Kombania A kulikuwa na kiafande kinaitwa Mwashamba..ebwana hiki kijamaa noma kweli.
.Kwa Msange kombania B ilikua na maafande poa na tulikua tukishinda kila mashindano kuanzia kwata na shughuli nyingine nyingi namkumbuka Afande Sijali,Afande,Mrope,Swai.Pia namkumbuka Afande Wela wa kombania D huyu jamaa alikua katili wa kupindukia.Kwa upande wa wimbo naukumbuka wimbo huu oo msange...msange malaika....oo msange nitarudi
Mwashambwa aka LB (Last born). Haka ka bwana kalikuwa kanapenda chini ile mbaya........
Kwa wale waliopitia Oljoro miaka ya 1989/90/91/.. watakuwa wanaijua "SINDANO YA GANZI" ni Koplo mmoja alidumu sana pale A coy. Dah kumbukumbu ni nyingi, nazitafutia muda nije na mkanda wote.
Capt Mrimba alihamia Oljoro baadaye miaka ya 90.. kama sikosei na huko pia aliendeleza "tifu". Nakumbuka tukiwa kwenye "range" pana service mmoja alirusha "grenade" likashindwa ku-explode! Na kama ilivyo sheria ni lazima li-explode... Capt Mrimba alilifuata lile "grenade" akajaribu kulipiga bastola haliku-explode, hivyo ikabidi aliokote na kurirusha tena (by the moment kila mtu alisubiri li-explode mikono mwake), kwa bahati aliporirusha mara ya pili "booom". Huyu mzee alikuwa balaaaaaa kwelikweli.......
Hizo zilikuwa za Nyundo C coy Ruvu. Thank God mie nilikuwa Danger, na on top nilikuwa naq kitengo cha kudumu garage.Wanataaluma mnanikumbusha mbali sana tena . . .
Nakumbuka wakati wa kwata na kunyakua, kuna afande alikuwa analala chini kabisa akidai anataka kuhakikisha kuwa miguu yote inaenda na kushuka pamoja bila kupinda.
Ilikuwa balaa . . . Kunywa uji mwendo wa kunyakua, kula mwendo wa kunyakua nk.
Jamani tunatoka mbaaaaali kweli kweli. Sijui kama watoto wetu watakuja kupata hii experience . . . .
Tutaongelea mazuri yote ya JKT lakini tusichopenda kukiongelea ni msambazo wa UKIMWI na wenzetu (sana sana akina dada) waliokufa kwa kuambukizwa ukimwi na maafande wa darasa na saba. Hatutaki tuongelee juu ya ubakaji uliokuwa unafanywa na maafande ambao kwa namna moja au nyingine uliahalalishwa na serikali. Ukiuliza takwimu za waliokufa kwa kuambukizwa ukimwi wakiwa JKT zinatisha, uliza takwimu za maafande wanaokufa kwa ukimwi..mbaya mno...Hongera kwa aliyeamua kutoendelea na taratibu za JKT....we have lost enough manpower for our country.
Hizo zilikuwa za Nyundo C coy Ruvu. Thank God mie nilikuwa Danger, na on top nilikuwa naq kitengo cha kudumu garage.
Yaani hivi Visa vya JKT, kila unaposoma simulizi zake ni burudani tosha . . . . .
Kuna afande moja alihukumiwa na Court Marshall kisa kamlazimisha kuruta kushika kinyesi . . . . .
Nadhani JKT inaweza kufanywa kwa sasa kuwa Chuo Cha Mafunzo ya jeshi na Ujasiliamali wa Vitendo yaani kama Incubators.