Arafat
JF-Expert Member
- Nov 17, 2009
- 2,581
- 758
..harakati za kuupinga ukoloni hazikuanzia DSM peke yake.
..maeneo mengi tu mikoani walikuwa wameanzisha harakati za namna moja ua nyingine kumpinga mkoloni.
..alichoweza kufanya Mwalimu ni kuzipa sura ya UTANGANYIKA na kuleta umoja ktk harakati hizo.
..katika harakati za kudai uhuru na Tanu na Mwalimu walipata msaada toka kwa watu mbalimbali hata wale ambao haikutegemewa wangesaidia. sijui kama unafahamu mchango wa Machifu mbalimbali, au shirika la kidini la kikatoliki la Maryknoll.
..maandiko ya Mohamed Said yako kuwakweza zaidi watu wa Pwani, na kupuuza mchango wa wananchi wa maeneo mengine ya Tanganyika ktk harakati za uhuru.
Great thinker asante umeongea yote muhimu, kama haelewi basi anaelimu ya chini ya darasa la nne