Je unaijua AMANA Bank, Inayokopesha bila Riba?

BISMILLAAHIR-RAHMAANIR-RAHIYM.
Imesemwa kuwa AMANA BANK ni Bank inayofuata sheria za Kiislamu. Katika sheria hizo kuna MLANGO wa biashara na fedha. Masuala ya njia za kuuza na kunua, vipomo, reahani (Bond) zawadi, ushirika, umiliki n.k yameelezwa katika kipengele hicho.
Katika kupitia kwangu baadhi ya Links nimeona kitu kikubwa kinachobishaniwa ni riba. Baadhi ya wachangiaji wanadhani kwamba Bank haziwezi kufanya kazi bila ya Riba!
Kwanza ni vizuri kuijuwa Riba Katika mtazamo wa Uislamu.
RIBA ni ziada ya mali inayoongezwa zaidi ya mali iliyokopeshwa. Mfano leo mtu anakopesha kilo moja au debe moja au shilingi mia moja lakini akataka mlipaji akija kulipa alipe zaiadi ya kilo moja, debe moja au shilingi mia moja. Na kuna baadhi ya watu kila unapochelewa kulipa wanaongeza kiwango cha riba (interest). Mfano anakopesha leo 100,000/= (laki moja kwa mwezi mmoja atataka riba ya asilimia ishirini (20%) na kama utachelewa kulipa inakuwa katika mtindo huu:
Mwezi wa 1 100,000 + 20% = 120,000
Mwezi wa 2 120,000 + 20% = 144,000
Mwezi wa 3 144,000 + 20% = 172,000 na kuendelea
Hapa utanona kuwa anayefaidika ni mkopeshaji na mkopaji ndiye anayenyonywa.
Tukumbuke kuwa Mtu hakopi ila kwa kubanwa na shida. Katika IMANI zetu na kanuni za Muumba inatakiwa kwamba mwnye nacho amsaidie asiye nacho ili DUNIA iwe sehemu bora ya kuishi kwa watu wote. Kwa kanuni hiyo tulitegemea kuwa Matajiri/Benki/Saccos/Viccoba n.k zisaidie kuwatoa watu katika udhalili kwa kuwakopesha MITAJI/BIDHAA bila ya RIBA. Kama tunjuavyo kuwa DINI zote zinakataza riba.
Katika uislamu kunaruhusiwa Biashara/Huduma.
Tuchukue mfano wa mkopo wa laki moja (100,000/=). Unapokwenda kutaka mkopo katika Bank za kiislamu watakuuliza unahitaji mkopo wa kufanya kitu gani. Wao wana mikopo tofauti. Mfano:
1. Biashara.
2. Ujenzi.
3. Masomo n.k
Kila mkopo una kanuni na taratibu zake. Kama ni biashara katika mkopo wa 100,000/= Bank wanaweza kukubaliana na wewe wakununulie bidhaa unazohitaji, halafu wanakuuzia kwa mkopo wakiwa wameweka faida yao, mfano 20%. mtakapokubaliana muda wa kurudisha mkopo huo yaani 120,000/= hakuna ziada ya malipo hata kama utachelewa kulipa ilimradi unawasiliana na bank na kuwapa taarifa ni kwa vipi unachelewa kurudisha mkopo waliokupa, ukitilia maanani kuwa wana dhamana yako uliyoweka kama 'BOND'
Na ujenzi ni mfano kama huo. Katika masomo na mfano wake kuna mikopo inaitwa KARDHATUN HASANAH (mkopo mwema) huu unakopeshwa bila ya ziada yoyote juu yake na inakuwa kwa kipindi maalum pamoja na dhamana (Bond)
Vilevile kuna bidhaa kama za USHIRIKA WA KIBIASHARA, UDHAMINI na huduma zote halali zinazoingiza faida.
Hii ni kusema kwamba kuendesha Bank/Saccos/Vicoba inawezekana kama tukiweka mbali UFISADI.
 
Amani ya bwana iwe juu yenu , swali kwenye mada hii je ukiwa hauna collateral yoyote nikiwa namaanisha assets , ila unafanya kazi kampuni binafsi, na unautambulisho wa uhakika ikiwa ni pamoja na kitambulisho cha Taifa je unaweza kupata mkopo unaohitaji kwa pato la mshahara wangu wa kila mwezi bila kumuhusisha mwajiri kwasababu mwajiri hayupo tayari kutoa udhamini, wassalamu
 
Kwa nini wasiwasaidie waislam wenzao kwani ndio most illiteracy?
Ama kweli fadhila mfadhili mbuzi binaadam...wangesema ni kwa waislam tu ungesema wabaguz na kila maneno..kama hauko interested si uache tu hawajalazmisha wametoa milango kwa yeyote analiyeinterested akajiunge..sio vizuri kuweka choko choko za udini hata pasipostahiki.
 
Amana Bank nawapongeza sana kwa kuendelea na utaratibu bora kwa misingi Ya UISLAM.
Lakin mimi binafsi nahitaji kukopa nasikia mnakopesha viwanja je ni kweli kama ni kweli utaratibu upoje?

Ahsanteni
 
hawa jamaa mikopo yao mingi ime base kwenye vitu,mfano kama unataka mkopo kwa ajili ya kujengea shule,wao hawakupi hiyo pesa wao wanaenda kukujengea shule watakukabidhi shule ikiwa imekamilka na pale wewe utakapoanza kusajili hao watoto ndipo pale utaanza kurejesha marejesho yao,wao wana asdume wanaweza kukupa pesa ukaitumia kwenye kitu kingine ambacho sio kusudiwa,sasa wataanzaje kukukata marejesho wakati hata pesa yenyewe haijaanza kufanya kazi iliyokusudiwa,ni dhulma.Benk zingine wanachokifanya wakikupa ile pesa hapohapo na makato yanaanza haijarishi umeitumiaje ile pesa,sasa kama wao walikujengea shule kwa milion hamsini labda wakakwambia utarejesha milioni 55 hii milioni tano ni faida sio riba maana kuna charges mbalimbali zilikuwa zinatumia wakati wa ujenzi wa shule kama kulipa walinzi nk,mafuta ya kwenda site,kifupi nenda watakuelekeza,jinsi gani wao wanapata faida nk,mambo ya kubuni biashara alafu wao wankatoa mtaji mkagawana faida nk,ila kuna tofauti kati ya faida na riba
 
u
Okay kwahio works like mortgage.., je wakati nalipia hizo 6m (lets say kiasi fulani kila mwezi) je takuwa ninatumia lile gari.. (naishi kwenye hio nyumba ?) na siku nikishindwa kulipa required amount katika mwezi fulani, Je ninanyanganywa hio nyumba / gari na kupoteza zile amount ambazo nimelipa mpaka sasa ?

Kama ni hivyo I can understand in terms of property.., Je kama nataka finance za kwenda kujengea bar au kununua machungwa ili niuze (how can this work..) wananianzishia biashara au ?
utakuwa unalitumia,wao wataagiza gari na kushughulika kila kitu kama insurence,TRA nk,sasa bila hivyo mkuu watakukata marejesho toka wapi?
 
Back
Top Bottom