, imearifu ameandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na copy kwa Katibu wa Bunge. Katiba imeelekeza barua ya kujiuzulu Spika, itatumwa kwa Bunge. Kitendo cha Spika kuandika barua na kuituma kwa CCM kabla ya Bungeni, kumeifanya Barua ya Spika kuwa Batilifu, Bila huo ubatilifu kuondolewa, then barua hiyo imekuwa ni barua barua batili!. Katibu Mkuu wa CCM ametoa taarifa ya kupokea barua ya kujiuzulu Spika na tayari ameliarifu Bunge kuhusu kujiuzulu huko, na Bunge limeipokea taarifa hiyo batilifu hivyo hivyo ubatili wake na kuikubali. Huu ni ubatili!. Kama Bunge ndio mhimili wa kutunga sheria, Bunge lisipofuata katiba kwa kuukubali ubatili, nani atafuata katiba?.

Haki ya CCM Kupokea barua ya kujiuzulu, ni kama Mhe Spika JYN angejiuzulu uanachama wa CCM, hivyo kupoteza ubunge wake na uspika, ndipo CCM ingeliarifu Bunge.

Jee tuliruhusu Bunge letu tukufu kukumbatia ubatili katika madogo, jee ubatili huu ukihamia katika makubwa, nani atakuwa na jeuri ya kulihoji Bunge?
A Way Forward.
  1. Kazi ya kwanza ya Vikao vya uteuzi CCM , iwe ni kulikata kwanza jina la Dr. Tulia, wala asijadiliwe ili yeye aendelee na Unaibu Spika. Na baada ya hapo hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake, kwa kitendo chake cha mtumishi wa umma kugombea nafasi ya kisiasa kupitia chama chake bila kwanza kujiuzulu utumishi wa umma. Ila iwapo CCM itaona Dr. Tulia Akson ndio the best, then ateuliwe tuu, lakini kabla hajagombea rasmi uspika kule Bungeni, lazima kwanza ajiuzulu unaibu Spika.
  2. Japo Spika Mhe. JYN tayari ameisha jiuzulu uspika, kujiuzulu huko, japo ni kujiuzulu batilifu, lakini kujiuzulu ni kujiuzulu tuu na Spika sasa amejiuzulu. Kwa vile barua ile batilifu imeisha kwenda CCM na imetangazwa imepokelewa na CCM kuliarifu Bunge, na Bunge nalo pia limetangaza kuipokea hiyo barua batilifu kutoka CCM na kukitangaza kiti cha Spika kiko wazi, lakini kwa kuheshimu katiba, lazima tuweke records straight na clean kwa kufanyika re filing kwa kufile barua proper kuondoa huo ubatili katika barua hizo uondolewe kwa kuandikwa barua rasmi kwa mujibu wa katiba.
  3. Nasisitiza nimesema barua ni batilifu na sio batili, hivyo Bunge lipokee kimya kimya barua mpya ya kujiuzulu kwa Spika iliyoandikwa kwa mujibu wa katiba, kisha Bunge ndio litoe copy kwa CCM.
  4. Kwa vile kazi ya kutafsiri sheria ni kazi ya Mhimili wa mahakama, mhimili huu sasa ujenge utamaduni mpya wa kutumia mamlaka yake yaitwayo, "Suo Motu" na kutoa tafsiri ya kisheria, kila kunapojitokeza mikanganyiko kama hii, bila ya mtu yoyote kuomba tafsiri hizo.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu
Je wajua, haramu Isipoharimishwa Inageuka halali?, na batili Isipobatilishwa inageuka halali!. Je, Tanzania, tuhalalishe ubatili huu wa kujiuzulu kinyume cha katiba kwa mkuu wa mhimili wetu wa Bunge? Kama katiba imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, kuna sababu gani ya msingi ya kutofuata katiba na badala yake tukumbatie ubatili?

Jumatatu Njema.
Pascal
 
Najua watakujibu kua Kwa saivi tupo na chama Kimoja ndio maana imekua hivo.

Ila huu ni uvunjifu mkubwa wa Katiba yetu,na sema sisi tushaanza kuichukulia katiba kama kitabu cha kiswahili darasa la Nne.
 
Paschal,

Ukiachana na lile tangazo je Umewahi kuiona barua ya Mheshimiwa Ndugai ya kujiuzulu Uspika?
Mkuu, tangazo lenyewe linajieleza. Linasema kuwa ameandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM na kumpa nakala Katibu wa Bunge. Ni kama tumeiona hiyo barua kuwa amemuandikia niliyemsema. Tangazo linaieleza barua husika, ingawa ni kwa kifupi. Ila aliyeandikiwa na kunakiliwa wametajwa.
 
Paschal,

Ukiachana na lile tangazo je Umewahi kuiona barua ya Mheshimiwa Ndugai ya kujiuzulu Uspika?
Mkuu Uzalendo Wa Kitanzania
Hatuhitaji kuiona barua ya Spika kujiuzulu uspika, kwasababu
  1. Spika mwenyewe ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa amemuandikia Katibu Mkuu wa CCM.

  2. Barua batilifu .jpeg
  3. Taarifa ya Katibu Mkuu CCM kupokea barua ya kujiuzulu Spika imetolewa
  4. Ofisi ya Bunge kukiri kupokea barua ya CCM, kujiuzulu uspika imetolewa.
P
 
Pasi, Wewe ni shiboub yaani mbobezi tambua ile ni taarifa na sio barua ya kujihudhuru. Kila kitu mnakitaka public?
Mkuu Ng'wanamangilingili , issue hapa sio contents za barua ya kujiuzulu bali nani amepelekewa barua hiyo. Spika ni muajiriwa wa mhimili wa Bunge, hivyo akijiuzulu barua ya kujiuzulu inapelekwa kwa mwajiri wake ambaye ni Bunge.

CCM ndio chama chake kilichompendekeza kwenye uspika ila sio mwajiri wake.

All and all, kwa vile katiba ipo na imeelekeza barua ya kujiuzulu ipelekwe kwa nani, kwanini katiba isifuatwe?.
P
 
Still umetetea sana uvunjifu wa katiba yetu.

Usitutoe kweli reli

You were magu-ass-wiper period!!!

And that dude never cared about that so called katiba.

He was a katiba and everything
 
Back
Top Bottom