Je utakubali???

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,253
12,869
Fikiria wewe ni binti (au mzazi wa binti) ambaye unataka/ anataka kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma (illiterate) utakubali? Hebu tujadili wanajamvi... kama utakubali ni kwanini??? na kama hautakubali pia ni kwanini???
 
Passion of learning tumeumbiwa wanadamu wote so hata kama ni mkubwa mtu anaweza kurudi shuleni kusoma.

Labda hakuwa na uwezo au msukumo. Lakini kwa sababu anataka kuoa lazima kauwezo nako kako juu, kama ni msukumo mkewe mtarajiwa ni msomi atampa hiyo inspiration-kwa hiyo arudi shule....Wakioana wakiwa na difference kubwa kielimu basi hata intermarriage communication itakuwa na challenge nyingi which is bad for the health of the marriage...

Ndio maana wenye busara wanasuggest the easy way ni kutooana lakini kama wanapendana enough huyo mmoja anaweza kwenda kujiupdate kielimu...
kwa kweli ukichunguza kwa makini utaona hana sababu ya kuremain illeterate wakati yuko na msomi anayeweza kumuambukiza(reignite) the passion for learning which burns deep in us
 
Kuna wengine ambao uwezo wanao ila wanaona ule muda wa kupoteza kurudi shule ni mwingi ni bora atafute pesa ambacho ndo kipaumbele chake. Vp mtu kama huto utamshawishi vipi arudi shule?
 
Ni sawa hakuna shida provided wamekubaliana. Kusoma au kutokusoma siyo kigezo cha msingi cha mtu kuoa au kutokuoa.

Halafu inategemeana na unakosema kusoma, kuna familia nyingine form six kwao hajasoma sasa sijui utasemaje hapo?

Halafu kusoma ni lazima uelewe ni chance. Hebu assume watu wote waliomaliza vyuo wangekuwa na uwezo wa kusoma masters ingekuwaje? Kwa baadhi ya watu kushindwa kusoma masters kutokana na uwezo hivyo hivyo na baadhi ya watu wanashindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni.

Labda swali la msingi ambalo wewe ulitaka kulisema lakini umeshindwa kulisema ni je vipi mtu akitaka kuolewa na mtu maskini? Indirectly umehusianisha kutokwenda shule na umaskini!!
 
elimu yako kutwa unalalamika na ccm elimu nini bwana watu wana pesa nakutajia matajili darasa la tatu.. nenda sinza au kkoo mbeya njombe songea ukikuta hotel zote za kisasa zimeandikwa wanyama hotel mwenyewe std 3 rombo grean view darasa la pili engeen mbezi beach za seif mwalabu kasoma chuo tu madrasa hela ndio mpango nyie niaje
 
Mapenzi na kusoma havina mahusiano....
Unaweza kuwa na mtu yeyote kinyume na hayo mawazo yako....
Mapenzi ni kupendana bila kujali elimu
 
Unaposema kusoma unamaanisha level gani? Ni kuwa literate tu kama ulivyoonyesha kwenye mabano (kujua kusoma na kuandika)? Degreee ya kwanza? PHD au? Inawezekana hajasoma lakini ana dili za uhakika na mapenzi ya kweli.
 
Kupasi shule si kupasi maisha...wangapi wasomi wanasota. Kama hajasoma anavigezo vingine vya muhimu why not
 
kikubwa au maana yangu ni kwamba kuolewa au bintî yako aolewe na mtu ambaye may b kamalza std seven. yan ye ajuacho ni kusoma na kuandika na kusoma kwenyewe ukimlinganisha na mtoto wa std 1 wa st.marys anamzidi. afu bint mwenyewe awe kapitia chuo
 
Yah, unaolewa naye, tatizo liko wapi? Atajiendeleza badae, kama we mpenzi wa movie za kihindi itafute hii
"SOORYAVANSHAM" ndo utajua hata ucwe na elimu mapenzi yapo, na utakuja fanikiwa badae.
 
Swali gumu. Kwangu itategemea;
form4 or less - NO. I may date the person but not marry...
form6 - not sure
bachelor/masters - ideal
phd - lol, how many are even there?

I prefer small gaps between couple attributes and i wouldn't feel comfortable having such large gaps with my lover. Some discussions zinakuwa ngumu kidogo because of the gap.
i guess it's my background and environment inanifanya niseme hivi. Most of my friends frequently challenge me intellectually and that's something i'd want in a future partner.
for the record, i'm not a chick but I would do this if faced with a such a situation
 
kwan mwanaume ambae hajasoma haruhusiw kuoa mwanamke ambae hajasoma?@ww jamaa wa nch gan?..ww umesoma?

hapo hujajadili mada charles, inabdi ww ndo uulizwe wa nchi gan, maana maelezo yanayohitajika ni mengine na wewe umetoa mengine ambayo ni tofauti
 
Mapenzi na elimu havina uhusiano lakini wakati mwingine inabidi vitazamwe kwa undani...
Mmoja wenu akiwa na elimu ndogo sana kuliko mwenzie lazima kutakua na gap kubwa sana kwenye mitazamo ya maisha cause mmoja atakua ana upeo wa darasa la 7 mwingine ana upeo wa masters,vipaumbele vya maisha vitatofautiana kulingana na elimu na hapa ndo matatizo yataanza..
Kwa mtazamo wangu ni bora mwanamke ambaye hajasoma kuolewa na mwanaume aliyesoma than vice versa..
Wanaweza kuoana kama mwanaume amejijenga kimaisha lakini ndoa itakua na migogoro sana..
 
Fikiria wewe ni binti (au mzazi wa binti) ambaye unataka/ anataka kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma (illiterate) utakubali? Hebu tujadili wanajamvi... kama utakubali ni kwanini??? na kama hautakubali pia ni kwanini???

Mimi kama mzazi swali langu ni moja tu kwao, wanapendana na wako tayari kufunga ndoa? Kama jibu ni yes, kazi ni kwao! Mambo ya elimu hapo siingilii kati maana wapo vijana wasio na elimu na wanafanya shughuli binafsi na wana hela kuliko hata hao wenye elimu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom