Je, Rais Kikwete amemaliza ubishi wa Dowans au amechelewa?

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amepigilia msumari wa mwisho katika jeneza la mzozo juu ya ununuzi wa mitambo ya kufua umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited, aliposema kuwa serikali haitanunua mitambo hiyo kama Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilivyo tangaza.



Akizungumza na wananchi katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Machi, mwaka huu kupitia vyombo vya habari juzi, Rais Kikwete alisema serikali haitabadili msimamo wa Tanesco juu ya ununuzi wa mitambo hiyo na kwamba, inajitahidi kukabiliana na tatizo la umeme, hivyo kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi kwani nchi haitaingia gizani.


Tunashukuru kusikia kauli ya mwisho ya rais juu ya suala hilo ambalo lilizua utata mkubwa na kuibua mjadala uliozua maswali mengi yaliyoihusisha moja kwa moja serikali kuwa iko nyuma ya mpango huo na hasa baada ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tanesco, Dk Idris Rashid kusema kuwa nchi ikiingia giza kutokana na kutonunua mitambo hiyo shirika lake lisilaumiwe.

Hata hivyo, tunasema rais amechelewa kumaliza mzozo huo ikizingatiwa kuwa sakata la mitambo hiyo ilivyoingia nchini alikuwa analifahamu kwa kina pamoja na wasaidizi wake; akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngereja kuonyesha kuunga mkono pendekezo la Tanesco la kuinunua badala ya kumshauri achukue hatua ya sasa mapema, ili kuzuia mjadala na malumbano yaliyotokea.


Ni ukweli usiopingika kwamba, mjadala wa mitambo ya Dowans ulitaka kuchafua hali ya hewa baada ya wanasiasa kuiingilia, lakini kwa hatua hii ya sasa tunampongeza rais kunusuru; tukiamini kwamba, huo ndiyo mwisho na hakutakuwa na njia yoyote itakayolifufua suala hilo kupitia mlango wa nyuma.


Tunasema hivyo kwa sababu, Watanzania wa siku hizi wameelimika kupita kiasi; kwani wakishindwa jambo hawakati tamaa, hutumia hila na mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa azma yao inafanikiwa.

Kwa sababu hiyo, tunamtahadharisha rais kuwa makini na watu wa namna hiyo ambao baadhi yao wanaweza kupitia kwa wasaidizi au washauri wake kufanikisha mambo yao na mwisho wa safari lawama zote kumwendea yeye kwamba, hakuwa makini. Pia tunasisitiza kwamba, washauri wa rais wafanye kazi yao kikamilifu kwa kumpa ushauri unaofaa na kwa wakati muafaka.

Source:Mwananchi Read News
 
Hili la Dowans ndiyo kwanza limeanza na hawa wanaodai Kikwete kapilia msumari wa mwisho naona bado hawajui kuzisoma alama za nyakati. Mjadala wa Dowans utafungwa vipi wakati 'hatujamjua' mmiliki wake ni nani? Pili hii kampuni bado inadaiwa na Serikali/TANESCO shilingi 23 billioni walitakiwa waridishe shilingi 30 bilioni lakini hadi sasa wamerudisha bilioni 7 tu sasa mjadala wa Diwans Kikwete anashinikiza ufungwe kwa maslahi ya nani? Ya Watanzania au ya wamiliki wa Richmond/Dowans?
 
Back
Top Bottom