Je, uundaji na mabadiliko ya sheria yanatija kwa Raia kwa kiasi gani?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Historia ya utungaji na upitishaji sheria nchini Tanzania, kwa mujibu wa tovuti ya bunge ni kuanzia mwaka 1963. Miaka miwili baada ya kupata uhuru, mwaka 1963 tukaunda sheria 246, hizi ndio idadi kubwa ya sheria kuwahi kupitishwa katika historia ya Tanzania. Aidha baada ya mwaka huo mwaka mwingine uliopitisha sheria nyingi ni 1977, ukifuatiwa na mwaka 1964 ambapo Tanganyika na Zanzibar ziliungana.

1704867446563.png

Sheria zilizopitishwa kabla ya mwaka 1990.

Aidha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi 2000, mwaka uliopitisha sheria nyingi ni mwaka 1994, ambao ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa kwanza wa mwaka wa uchaguzi wa vyama vingi. Hata hivyo taarifa za kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 hazipo kwa hiyo kuna missing variables kwa kipengele hiko.

1704867846031.png
Sheria za kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 1995. Rekodi za bunge hazijaweka sheria zilizopitishwa kuanzia mwaka 1996 hadi 2014. hivyo kwa sheria zilizopitishwa mwaka 2015 hadi 2023 ni kama ifuatavyo

1704866979811.png
Kwa rekodi hii ni kuwa mwaka 2022 ndio ulitambulisha na kurekebisha sheria nyingi zaidi kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015. Na mabadiliko yanaendelea kutokea,

Swali ni je mabadiliko haya yana tija ya kutosha kwa raia?
 
Back
Top Bottom