Je, unajua tofauti kati ya social isolation (kujitenga kijamii) na health quarantine (kifungo cha afya)?

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Sasa tunaelewa social distancing? Nikuibie kiduchu:

- Working from home instead of at the office/kufanya kazi kutokea nyumbani. Hii mambo ya kila mtu kwenda ofisini tuache. Kwanza tunaenda kusoma magazeti na kuongelea Bunju Arena!

- Closing schools or switching to online classes/ kufunga mashule na vyuo na kuanzisha kutoa mafunzo kupitia mtandao. Badala ya kutumia vifurushi kwa soga tutumie vifurushi kusoma na kufundisha.

- Visiting loved ones by electronic devices instead of in person/Tutembelee wapendwa wetu kupitia vifaa vya electronic kama simu . Kwanza hata tukienda kuwatembelea kila mmoja anashughulika na simu yake na inaharibu maana ya kutembeleana.

- Cancelling or postponing conferences and large meetings/Kufuta mikutano isiyo na lazima. Mikutano mingine ni ya kuumizana tu! Mfano unaenda mkutano usio na kibali wakati wa janga la Corona.

- Ikibidi ukutane na wenzako hakikisha umekaa si chini ya futi 6 toka alipo mwenzako. Wataalam wa China wanasema hakuna maambukizi yaliyompata mtu nje ya futi 6! Ina maana walioenda kwa Olomide na siku Yanga inapiga nyama mwitu tarehe 8/3 walikuwa hawajui watendalo! Sema mungu ni mtanzania ama sivyo ingekuwa balaa!

Hii ni mifano tu ya social distancing aka kujitenga kijamii!

Baada ya kuelezea nini maana ya social isolation na namna ya kuitekeleza. Sasa tuangalie HEALTH QUARANTINE aka kifungo cha kiafya).

Kuna wengi wanachanganya mambo haya mawili. Na ukiyachanganya unaweza kuleta shida katika jamii au kushindwa kuzuia maambukizi.

Health quarantine inaweza kuwa kwa HIARI (Self/voluntary quarantine) au kwa kulazimishwa (forced quarantine).
Tofauti kubwa ni kwamba SOCIAL ISOLATION inafaa kwa mtu ambaye bado hana dalili au hajaambukiza wakati HEALTH QUARANTINE inamfaa aliyekwisha onyesha dalili au kuambukizwa.

Ni upumbavu kumweka au kumlazimisha mtu ambaye hana dalili au hajaambukizwa kwenye QUARANTINE! Psychologically na epidemiologically haisimami!

Somo fupi ila zingatia! Ndio maana haswa ya msemo TUSITISHANE KUPITA KIASI. Wa social isolation asilazimishwe kuingia kwenye KIFUNGO CHA KIAFYA! Sawa?
 
Back
Top Bottom