Raila Odinga aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Kenya ni rafiki mkubwa wa John Pombe Magufuli.
Wakati wa kampeni za uchaguzi nchini Kenya, wakati huo Raila Odinga akiwania urais wa Kenya kwa Muungano wa ODM, John Pombe Magufuli alikwenda nchini Kenya na kupanda majukwaani kumnadi mgombea wa ODM, Bwana Raila Odinga.
Alipoulizwa John Pombe Magufuli kama yeye akiwa waziri wa SMT, nchi jirani kabisa na Kenya kwenda kumnadi mgombea wa chama kimojawapo nchini Kenya, sio kwanza kuifarakanisha Kenya na Tanzania, lakini pia kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine?
John Pombe Magufuli alikiri kwenda Kenya na kumfanyia kampeni rafiki yake Raila Odinga. Lakini John Pombe Magufuli alijitetea kwamba alikwenda Kenya kama Pombe Magufuli na wala sio kama Waziri wa SMT.
Baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya Bwn. Raila Odinga alishindwa na mgombea wa Jubilee Bwn Uhuru Kenyatta ambaye sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Kenya. Huku Bwn Raila Odinga wa ODM akiwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani Kenya.
Swala la kujiuliza, Je Bwn Raila Odinga atakuja naye kumpigia kampeni mgombea wa CCM ambaye ni rafiki yake wa siku nyingi bwana John Pombe Magufuli?
Kama John Pombe Magufuli na Raila Odinga wana mambo ya kufanana, Je hiyo ni ishara pia kwamba John Pombe Magufuli naye atashindwa na Lowassa mgombea aliyetoka chama tawala na kuhamia upinzani i.e. muungano/ushirikiano wa UKAWA?
Kumbuka Uhuru Kenyetta akiwa mgombea wa Jubilee alimuangusha Raila Odinga aliyekuwa waziri mkuu kwenye serikali iliyokuwa inamaliza mda wake.
Historia ya John Pombe Magufuli inakwenda kuandikwa kama ilivyokuwa historia ya rafiki yake mkubwa Bwn Raila Odinga wa Kenya.