Je uongozi tanzania ni ajira au opportunity, na kiongozi anawajibika kwa nani?

mabadilikosasa

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
379
85
Wana JF
Tanzania mie sielewi vizuri. Inakuaje viongozi hawawajibiki wa wananchi. Unaenda wilayani hata wananchi hawajui mkuu wao wa wilaya jina lake ni nani. Mfumo mzima kila mtu nateuliwa na rais na anawajibika kwake, wananchi hawana nafasi ya kupinga lolote.Mkuu wa wilaya anaweza akafanya anavyotaka. Rais anachagua watendaji mbalimbali anavyotoka, watoto wa ndugu zake, marafiki zake, etc. Anaweza kuchagua shemeji yake, mtoto wa mjomba wa shangazi nk. Nchi iendelee inategemea ni watu wa aina gani wapo katika nafasi mbalimbali. Rais anaweka watu ktk nafasi mbalimbali kutokana na mahusiano yake na wao. Pale inapokuja kumwajibisha inakua tabu. Kwa namna hii maendeleo ni ndoto. watafaidi tuu wale waliopo ktk mtandao wa rais.

Ili jambo ninanipa shida.
 
Back
Top Bottom